Maajabu ya Serikali ya CCM kusalimu Mwishoni

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,817
35,827
Kumekuwa na kelele nyingi za watu kuashiria kutoridhika na agenda kadhaa za serikali.

Rejea misimamo ya serikali na wapambe wao kwenye:

1. Uwepo wa Corona
2. Umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona
3. Uhitaji wa chanjo dhidi ya Corona
4. Umuhimu wa wanafunzi wanaopata mimba kurejea shule.

Ikumbukwe tumepita huku:



Kwamba leo tuko hapa:



Kipi walicho tunyanyapaa nacho, walikomaa nacho hadi mwisho?

Tutafika tu. Kwani wala ipo hiyana basi? Ya msingi zaidi yanayobakia:

I. Mbowe siyo gaidi
II. Tunataka katiba mpya.

Hawa ni suala la muda. Tutaelewana tu.

IMG_20211125_090152_963.jpg


Kwamba leo ajira zimeongezeka?

Labda kama ni mahsusi kwa ajili ya kuwaambia ndege.
 
Waliolaaniwa wameshakufa!
Nyote mlaaniwe na roho zenu za husda. Mnaongea vitu kufuata mkumbo. Unashangilia mtoto akipata mimba arudi darasani, kwa wapuuzi kama brazaj sawa ila mwenye akili hawezi kufurahia maana serikali inatakiwa kuhakikisha mtoto ambaye hajawa tayari kubeba mimba haibebi.

Mimba haitoke hewani au kama ya Bikra Maria, bali inatoka katika kujamiiana; je, tunaruhusu kujamiiana? Mbona watu wanahangaika na matokeo (end result) baadala ya kupambana na chanzo (source).

Aidha unadhani bila kujua chanzo cha kuanza kujamiiana unakuwa umepata jawabu la tatizo, la hasha. Kama ni umaskini uliomsababisha mtoto ajamiiane ili apate pesa za kujikimu, je akirudi shule ufukara huo utakuwa umekoma au umeongezeka. Hili suala ni zito siyo kama wapuuzi kwa kumchukia JPM wanataka kutueleza
 
Nyote mlaaniwe na roho zenu za husda. Mnaongea vitu kufuata mkumbo. Unashangilia mtoto akipata mimba arudi darasani, kwa wapuuzi kama brazaj sawa ila mwenye akili hawezi kufurahia maana serikali inatakiwa kuhakikisha mtoto ambaye hajawa tayari kubeba mimba haibebi...
Hatuwezi kulaaniwa ili kuridhisha roho yako dhalimu.

Nyie mnaoabudu miungu ya kuzimu mtapotea mmoja baada ya mwingine.
 
Kumekuwa na kelele nyingi za watu kuashiria kutoridhika na agenda kadhaa za serikali.

Rejea misimamo ya serikali na wapambe wao kwenye:

1. Uwepo wa Corona
2. Umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona
3. Uhitaji wa chanjo dhidi ya Corona
4. Umuhimu wa wanafunzi wanaopata mimba kurejea shule.

Ikumbukwe tumepita huku:

View attachment 2022822

Kwamba leo tuko hapa:

View attachment 2022824

Kipi walicho tunyanyapaa nacho, walikomaa nacho hadi mwisho?

Tutafika tu. Kwani wala ipo hiyana basi? Ya msingi zaidi yanayobakia:

I. Mbowe siyo gaidi
II. Tunataka katiba mpya.

Hawa ni suala la muda. Tutaelewana tu.

View attachment 2022825

Kwamba leo ajira zimeongezeka?

Labda kama ni mahsusi kwa ajili ya kuwaambia ndege.
Hicho chama kinatakiwa kufutwa duniani

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom