Maajabu ya wilaya ya Rombo-Kilimanjaro

Maajabu ya wilaya ya Rombo-Kilimanjaro

Mtoa taarifa acha upotoshaji wewe,Kwamba wilaya haina Hospital ya Wilaya huu ni uongo.Ipo Hospital kubwa na yenye hadhi ya hali ya juu pengine tofauti na Wilaya nyinginezo.Sema tu hospital hiyo ni designated kwa maana ni ya Kanisa na inaendeshwa na Serikali.Kwa kifupi Hospital ipo,tena si moja bali ni Mbili zenye utaratibu huo.(Huruma na Ngoyoni).Vituo vya Afya pia vipo kila Tarafa na vyenye uwezo mzuri.Ukarabati wake umekuwa ukifanyika kila mara.
Mahakama ipo tena imekarabatiwa hivi karibuni,Magereza ipo ya kawaida na yenye hadhi kuliko Magereza mengine kama ya Korogwe,Mwanga na kwingineko,
Kituo cha Polis kipo walau hakipo vizuri sana lakini kinakidhi.
Hivyo utoe taarifa zenye uhakika.usitubabaishe.
Toa sifa pia kama shule kuwepo nyingi,na watu kujituma katika uzalishaji.
Tatizo kubwa ni Maji yasiyo ya uhakika kwa hapa Rombo na hasa wakazi wa tambarare wanataabika sana maji.
UKIACHILIA HURUMA HOSP KUNA HOSPITAL MPYA WILAYA INAITWA KARUME IPO USSERI
 
Na sio kweli mtoa mada : alivyosema Rombo kituo cha polisi ni magofu sio kweli mi ni mwenyeji wa Rombo kituo kipo vizuri kabisa . usilete uongo na unafiki.
 
Rombo imeendelea sana ,yani mm nimetembea sana hapa tz hasa vijijini naweza kukupa ushuhuda kuwa Rombo hakuna hata nyumba yanyasi na kama ipo imeachwa kama kumbukumbu tu ya wanafamilia,sasa Rombo unayoisema wewe ni ya Kenya mana Kenya kuna Rombo pia,tatizo Rombo ni maji hasa ukanda wa mashariki ,ila shule zipo nzuri kuliko hapa dar,pia kila mtaa unapitika tena kwa gari na kila familia kuna njia ya kwenda hm kwa gari,sio dar gari inalazwa ccm
 
Na sio kweli mtoa mada : alivyosema Rombo kituo cha polisi ni magofu sio kweli mi ni mwenyeji wa Rombo kituo kipo vizuri kabisa . usilete uongo na unafiki.
Nimependa jina lako. Ndeambase. Na akaseme tena huyu. Nina wasiwasi huyu alipita lower road ndo maana haielewi Rombo.
 
Na kama alivyosema mtoa mada Rombo iko vizuri kiuchumi pia kwani umeme tuliupata tangu Mwaka 1980 nakumbuka hata nyumbani kwangu kuvuta bomba LA maji safi tulivuta Mwaka 1982 wakati huo kulikua na bomba za mitaani ,almaarufu kama vihula vya mtaa .niongezee Barbara za uswazi zinapitika kwa gari aina zote kubwa, ndogo bila wasi wasi.. na vinjia vya kuelekea kwenye nyumba husika Mara nyingi zimepandwa maua na hupitika vizuri mno kwa gari pia.we VIP,
 
Kuhusu vituo vya radio kutoshika kule nakuunga mkono kule inashika radio maria tu na hata radio zilizopo hapa moshi mjini kama kili fm na moshi fm kule rombo hazishiki vizuri kabisa
 
Kuhusu vituo vya radio kutoshika kule nakuunga mkono kule inashika radio maria tu na hata radio zilizopo hapa moshi mjini kama kili fm na moshi fm kule rombo hazishiki vizuri kabisa
Radio Citizen ya Kenya ndio inashika vizuri kuliko radio zote, ila mtoa mada kaweka chumvi nyingi sana eti Rombo ni kama haipo Tanzania!!! Duh
Zamani miaka ya 90's na mwanzo wa 2000's kweli ilikuwa imekaa ki Kenya zaidi kuliko Tz ila kwa sasa mambo yamebadilika sana
Na tatizo la maji ni kutoakana na ukame wa sasa hivi , zamani kulikuwa vizuri kwenye maji
na zahanati nafikiri vijiji vingi vina zahanati sasa
Ila tatizo kubwa la Rombo ni Rombo-Dar migration na Rombo-Arusha miration, watu wamepukutika nyumba zipo tupu, makanisa hayajai kama zamani yanakuwa na watu wakati wa krismasi tu....inasikitisha kweli yani wnabaki wazee tu kule
 
Na kama alivyosema mtoa mada Rombo iko vizuri kiuchumi pia kwani umeme tuliupata tangu Mwaka 1980 nakumbuka hata nyumbani kwangu kuvuta bomba LA maji safi tulivuta Mwaka 1982 wakati huo kulikua na bomba za mitaani ,almaarufu kama vihula vya mtaa .niongezee Barbara za uswazi zinapitika kwa gari aina zote kubwa, ndogo bila wasi wasi.. na vinjia vya kuelekea kwenye nyumba husika Mara nyingi zimepandwa maua na hupitika vizuri mno kwa gari pia.we VIP,
Ila watu wanahamia sana Dar na Arusha, hii ni tishio la uchumi, maana wanabaki wazee tu
 
mleta mada hata kama unanyemelea jimbo la Rombo upotoshaji wa kiwango hili haukubaliki! Nakushauri kama unautaka ubunge wa Rombo jipange kivingine na si kutumia propaganda uchwara kama hizi na tena kama ni CCM sahau kabisa.
 
Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.

Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana . Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.

Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika hata moja kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station redio za kenya .

Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya.

Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.

Ni vyema serikali ikayatazama hayo niliyodokeza japo matatizo ni mengi sana yalio kwenye wilaya ya Rombo
Ahsante. Ila hujafanya utafiti kuandika ulichoandika.
Unaposema Kuna miundombinu mizuri ya bara bara unamaanisha barabara hii moja ya lami inaoishia msitu wa Rongai au barabara za mitaa?
Unaposema hakuna radio station ya Tz inayokamata huko Rombo, radio Maria ni ya wapi?
Unaposema hakuna hospital ya wilaya, unaelewa nini kuhusu hospital teule ya Huruma?
Je unaposema ni wilaya kongwe, unailinganisha na wilaya gani nyingine?
 
kwa kuwa hata pombe inayotumika hapo ni ya kutoka kenya,nawashauri waiombe serikali ya tz iwape kibali ili wajiunge na kenya kabisa..iwe ndan ya kenya.
 
Ila watu wanahamia sana Dar na Arusha, hii ni tishio la uchumi, maana wanabaki wazee tu
Haha mnama umenikumbusha juzi nilikua kwenye mwendokasi natoka kivukoni naenda kimara kwakweli ile gari 80% walikua ni wachagga na kuna siku natoka buguruni kwenda msasani mpaka konda na dereva walikua ni wachagga achilia mbali abiria karibu wote mpaka kuna jamaa akasema hivi nimepanda gari ya masaki au Moshi watu wote kicheko!! !
 
Aisee Arusha ndio zaidi, Achilia mbali Arusha mjini, yaani ukiingia vijiji vya ndani ndani kabisa huko utakuta wachaga wamejaa huko, sehemu ambayo ulikuwa unawazia utakuta wamasai na waarusha tu unakuta warombo unajiuliza waligunduaje haya maeneo?
 
Arusha me huwa sioni tofauti na Moshi kabisa sababu idadi ya wachagga pale Arusha inazidi idadi ya wachagga waliopo Moshi mpaka Manyara Singida Dodoma kote huko wachagga wametapakaa niliingia visiwani ndani kwenye wilaya fulani ya Buchosa Mwanza nilipigwa na butwaa kuwakuta wachagga huko wanafanya Biashara ya Samaki na dagaa visiwa vyote.
 
Yule msemaji uchwara wa chadema Ben Saanane ndio kwao huko??
 
Back
Top Bottom