Maajabu ya wasafiri na smartphone

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,596
4,890
Barabara ilikua mbovu na mizigo ilikua inapakiwa juu , lakini hatukuwahi kusikia eti basi limechinja ishirini au kuona watu wakipiga selfie na maiti na majeruhi badala ya kuwasaidia
380cc49dd9521ac20fba1a3dea1b1bbf.jpg


Siku hizi barabara nzuri na mzigo unapakiwa chini , lakini kila kukicha utasikia basi limechinja kibao huku watu wakishindana kusambaza picha za watu waliokatwa vichwa na video za wanaokata roho. Kwa kifupi ni kama vile simu zao ziko standby zinasubiri ajali mbaya itokee ili wawe wa kwanza kurusha watu wanavyokufa

Hivi aliyeturoga yupo au amekufa...?
 
Nafikiri kipindi hicho vyombo vya barabarani havikuwa vingi.

Kwahiyo hakukuwa na msongamano.

Na ukumbuke zama hizo kiteknolojia walikuwa nyuma sana.

Ndio maana hawakuweza kuchukua Video, Video inabidi iwepo Camera ya kuchukulia Video, na Picha hadi Camera ya picha mgando iwepo, tofauti na hivi sasa kwenye simu zao Watu wanazo Camera za kuchukua Video na Camera za picha mgando.

Siku hizi tukio linapotokea, dakika chache tu Habari zimeshasambaa kwa haraka sana tofauti na zamani
 
Mimi inanisikitisha sana ajali inatokea watu hawatoi msaada ni kupiga picha tu
 
Mtoa mada bonge la kilaza. Hizo smartphone zilikuwepo enzi hizo? Mi nakumbuka kulikuwa na mpiga picha mmoja tu aliyekuwa anatembelea shule yetu kila weekend.Yaani shuleni ukimiliki camera wewe bonge la tajiri
 
Sikuizi ukipata tatizo badala ya kusaidiwa , unatwanga mipicha kwanza... teh teh teh
nahisi ni Matumizi mabaya ya teknolojia tu
 
Tunachangia utadhani sisi hatumo, mbona baadhi yetu tumo humu?
Kujifanya wema wakati Instagram, wasap, fb tunashindana kutuma picha, tena nyingine za aibu
Haipendezi, Naam Haipendezi
^^
 
Sikuizi ukipata tatizo badala ya kusaidiwa , unatwanga mipicha kwanza... teh teh teh
nahisi ni Matumizi mabaya ya teknolojia tu


Yah ni lazima wakufotoe katika kuweka kumbukumbu sawa na kutu update wengine. Au we hutaki habari na takwimu?
 
Yah ni lazima wakufotoe katika kuweka kumbukumbu sawa na kutu update wengine. Au we hutaki habari na takwimu?
Aah Ni sawa na kupatwa na ugonjwa alafu unaenda kununua vocha ili uposti fesibuku badala ya ile hela kununulia dawa.. Hiyo ni MisUse
 
Unapigwa picha kwanza alaf mtu adi azisend akiwa huko njiani porini network shida anahakikisha tiki kabisa Whatsapp alaf ndio anaangalia vp umeumia kiasi gani akusaidie" dunia ya sasa
 
Hizi comments wakuu nimejikuta nacheka sana.....kiukweli tunatakiwa tubadirike panapohitaji msaada tutoe msaada kufotoa kuje baadae
 
hiyo picha lazima itakua African bus enzi hizooo Mwanza kama sio Trans Africa ama Tanganyika bus
cc ram
 
MTOTO WA KUKU, we mwenyewe una shida. Kulikua na 7bu gani kuzungumzia uchawi?

Na hilo ndo tatizo kubwa. Kila kitu utaskia 'nani aliyetuloga?'

Huu ujinga mtauacha lini? Mnaamini sana uchawi badala ya kutumia akili na kanuni za kisayansi kutekeleza yanayotuhusu.

Uchawi ni aina nyingine tu ya utapeli uliokubuhu.
 
MTOTO WA KUKU, we mwenyewe una shida. Kulikua na 7bu gani kuzungumzia uchawi?

Na hilo ndo tatizo kubwa. Kila kitu utaskia 'nani aliyetuloga?'

Huu ujinga mtauacha lini? Mnaamini sana uchawi badala ya kutumia akili na kanuni za kisayansi kutekeleza yanayotuhusu.

Uchawi ni aina nyingine tu ya utapeli uliokubuhu.


Mkuu umechukulia siriaz mno.. shake it lose a little! nani aliyeturoga ni metaphor au wewe sio mbongo?
 
Mkuu tatizo kubwa ni design ya mabasi ya siku hizi, mabasi ya zamani frame/skeleton nzima ilikiwa inachomelewa/welded na vyuma imara sana,baadae ndio wana wanaweka mabati ya steel nje na ndani kwa kutumia rivets, mbinu za ujenzi wa mabasi kwa kutumia mbinu hizo ulikuwa unayafanya mabasi yawe imara sana, hata yalipokuwa yanapinduka yalikuwa yanabonyea kidogo, frame nzima inabaki almost intact.

Mbinu hizo zinatumika katika uhundaji wa ndege za abiria na mizigo, ukiwa kwenye ndege karibu na dirisha linalo pakana bahawa ukichungulia nje utaona jinsi mabati yalivyo banwa na rivets chungu nzima,airframe building za type hiyo zina aminika sana kwa uimara wake.

Uhundaji wa mabasi wa siku hizi ni hatari sana, wanaimarisha tu chini ya chasiss wanakoweka mizigo ya abiria,spacing ya vyuma vya kushikilia mabati ni kubwa mno kiasi cha kwamba ikitokea accident watu wanakufa sana, si hilo tu hata spacing ya abiria na na dari/roof ya basi ni ndogo sana na si imara ndio maana basi likipinduka miguu juu kichwa chini abiria wote wanangamia kwa kupondwa na roof kutokana na uzito wa chasiss na matairi.

Nakumbuka Ulaya walikuja juu kuhusu hatari ya design za mabasi ya siku hizi, walipaswa kuyafanyia merekebisho fasta, sisi kwetu hapa sioni kama SUMATRA imekwisha lishtukia hilo.
 
Back
Top Bottom