Pongezi Lissu, Maalim na upinzani kwa ujumla kuyathamini maisha ya Watanzania

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,026
2,000
Mabibi na mabwana ni asiye na macho tu ndiye anayeweza kudhani palikuwa na uchaguzi hapa kwetu na kuwa eti matakwa ya wapiga kura yameheshimiwa.

Ndani ya nchi watu wako kimya si kuwa wote wameridhika au waliridhika na mwenendo wa uchaguzi huu. Mbaya zaidi idadi ya watu wenye manung'uniko na uchaguzi huu si kidogo wala kubeza.

Kunalalamikiwa uhalali wa uchaguzi, wizi, matumizi ya nguvu, uuwaji, utekaji, unyanyasaji, kukandamizaji, nk.

Kwamba Uganda tayari pana marehemu 37, Majeruhi 60 kati yao 48 wakiwa na majeraha ya risasi (kwa sababu ya harakati za uchaguzi huu) na kwetu haikuwa hivyo, washukuriwe sana Lissu, Maalim, na upinzani kwa ujumla kwa kitupishilia mbali na madhila kama hayo.

Kwa hakika waliotuvusha salama ni Lissu, Maalim na upinzani kwa ujumla. Hawa kama yule mama mwenye mtoto mbele ya mfalme Sulemani hawakuwa tayari kumvutania mtoto.

Lissu, Maalim na upinzani japo kwa shingo upande waliamua kuwaacha majahili kufanya yao kwa kila mtu kuwabaini. Kwa hakika walikuwa na wanao uwezo wa kukinukisha vilivyo. Lakini jamani maisha ya watu hayana thamani kiasi hicho?

Polisi Uganda na watawala Uganda kama ilivyo kwetu, wako tayari kumvutania mtoto eti kuonyesha kuwa mtoto ni wao.

Kwa kiu ya madaraka yao iliyopitiliza wako tayari hata kuuwa watu. Pathetic!

Kwamba hayakutokea maafa zaidi, busara za viongozi wetu hawa na zishukuriwe sana. Linganisha na upande wa pili njaa yao ya madaraka ni kubwa kupitiliza hata kama ni kwa kuuwa watu, wako tayari! Jambo la aibu sana.

Kama ilivyo Uganda sisi pia tumekuwa wa kunyooshewa vidole na wote wapenda haki wakiwamo jumuiya za kimataifa kuwa mamlaka zetu ni mijizi, miuaji, isiyojali haki za binadamu, isiyoheshimu uhuru wa watu wake nk, nk.

Nakazia, washukuriwe sana Lissu na Maalim Seif kwani bila ya busara na ustahamilivu wao usio kipimo katika mazingira magumu, baadhi yetu tu hai hata leo.
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,088
2,000
Acha uongo, wananchi waliwapuuza tu hao wabwatukaji. Lissu alisema ataingiza watu barabarani badala Yake kaingizwa yeye na beberu lake Amsterdam, wakaitisha màandamano yasiyo na kikomo, FFU wakasubiri wachumba hawakutokea, watanzania tulimwelewa Magufuli, Lissu na beberu lake wanahangaika na ICC.
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
4,587
2,000
Pongezi kwa watanzania walio amua kuwapuuza wapinzani wenye uroho wa madaraka walio dhani kwamba uchaguzi huru na haki maana yake ni wao lazima wapate ubunge wakafaidi na familia zao.

Wameanza kuwapuuza kwenye sera zenu za matusi

Wakawapuuza kwa kulinda Kura vituoni

Kisha wakawapuuza kwenye wito wa maandamano ya kutetea matumbo ya wanasiasa.
 
Bandiko limetambua kuwepo wa watu kama wewe wasiokuwa na macho. Kumbuka kutokuwa na macho ni tofauti sana na kuwa kipofu.

Hawakukinukisha walipoenguliwa wagombea wao. Hawakukinukisha walipokuwa wakiwekewa mizengwe wakati wa kampeni. Hawakukinukisha kura za mabegi zilipokuwa hadharani. Nk, nk.

Hawakukinukisha wakati uwezo huo walikuwa nao tena ukiwa mkubwa kweli kweli.

Waulize kina Jiwe, Chirro na washirika wao watakwambia.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,026
2,000
Pongezi kwa watanzania walio amua kuwapuuza wapinzani wenye uroho wa madaraka walio dhani kwamba uchaguzi huru na haki maana yake ni wao lazima wapate ubunge wakafaidi na familia zao.

Wameanza kuwapuuza kwenye sera zenu za matusi

Wakawapuuza kwa kulinda Kura vituoni

Kisha wakawapuuza kwenye wito wa maandamano ya kutetea matumbo ya wanasiasa.

Amefikisha 37 vifo kabla ya uchaguzi. Huyo ni mshirika wetu kindakindaki anayefuata nyayo zetu. Anafanya kama tulivyofanya na kuita tumeshinda kwa kishindo.

Alikuwapo pia physically kutupongeza kwenye kuapishwa kwetu.

Kina Lissu na Maalim hawakupuuzwa bali wanaungwa mkono mno kama wanavyoungwa mkono pia na jumuiya zote za kimataifa na pia wapenda haki wote.

