Maajabu ya ulimwengu usiofahamika kwa wengi

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,675
Reaction score
14,056
Ilikuwa ni December 2004,,,ni miaka 20 iliyopita katika Mkoa wa Shinyanga _Tinde.

Miaka hiyo kulikuwa na fisi wa kutosha...nilikuwa nimekosa nauli ya kwenda krismas Moshi,,,,,hivyo nyakati za jioni tunaweka mkeka nje kwenye mbalamwezi huku tukinywa pombe ya gongo iliyotengenezwa kwa mihogo.....

Usiku wa jana yake katika kijumba nilichopanga kulitokea mtetemo mkubwa wa kundi aidha ni ng'ombe au punda... sauti ilikuwa ni kubwa sana mpaka kijumba kinatikisika,,,,wanakuwa wanazunguka nyumba niliyomo,,,,

Sikutoka nje wala kuchungulia dirishani,,,,nikapuuzia nikaendelea kulala..nikawasha fegi nikaendelea kupuliza nikacheki kichupa cha gongo ya kuzimulia usubuhi nikakipiga nikalala....

Kulipokucha nikasahau kabisa kuwasimulia wenyeji wangu.... mpaka ilipofika hiyo mida ya jioni mkekani tukiwa tunakunywa gongo..... baada ya fisi kupita mbele yetu akasimama akawa anatuangalia ndipo nikakumbuka jana usiku sauti nilizosikia,,,nilipowasimulia wenyeji wangu..kwanza walishtuka halafu wakasema una bahati hukutoka nje wala kuchungulia dirishani,,,,,lakini hata hivyo nikaonywa haya mambo hayazungumzwi hadharani.....

Basi pakawa pametokea ubishi kama ugomvi kwa wenyeji wangu..... wakabadili lugha na kuanza kuendelea kubishana sana .....usiku huo kulikuwa na mbalamwezi....fisi wakazidi kutusogelea pale tulipo wakaanza kulia huku wakitazama mbalamwezi,,,changanya na mambo waliokuwa wanaongea wenyeji wangu ambayo sikuyaelewa yakawa kama yanavuruga hali iliyopo,,,

Ghafla nikaona kama mkeka tuliokalia unapaa na tunasafiri kama vile ndoto kaubaridiii sauti za fisi nazisikia kwa mbali na mabishano ya wenyeji nayo bado yanaendelea kwa mbali,,,,,,,

Nikawa kama nimetoka usingizini nikajikuta sehemu fulani Iringa ambayo naifahamu vizuri...tupo nje kuna mbalamwezi tunakunywa komoni na ulanzi....sasa nilionao hapo ni wengine kabisaa lakini hawana habari kama nimetoka shinyanga wao wanaona nilikuwa nao kwa siku kadhaa....

Nikapiga moyo konde nikasema labda hii ni namna ya kufa hivyo basi sikutaka kuzungumza chochote,,,bali nilikuwa msikilizaji tu.....

Kwa kifupi nikapitiwa na usingizi,,,kushtuka ni asubuhi kunakucha tupo Tinde,,,,,

Wala haikuwa ni ndoto wala ulevi,,,ni ulimwengu fulani wa nguvu ya KIAFRIKA,
 
downloadfile-11.jpg
 
Back
Top Bottom