Maalim Gurumo alipataje hitilafu ya jicho?

Maalim Gurumo alipataje hitilafu ya jicho?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,101
Reaction score
16,792
Mzee wetu Muhidini Maalim Gurumo (r.i.p) nguli wa Muziki wa dansi nchini alikufa na kuzikwa kijijini kwao kule Masaki, kata ya Masaki, tarafa ya Sungwi, wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani kilometa kama 28 kutoka Kisarawe mjini.

Amezikwa hatua chache tu (kama 10) toka barabarani mkono wa kushoto wa barabara ya Kisarawe- Msanga karibu na soko la Masaki.

Inafahamika vema kuwa mzee huyu alikufa akiwa na jicho moja halifanyi kazi (limevunjika), kwaajili ya kuweka kumbukumbu nzuri ya mzee wetu huyu maarufu naomba kufahamu jinsi mzee huyu alivyopata kuwa na hitilafu ya jicho lake moja, nini ilikuwa sababu na lini?
 
Ebu wasiliana na yule mchambuzi wa muziki radio one anaweza kukusaidia.
 
alivyokuwa mchanga mama yake alimlaza kwenye mkeka uliokuwa chini ya mwembe, mama akatoka kidogo ndipo tawi likakatika kutoka kwenye huo mwembe, moja kwa moja, chubwi, kwenye jicho la mtoto, ndio ikawa hivyo, so sad.
me nilimsikia akimjibu salama jabir kwenye mikasi
 
Mkuu hili neno lilivyowekwa hapa linaleta mvuto wa usimulizi zaidi
 
Mkuu hili neno lilivyowekwa hapa linaleta mvuto wa usimulizi zaidi

Nakumbuka maswali ya kiswahili zamani:
Chagua jibu sahihi
1. Jiwe lilianguka kwenye maji
a) Chubwi
b) Pwaa
c) Twende
d) Mwaaa
 
Back
Top Bottom