Kwamba hawakukaza msimamo hata kama watu wanauawa na majahili hawa - na washukuriwe sana!
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,026
2,000
Aibu zaidi kwa majahili kama M7 zenji badala ya kukaa nchini kufanyia kazi hatima yao, bwana yule anasema kawapa ACT nafasi 2 za u naibu waziri na nafasi ya umakamu wa rais.

Kwa uchaguzi upi?! Hatima ya Zenji iko mikononi mwa wa Zenji. Haramu haijawahi kuwa halali.

Ama kweli majahili kufaidi hadi siku ya Idd!

Ngoja Kyaguranyi atoe somo. Seems very soon somo litaeleweka la namna sahihi ya kushughulika na madikteta!
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
4,587
2,000
Amefikisha 37 vifo kabla ya uchaguzi. Huyo ni mshirika wetu kindakindaki anayefuata nyayo zetu. Anafanya kama tulivyofanya na kuita tumeshinda kwa kishindo.

Alikuwapo pia physically kutupongeza kwenye kuapishwa kwetu.

Kina Lissu na Maalim hawakupuuzwa bali wanaungwa mkono mno kama wanavyoungwa mkono pia na jumuiya zote za kimataifa na pia wapenda haki wote.

Kwamba hawakukaza msimamo hata kama watu wanauawa na majahili hawa - na washukuriwe sana!
Kina nani walio muunga mkono?

Hawa walio mpa kura mil 1 au wepi?

Hawa walio goma kulinda kura vituoni ?
Hawa walio goma kuingia barabarani kwenye maandamano yasio koma?

Au wale wenyeviti wa vile vyama viwili na viongozi wenzao walio itisha yale maandamano walikuwa wanafanya igizo pale?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,026
2,000
Kina nani walio muunga mkono?

Hawa walio mpa kura mil 1 au wepi?

Hawa walio goma kulinda kura vituoni ?
Hawa walio goma kuingia barabarani kwenye maandamano yasio koma?

Au wale wenyeviti wa vile vyama viwili na viongozi wenzao walio itisha yale maandamano walikuwa wanafanya igizo pale?

Ni kwa kutambua kuwepo wasio na macho kama wewe bandiko liliweka angalizo hilo mahsusi?

Milioni moja unawahesabia wapi? Kwa uchaguzi upi? Uchaguzi wa wizi?

Waliogoma kulinda kura unawahesabia wapi? Kwa hiyo kumbe unajua kura kura hazikulindwa kwa mashinikizo bali kama kwa mabucha, mafisi yaligeuka walinzi?

Waliogoma kuingia barabarani ni hawa ambao wanakesi za ugaidi, kutakatisha pesa, wengine walioko bado korokoroni na wengine sasa ni wakimbizi?

Maigizo yapi unayoongelea, au yale ya usafi nchi nzima au propaganda za vitisho za mamlaka na pia kupitia media?

Ewe usiokuwa na macho yaliitishwa maandamano ya amani ambayo mlitaka kuyafanya kuwa ya shari ili mpate sababu za kuwatoa watu roho kama anavyofanya quarter pin?

Subirini Kyaguranyi amalizane na dikteta wake. Kwani yule aliyesihi kushangilia kwa staha hakuyajua ya Kyaguranyi?

Hayapo marefu yasiyo na ncha jombi.

Twala pop corn hapa, macho yote kwa Bobi Wine kwanza, darasa tosha (on job training - OJT). Eeh mola wetu na ukamsimamie moja wako Bobi Wine katika kuwakomboa watu wako toka katika makucha ya dikteta fedhuli bwana yule.

Tafadhali ukazisikie sala zetu.
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,767
2,000
Huwa mnajifaragua tu nyie jamaa ila ukweli ni kwamba hakuna mpinzani Tz kwa sasa mwenye influence kama Wine.

Maandamano yakipigwa marufuku Kampala lazima yawepo.

Wine ana wafuasi ambao ni real siyo ghost supporters wa bongo.

Mara zote Wine akitiwa ndani Kampala inachafuka hapa kwetu Jf na twitter ndo huchafuka.

Viongozi karibia wote top wa upinzani wametiwa ndani bongo ila hakuna hata kenge tu mtaani achilia mbali watu kuonekana.

Pongezi ziende kwa Watanzania wenyewe na vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Mkuu wewe uko upande gani? Au wewe ni mboga mboga kindaki ndaki?

Uko tz hii hii wewe? Hujui kuna watu wamekufa, wako mbaroni au ni majeruhi mikononi mwa majahili hawa? Au ndiyo kurejelewa kutoka sayari nyingine?

Kwamba yakipigwa marufuku Kampala lazima yawepo? Hapo ndipo kwenye shukurani kwa wapinzani kwa kuepusha shari hadi sasa (so far) hapa kwetu.

Hii ni kwa sababu ule upande wa mboga mboga kama ilivyo Uganda wako tayari kuvutania mtoto - wako tayari kuuwa!

Tofauti hiyo ya upinzani huku ndiyo msingi wa mada - "pongezi kwa upinzani kwa kulinda maisha kuliko vyote." Mategemeo yaliwahi majahili kubadilika kwa kheri. Hata farao ilikuwa hivyo hivyo.

Hata hivyo, yote yana mwisho. Kyaguranyi na a endelea kutoa somo - popularly known as OJT.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom