Killing machine
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 2,374
- 3,395
Habari za Sasa hivi wakubwa zangu, wadogo zangu, kaka na dada zangu hapa Jamii Forums. Bila kusahau babu zetu hapa JF kina mshana Jr, Bujibuji n.k, heshima kwenu wakuu.
Leo nimeona niwashirikishe maajabu ya viongozi wetu tangu uhuru hapa Tanzania. Na yafuatayo ndiyo maajabu yenyewe ambayo mataifa mengi duniani wanatusifu na kutuona watu wa ajabu sana, tuliyotukuka na kuna habari za siri siri kwamba Tanzania ndiyo tunaoongoza kwa kuwa na akili hapa Afrika Mashariki.🤣🤣
Basi tuanze na maajabu yenyewe kama ifwatavyo;
(1) Naskia kuna kiongozi alishawahi kutawala hapa Tanzania, kiongozi huyu ilikuwa ikifika kipindi cha uchaguzi basi aliweka picha yake na kimvuli kwahiyo watu walichagua kati ya picha na kimvuli.🤣🤣🤣
Narudia tena Watanzania walifanya uchaguzi kati ya picha na kimvuli, huu ulikuwa ni uchaguzi wa haki uliyovunja rekodi ya Dunia.🤐🤐🤐 Hongera Tanzania yangu, ninaomba anayemjua kiongozi huyo anipe jina tafadhari.
(2) Tanzania ndiyo inchi inayoongoza kwa ukubwa wa kijografia, madini, vivutio vya utalii, ardhi nzuri, lakini ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na wasiyokuwa na kazi wengi zaidi Afrika Mashariki, pia wasiyokuwa na makazi wengi.
(3)Tanzania iliyozungukwa na maziwa makuu matatu Yani Nyasa, Tanganyika, Victoria, bado kuna maziwa ya ndani kama vile Natroni, Manyara n.k, pia kuna mabwawa kama vile Kyungu lulu, Chara, mito mikubwa mikubwa kama Rufiji, Ruaha, lakini ndiyo nchi pekee inayosumbuliwa na tatizo la umeme,😂😂 maji😂😂 na wanaogopa sana mvua zikichelewa. Utadhani hawafahamu chochote kuhusu irrigation agriculture maarufu kama kilimo cha umwagiliaji.😂😂😂🤗🤗
(4) Tanzaniaukinunua ndege andaa na uwanja wako,😂😂ukinunua treni andaa na reli yako.🤣🤣🤣
(5) Tanzania bei ya gari Japan ni nusu ya ushuru wa gari hapa Tanzania "Kwa watu wanaitwa T.R.A.". Yaani ukinunua gari la milioni 50, basi andaa milioni 100 za kusajiria na ushuru.😋😋😋
(6) Tanzania huku kubaka au kumpa mwanafunzi mimba ni miaka therathini jela, lakini ufisadi wa billions of Tanzanians shilings ni mambo ya kuzungumza tuu kisha yanaisha, unaendelea kula bata Dar. Isitoshe wanakupa na ulinzi ili usije ukaibiwa ulichoiba.🤣🤣🤣🤣
(7) Tanzania ukiiba kuku ni hatari zaidi kufungwa kuliko ukiiba gari, bajaji n.k.🤗🤗🤗
Basi wakuu mimi niishie hapa, endeleeni kumimina sifa zilizotukuka za taifa letu hapo chini kwenye comment. Mimi zangu zimeishia hapo.
Karibuni.