Maajabu ya soka la Afrika: Guélor Kanga kukutana na kamati ya nidhau kuhusu sakata la umri wake

political monger senior

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
1,801
5,788
Mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon Guélor Kanga Kaku atakutana na kamati ya nidhamu ya CAF kueleza kwa nini mama yake alifariki mwaka 1986 lakini yeye alizaliwa 1990.

1689084407119.jpg
 
Huyu mwamba nampongeza sana, ni miongoni mwa mashujaa halisia wa maisha yao.

Afrika wengi wetu tunazaliwa ktk familia duni, hivyo kuja kufanikiwa kwa wakati ni kisanga. Angesema umri halisia mpaka sasa huenda asingepata nafasi ya kujikomboa kimaisha maana angekuwa anacheza ndondo cup muda huu huko kwao.

Kwenye mafanikio kuna siri kubwa na hiyo siri ndio mafanikio yenyewe.

Humu ndani ambaye hajawahi kudanganya maisha yake yote awe wa kwanza kumnyooshea vidole, nje ya hapo kaeni kimya maana amevuja jasho la kutosha kuwa na uwezo wa kumiliki $5M alizo nazo Legendary wetu huyo
 
Mie nadhani inabidi mindset ya watu wa mpira ibadilike badala ya kuangalia umri wa mtu waangalie zaidi kipaji na uwezo.

Hii itapunguza sana tabia za udanganyifu wa umri na mambo mengine kama hayo. Wachezaji wengi wazuri wamewekwa kando kwa kigezo kidogo tu Cha umri kitu ambacho naona sio sawa
 
Back
Top Bottom