Maalim Seif, jembe la Zanzibar

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,812
35,803
Mabibi na mabwana si busara sana kuukimbia ukweli. Ukweli ni mchungu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Au nasema uongo ndugu zangu?

Kumekuwa na mengi kuhusu ACT na Maalim Seif hasa baada ya kujiunga SUK.

Ufuatao ndiyo ulio ukweli kuhusiana na jembe hili la Zanzibar.

Maalim Seif kaipigania Zanzibar maisha yake yote. Angali anapigana na ataendelea inshallah (mola apishilie mbali) hadi kifo kitakapo mtenga.

Kuipigania kwake Zanzibar ndipo kunakompa hii credibility au kupendwa aliko nako. Ni umaarufu huo ambao pia ndiyo iliyo sababu kuu ya yeye kuibiwa kura na mahasimu wake kila uchao.

Alipo Seif wapo!

Alikuwa CUF yuko ACT hata akienda TADEA au wapi watakuwa naye huko.

Zanzibar ni kipaumbele chake. Si Bara. "Mtu kwao" na "mcheza kwao hutunzwa."

Akiitisha Seif hata leo kule Zanzibar kitanuka. Tofauti kubwa sana ya kule na Bara. Huyu gwiji ana msingi uliojichimbia barabara chini ya ardhi.

Pana tofauti kubwa ya Maalim Seif kama binadamu na ACT kama chama. Huu nao ni ukweli mchungu. ACT ni chama imara ushukuriwe uwepo wa Maalim. ACT ni butu kama CUF bila Maalim. Profesa anaweza kuuthibitisha ukweli huu.

Maalim ni mpambanaji mzoefu. Huyu ana mbinu na uwezo wa mapambano kuliko majenerali wengi. Kumbeza Maalim ni kukosa kumtambua vyema wala kutambua agenda yake iliyokuu.

Kumhusisha Maalim na ukosefu wa haki kule Kagera au Rukwa ni kutojitendea haki sisi wenyewe.

Mambo ya Ngoswe huachiwa Ngoswe mwenyewe!

Kila mtu na apambane na hali yake. Maalim anapambania Zanzibar na anaowapigania wamempa ridhaa hiyo.

Kwenye hili si CCM wala awaye yote Bara anaweza kujidhania kashinda au kashindwa au hata kasalitiwa. Busara ni kukubali kutokubaliana.

Udumu Maalim Seif jembe la ukweli la Wazanzibari!
 
Huyo ndio basi tena , yeye na Zitto they are politically finished like Lipumba , nobody could listen to them again .

Mkuu Zanzibar si Bara.

Alipo wapo!

Wala hii issue kumvesha Zitto ni kumpa umaarufu asiokuwa nao.

Ukweli mchungu.
 
Sasa ACT mnaanza kunivuruga akili,mmekosa urais sasa hata umakamu muukatae?mlitaka seif afanye nn,mnaujua nyinyi umakamu!!!
 
Sasa ACT mnaanza kunivuruga akili,mmekosa urais sasa hata umakamu muukatae?mlitaka seif afanye nn,mnaujua nyinyi umakamu!!!

Kudhani ACT wamekosa urais ni kujidanganya.

Aliyekosa urais ni Seif. Tofautisha Seif na ACT kuweza kutambua.

Usisahau Seif ni mgombea wa ZEC wala hajawahi kuwa na pressure na NEC.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kuna kitabu kimoja cha masimulizi nilikisoma zaidi ya miaka 20 iliyopita, ndani yake kuna simulizi ya "Mdomo uliponza kichwa" Nikiitafakari simulizi hiyo moja kwa moja inanasibiana na Maisha ya huyo unaemuita jembe! Kiufupi ni kwamba awe jembe awe trekta "mdomo wake umeponza kichwa chake" hivyo amekosa credibility machoni pa Wazanzibar, ni mwongo wa kisiasa mnafiki kwa vitendo na pia ni mbabaishaji. Na ukifuatilia wengi wa wanaomuunga mkono ni wale wanaonasibiana nae kwa udugu wa damu au kwa Kisiwa alipozaliwa.
Kumbuka pia jembe haliwezi kufanya kazi bila kutiwa mpini!.

Unaandika tokea pande za wapi jombi?

Kama credibility Seif kakosa Bara si huko ambako hata kesho akitaka kinuke kinanuka kikamilifu.

Ukweli mchungu, Seif ni mwana halisi wa Zanzibar!

Hilo jembe limekamilika na mpini wake. CCM na wapinzani way forward hapo ni kukubali kutokubaliana.

Kwa Seif - anapigana kama anavyotaka yeye na watu wake huko kuliko ZEC si kuliko NEC.
 
Siasa za kumfuata mtu nyuma karne hii sio za kujisifia hata kidogo, mtu mmoja au kikundi cha watu kinaweza kutumbukia shimoni na ninyi wengine wote mkatumbukia.

Yaani mtu mzima na akili zako timamu ndugu yako abakwe, au apigwe, au achomewe nyumba yake, halafu uje kuimba hapa Seif ni jembe, utakuwa na mtindio wa ubongo, huko ni zaidi ya kuwa msukule.

Unaweza vipi kuikana familia yako au ndugu zako kwa ajili ya mtu baki?!

Nyie mmelogwa. Kwa akili zenu hizi huyo Seif ataendelea kuwachezea kama vitenesi.
 
Siasa za kumfuata mtu nyuma karne hii sio za kujisifia hata kidogo, mtu mmoja au kikundi cha watu kinaweza kutumbukia shimoni na ninyi wengine wote mkatumbukia...

