Maajabu ya TRA, unaweka kodi kubwa kwenye magari wakati hauzalishi magari nchini. Mzunguko wa mafuta lazima ushuke tu

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,033
Tunaendelea na maajabu ya TRA, hii ni segment mpya kabisa hebu jaribu upige hii hesabu.

Nchi hii haina viwanda vya kutengeneza magari, sio kwamba unaongeza kodi kwamba unalinda viwanda vya ndani vinavyozalisha au kuunganisha magari hapana.

Matokeo yake mwananchi anaacha kuagiza gari anahamishia kipaumbele kwenye mambo mengine, gari TRA wanaona ni kama anasa hivi wanajificha kwenye kivuli cha kulinda mazingira kajionee maajabu, kodi ya kuagiza gari lililotumika ni kubwa na kodi ya gari jipya nayo ni kubwa, na kodi ya gari ya miaka michache toka litengenezwe ni kubwa.

Unawaza wanalinda mazingira gani?

Haya mwananchi ataacha kuagiza gari halafu mzunguko wa mafuta utakua chini hapo kodi kubwa inakufanya ukose vyote,
Tanzania yenye Bandari kumiliki gari ni gharama kuliko kumiliki gari Zambia, Rwanda, wala Congo ambazo hazina bandari.
 
Ukiagiza gari pia kuna tozo inaitwa railway levy. Hii itawahusu wanaoagiza magari. TRA wanaiongeza kwenye kodi ya gari mteja anayotakiwa alipe.
 
Hiyo ndiyo serikali ya wanyonge ambayo wenye nayo wao wenyewe hawalipi hata ndururu ya kodi.

Kodi watukamue, hata ikija kuwajibika kwetu kwenye nyakati za dharura, wao haiwahusu.

Kwani wao ndiyo waleta matetemeko? Kwani wao ndiyo waleta corona?

Hawa si wa kufumbiwa macho!
 
Kabla ya hili, wanyonge wengi walilalamika kwamba tozo za kuagiza gari ni kubwa sana na hazina uhalisia na zinamuumiza mwananchi. Watu walilia sana kwamba kumiliki gari isiwe anasa nchini, nikajua siku serikali ikiingia huko gharama itashuka. Kumbe wapi, badala yake kilio kimezidi.
 
Infwakti unapo diskareji kuagiza magari unaongeza uharibifu wa mazingira kwani unalazimisha wale wenye magari waendelee kuyatumia kwa miaka mingi zaidi. Kwa sasa tutegemee kuona mikweche ikiongezeka barabarani kwani hakuna tena mwenye uwezo wa kuagiza walau yale yenye afadhali.
 
Tutawaachia wao wenyewe wawe na magari, wengine tutaendesha baiskeli
 
Ukiagiza gari pia kuna tozo inaitwa railway levy. Hii itawahusu wanaoagiza magari. TRA wanaiongeza kwenye kodi ya gari mteja anayotakiwa alipe.
Inahusiana vipi na gari, ukizingatia asilimia kubwa limepitia baharini?
 
Ninapimsikia mtu anasema serikali hii ipo kwa maslahi ya wananchi huwa namshangaa mpaka nakaa chini. Hawa wakikaa kwenye vikao vyao wanafikiria matumbo yao na familia zao. Ndo maana mradi ukiletwa wilayani lazima DC na anaofuatana nao wafaidike. Wanahimiza kodi, wanaweka kodi kubwa, wao wana exemption ya kodi.
 
Kiukweli kwa namna hii waTz wengi tutaendelea kutumia magari yenye Manufacture year zaidi hata ya miaka 10,,, tutaendelea kuwa soko la magari chakavu ktk ukanda wetu wa EA

Ukilinganisha na wenzetu wa Kenya ambao asilimia kubwa ya magari wanayoaigizia year of Manufacture ni 2014, 2016 mpaka 2018 wakati sisi huku mtu anaagizia Toyota Premio, Brevis au Mark X ya mwaka 2005 kajitahidi sana 2007
 
Safi Sana Mitano tena.Hii inaenda sambamba na kuwafanya muwe sawa afu magari yawe ya Serikali tuu Ili muwaabudu vizuri
 
Back
Top Bottom