BAKWATA KIDONDA KIPO MGUUNI DAWA MNAWEKA MACHONI !
Na Maalim KONDO BUNGO
Nikweli tunafahamu kwamba Bakwata haijawahi kupingana au kutofautiana na Ccm na Serikali yake hata mara moja hata pale Serikali inapofanya matukio yanayo onesha kuwadhuru waisilam.
Tumeona mwaka 1993 waisilam ( wahadhiri ) wa kiisilam walipofungwa kwa kusingiziwa wamevunja Bucha za nyama ya Nguruwe Bakwata walikua upande wa Serikali.
Ni Taasisi ya Barukta tu chini ya Sheikh Yahya Huseyn (marehem ) ndiyo ilikua pamoja na Wahadhiri.
Mauaji ya Mwembechai pia Bakwata ilikua upande wa Serikali bila ya kujali vifo vya waisilam kila kilichosemwa na serikali ndiyo ilikua sauti ya Bakwata.
Waisilam waliuwawa walikaa magerezani, madai ya Mahakama ya Kadhi waisilam walifikia hatua nzuri katika kuibana Serikalini lakini wakatumika bakwata kuuvuruga mchakato huo kwa kuunda Mahakama ya kadhi kinvuli ili kuufuta kabisa mchakato huo.
Mauaji ya waisilam kibiti Bakwata haikusema chochote wapo waliopewa kesi za Ugaidi za kusingiziwa bakwata kama chombo kinacho jiita cha kiisilam wameshindwa kusema chochote ya mateso hayo ya waisilam.
Kupigwa risasi Sheikh Ponda Sheikh Alhadi Mussa pekee kwa nafsi yake mwenyewe ndiyo alitoa tamko la kusikitishwa na baadae inasemekana alionywa na wakubwa zake na hakurudia tena.
Siwezi kuyasema yote nitajaza vitabu na sito yamaliza,
Kuhusu Maandamano ya October 29 kama ningejua watakacho kisema kabla ya kukisema ningewashauri wasiseme maana walicho kidhihirisha katika jamii ni uelewa dhaifu au uchawa ulio pitiliza na kuitumikia Serikali kwa kimvuli cha Dini.
Naona mitandaoni kiwango kikubwa cha mashambulizi dhidi yao kashfa matusi dharau na kejeli
Kwanza Falsafa wanayo isimamia ni mbovu ya hovyo nathubutu kusema ni yakipuuzi eti Amani inatangulia Haki inafuata na hii siyo Falsafa ya kiisilam, nadhani ni neno walilopewa waliseme kwa maslahi ya watu fulani ili kuhalalisha dhulma tu.
Nimesoma andiko la mwanachuoni mmoja ninae Muheshimu sana amejitahidi kudadavua ili kuipa nguvu hoja hiyo nilicho kiona ni sawa na kuihalalisha nyama ya nguruwe tu kwasababu kachinjwa kwa Bismillah, wafanya Maandamano walieleza sababu zao mapema tu kwamba hawata shiriki uchaguzi na badala yake watavuruga uchaguzi kwasababu Tume haitendi haki inaisaidia Ccm tu Kushinda.
Hivi ni kweli Bakwata hawajui kua chanzo cha vurugu ni kukosekana haki kwenye chaguzi zetu tume inatangaza wasioshinda wizi wa kura, mimi nilifikiri Bakwata wangetoka na msimamo wa Sheikh Alli Geruko
Kuna siku alisema alipo kaimu umufti wakati mufti alipokua Makka kwenye swala ya Idd :
Tume ya uchaguzi itende haki inaweza kua chanzo cha kuvuruga amani Mungu amlipe kwa ukweli huu, lakini kuficha ukweli wa chanzo cha kuvurugika amani tunatafuta maneno ya kuwafurahisha wakubwa kwa maslahi binafsi hatuwasaidii viongozi bali tutaliangamiza taifa
Sikuzote Haki ni kitendo cha asili na kimaumbile Qur-an 6 : 73 وهو الذى خلق السموت والاض بالحق yeye ndie alie umba mbingu na ardhi kwa Haki,,, aya hii utafsirika kwa maana nyingi sana lakini kwa kifupi haki haitanguliwi na chochote bali yenyewe hutangulia na Mungu haki ameifanya iwe mwanzo kwani ndoyo kustawi kwa kila jambo siyo amani pekee mfano haki ya chakula kipite mdomoni ukikipitisha pengine popote utakua hukukitendea Haki ni kazima patatokea Madhara tu,, huo ni mfano tu lakini kila kitu Mungu alicho kiumba amekipa haki yake، na Haki za makubaliano ni hivyo hivyo chanzo cha migogoro yote Duniani hata ukienda katika Mahakama kesi zote zilizopo hapo utakuta kuna mmoja hakutenda Haki kwa mwengine
Sasa ukisema Amani inatangulia alafu ndiyo Haki,,,
Mna Haki ya kudharauliwa.
Naishauri Serikali kama Raisi alivyosema mchakato wa Katiba uwepo haraka Tume huru ya uchaguzi na iwe huru kweli anae chaguliwa ndiyo awe kiongozi kuwalazimisha watu kuongozwa na watu wasiyo wataka kwanguvu za Dola amani itaendelea kudorola
Ahsante