Alipo wapo huo ndiyo ukweli mchungu. Kumbuka si kwa uzuri wa sura yake au huruma.

Huyu ni self made. Ameweza kukoga nyoyo za watu. Hata kina Mandela (rip), Chris Hani (rip) , Winnie Mandela (rip), Nyerere (rip) nk walijijengea uhalali kama huo.

Ukweli mwingine mchungu Lissu yuko huko huko. Palikuwa na mkanganyiko kidogo pale CDM hii ngoma ilikuwa imesha kwisha!
 
Kujua upande nitokako wala sio shani, huyo mzee ni mchonganishi na ndicho kilichomkosti hadi leo hii, Marehemu mzee Jumbe hadi amefika kufariki hakutoka nje ya Kigamboni sababu ni huyo, leo hii aaminike na Wazanzibari. Pole sana!!

Utokako kama ni kibondo, Seif huko siyo kipaumbele. Huyu ni ZEC si NEC.

Wapi uko ni muhimu sana jombi na ndiyo maana visiwani ni Maalim kama primary ACT ni secondary.

Huo ndiyo ukweli mchungu.

Inaitwa shusha tanga pandisha tanga!

Ndiyo maana ya alipo tupo.
 


Mkuu BAK heshima kwako. Kwa nini Seif aliamua kusitisha kukinukisha hadi mwisho?

Jibu ni hili hapa chini:

Seif alishuhudia kwa macho yake kipigo walichopata kina Jussa, Mazrui na wenzao walipokuwa wamekamatwa. Wakiwa hawajaonyesha resistance yoyote kwenye kukamatwa kwao. Hii achilia mbali wale waliouawa.

Seif aliiona police brutality in real sense, ambayo kwa maneno yake alitamka kuwa hakuwahi kuona udhalimu kama ule.

Seif hakupigwa lakini kwa kuchelea madhara zaidi kwa watu waje kwa wakati ule aliiona "it was not worth it."

Hii ni kama ya yule mama mwenye mtoto na mfalme Suleiman.

Mwenye mtoto kuokoa maisha ya mwanawe alikuwa tayari kumwachia mtoto kwa mama mwingine badala ya kumvutania. Hii ikiwa against all the odds!

Kwa kuokoa maisha ya watu wake Seif aliamua kama hicho kitaokoa maisha kwa watu wake akiangalia uwezekano mwingine kwa wakati huo, bora iwe hivyo.

Lissu alikimbilia ubalozini kwani mwenyewe alisema heri kuwa hai ukipambana kuliko kuwa mfu. Ambayo ni logical.

It is not over yet hiyo ni strategical retreat.

Acceptable kwenye uwanja wa vita.
 
Nchi hii inachekesha sana,waliokuwa wanamshangilia Maalim saizi wanamchukia na kumtolea maneno magumu magumu,wakati wale waliokuwa wanamtusi saizi ndiyo wanamsifu na kumshangilia.

Siasa ni unafiki mkubwa sana.
 
Nchi hii inachekesha sana,waliokuwa wanamshangilia Maalim saizi wanamchukia na kumtolea maneno magumu magumu,wakati wale waliokuwa wanamtusi saizi ndiyo wanamsifu na kumshangilia....
Siasa sio unafiki, wanasiasa wanaoongozwa na matumbo yao ndio wanaiharibu siasa, na mbaya zaidi wakiwa na wapiga debe wasiojitambua.

Wapo watu perfect wameifanya siasa dunia inawaheshimu, the likes of Mandela, Patrice Lumumba and so forth.
 
Huko unakosema alipo wapo mimi ni mzawa, kilichopo naendelea kukushangaa wewe! Unaeongelea ambacho hukijui. Zanzibar serikali yoyote inaundwa na baraza la mapinduzi hivyo sahau!
Hilo jembe lako katilishe mpini ukalimie mahindi.

Ulishasema haijali uko wapi mara umekuwa mzawa.

Malumumba wenzio wako mashimoni.

Usisahau hamuwezi kutudanganya wote siku zote.

Alipo tupo!
 
Ni msaliti tu na mchumia tumbo huyo hana jipya. Yeye, Zitto na wengine wachache wameshikishwa mshiko mnene sasa wamekaa meza moja na dhalimu kwa uongo kwamba wanachama wao waliunga mkono maridhiano na wauaji. Kitu ambacho si cha kweli.
Mkuu BAK heshima kwako. Kwa nini Seif aliamua kusitisha kukinukisha hadi mwisho?....
 
Bwana mdogo! Humu mimi siko upande wa Lumumba wala Ufipa!
Bahati nzuri huyo unaemuongelea namfahamu mpaka kwao Zanzibar, kisiwani Pemba, Wete, Mtambwe, Nyali. Sasa we endelea kuropoka tu!

Usitufokee wala kututisha jombi. Kila mtu anaufahamu wake.

Ndipo dhana ya kukubali kutokubaliana inapokuja.

Hii ni kama tunavyotambua uwepo wao hata mapanya walio mashimoni bado.
 
Ni msaliti tu na mchumia tumbo huyo hana jipya. Yeye, Zitto na wengine wachache wameshikishwa mshiko mnene sasa wamekaa meza moja na dhalimu kwa uongo kwamba wanachama wao waliunga mkono maridhiano na wauaji. Kitu ambacho si cha kweli.

Dhana ya kukubali kutokubaliana ni imara sana.

Apewe muda Maalim Seif inaweza kuwa mapema mno kumhukumu. Utenzi huu una husika:
IMG_20201215_003105_016.jpg

IMG_20201215_003134_112.jpg


Yote hii tokea kwenye uzi huu:

 
  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom