Maalim Kuridhia huu uhalisia (Shairi)

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Mabibi na mabwana Maalim karidhia serikali ya umoja wa kitaifa. Pamoja na yote Maalim si wa kubeza.

Karibuni kwenye mwendelezo wa tungo hizi waungwana:

IMG_20201207_102726_791.jpg


IMG_20201207_102905_755.jpg


IMG_20201207_103316_751.jpg


Ninaamini Seif kaipigania Zanzibar mara zote katika namna ambayo hawapo wazanzibari wanaoweza kujinasibu zaidi yake.

Asili ya uzi huu ilikuwa mwendelezo wa huu mwingine:


Naomba kutoa hoja.

Cc: Senzighe wa Senzighe
 
Nakukaribu Senzige, rasmi sasa ni hapa,
Tukihamishe kilinge, kusongesha tuloapa,
Wazandiki tuwanange, bazazi watoke kapa,
Hongera Sefu Hamadi, Vita sasa humo humo!

Vita sasa mumo mumo, hongera bwana Hamadi,
Walidhani huna kimo, wakuchomeshe mahindi,
Itahitajika Omo, kuusafisha ushindi,
Ndani sasa yuko Sefu, pa kuficha pawe papya!
 
Nikweli kapigania, haki zenu visiwani
Lakini amezingua, kujiunga na shetani,
ukweli tumeumia, wale tulio amini
Sitapiga tena Kura,udhwalimu sitamani


Kwa leo nakwama hapa, ACT ni takataka,
Ulafi wa madaraka, ndio mana tupo hapa,
unapewa mamlaka, Haram kuitakasa,
Wengi matumbo ya paka,ukiwamini utalia
 
Nikweli kapigania, haki zenu visiwani
Lakini amezingua, kujiunga na shetani,
ukweli tumeumia, wale tulio amini
Sitapiga tena Kura,udhwalimu sitamani


Kwa leo nakwama hapa, ACT ni takataka,
Ulafi wa madaraka, ndio mana tupo hapa,
unapewa mamlaka, Haram kuitakasa,
Wengi matumbo ya paka,ukiwamini utalia

Kunguru bwana sikia, vita ni kama mchele,
Ule mnaoshushia, katika sherehe zile,
Ni mengi wakupikia, usishindwe wewe kale!
Mchele huwa mmoja, lakini mapishi mengi!

Katika mapishi mengi, Sefu kachagua moja!
Mimi wewe sikupingi, wala yeye sina haja,
La kheri tuwapo wengi, tunufaike kwa hoja,
Namkaribu Senzighe, kwa mambo haya ya tija!

Kwamba Sefu yumo humo, pakuficha pawe papya,
Nionavyo hoja imo, kwani Sefu siyo mpya,
Sefu kama mwana Sumo, mbona atawachachafya?
Hongera Sefu Hamadi, vita sasa humo humo!
 
Kunguru bwana sikia, vita ni kama mchele,
Ule mnaoshushia, katika sherehe zile,
Ni mengi wakupikia, usishindwe wewe kale!
Mchele huwa mmoja, lakini mapishi mengi!

Katika mapishi mengi, Sefu kachagua moja!
Mimi wewe sikupingi, naye pia sina haja,
La kheri tuwapo wengi, tunufaike kwa hoja,
Namkaribu Senzighe, kwa mambo haya ya tija!

Kwamba Sefu yumo humo, pakuficha pawe papya,
Nionavyo hoja imo, wala Sefu siyo mpya,
Sefu kama mwana Sumo, mbona atawachachafya?
Hongera Sefu Hamadi, vita sasa humo humo!
Kukubali jambo hili, yataka moyo kwakweli
Wamekufa watu wengi, kujeruhiwa hatari
Wamepigania mengi,kujitoa kwao tusijali ?
Uonevu na hu wizi, unataka tukubali?


Nikua demokrasia, udhwalimu kukubali
Tutakuja kujutia, nayo kwambia ya kweli
Brazaj utajalia, unovu ukikithiri
Tusichoke kupigana, kuupinga udhalili


Sipendi kula haramu, hilo naomba fahamu,
Tumeona nyingi damu, nini usichofahamu?
wanafanya na karamu, wanyonge na zetu damu
Naweka chini kalamu, Nani atawa hukumu ?
 
Kukubali jambo hili, yataka moyo kwakweli
Wamekufa watu wengi, kujeruhiwa hatari
Wamepigania mengi,kujitoa kwao tusijali ?
Uonevu na hu wizi, unataka tukubali?


Nikua demokrasia, udhwalimu kukubali
Tutakuja kujutia, nayo kwambia ya kweli
Brazaj utajalia, unovu ukikithiri
Tusichoke kupigana, kuupinga udhalili


Sipendi kula haramu, hilo naomba fahamu,
Tumeona nyingi damu, nini usichofahamu?
wanafanya na karamu, wanyonge na zetu damu
Naweka chini kalamu, Nani atawa hukumu ?

Kunguru nina kusoma, hata mimi ninalia,
Yatakikana hekima, usiwahi kurukia,
Kule Zenji husimama, alipo wana mjua,
Mikononi mwake Sefu, Jahazi liko imara!

Kumbuka katoka kafu, leo yuko wazalendo,
Hata huku akikifu, hapungukiwi uhondo,
Zenji mambo si sarafu, kama makwetu kibondo,
Mikononi mwake Sefu, Jahazi liko salama!

Hata kama angesusa, kwani ipo tofauti?
Kaendelea kuasa, tuwaweke mtu kati,
Waliofanywa asusa, ni moja ya yale nyeti,
Tumpe Sefu nafasi, mapambano ndiyo kwanza!

Cc: Senzighe wa Senzighe
 
Back
Top Bottom