Maajabu ya Mji wa Moshi

ESCORT 1

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
1,368
2,890
Nimekuja Mo town kwenye msiba wa Mzee Ndesamburo, nimeshangaa na kustaajabu.

Mara ya mwisho kukanyaga Moshi ilikuwa mwaka 1998, almost miaka 20 iliyopita lakini mji huu haujabadilika.

Miaka nenda rudi Mji wa Moshi upo vile vile tena upo kizamani sana. Wachagga mnaniangusha, yaani ile misifa yote ya Kugombea magari mwisho wa mwaka kumbe mnakuja kwenye kamji uchwara kama haka.

Wachagga hebu, amakeni acheni kujisifu haswa mkiwa nje ya Mo town, badilisheni hiki kijiji chenu mnakokaita Mji.

Baada ya Msiba nitafika huko A town kwa Machalii nikaone nini kimejiri, maana hawana tofauti sana na watu wa Mo town.
 
Miaka 20 ilopita Daslam street haikua na lami. Leo stori ni ingine.

Miaka 20 ilopita ukiwa town ungeona barafu nyingi mlimani. Leo ukiwa town unaona vijibarafu tu.

Miaka 20 ilopita mto karanga ulikua na mimaji. Leo ni kama mfereji.

Miaka 20 ilopita hakukua na Supamaket hata moja. Leo zinaota kama uyoga.

Miaka 20 ilopita Panjwani tu ndo alikua anauza mavifaa ya maana ya umeme. Leo wakibosho nao na masabufa yao wametamalaki.

Miaka 20 ilopita Temba Watch ilikua ndo unapata saa na raba za ukwee. Matajiri tu. Leo Temba watch ni kijiduka.

Miaka 20 ilopita hoteli za Moshi mjini za ghorofa hazikuzidi 5. Kindoroko, Newcastle, Leopard, Buffalo na Zebra. Leo kuzihesabu hadi tume makini iundwe.

Miaka 20 ilopita stendi ya Moshi ilikua tu na baraza ya kusubiria abiria hotel ya Shangazi na maduka ma3 hapo kwa Shazily. Leo ni bonge la shopping mall. Na Morogoro wameiga Moshi.

Miaka 20 ilopita mji wa Moshi ulikua na kasehemu kanaitwa Shaonaro. Leo hakapo.

Miaka 20 ilopita alikua Chrisburger mwenyewe. Leo kuna Mekus, Red Stone, Story Lounge, Black Diamond, Hugos, n.k.

Yote kwa yote, Moshi inapnekana haibadiliki kwa sababu biashara nyingi za miaka hiyo ziko tu hadi leo japo na nyingine zimekuja. So kwa mtu wa zamani akirudi ataenda kulekule. Milans, Chrisburger, KNCU, Panjwaniz, Moshi Drapers, Temba Watch, etc. Labda ataimis Shaonaro na chapati zao.

Jipe Muda utaiona Moshi katika mwanga mpya man.
 
Nimekuja Mo town kwenye msiba wa Mzee Ndesamburo, nimeshangaa na kustaajabu.

Mara ya mwisho kukanyaga Moshi ilikuwa mwaka 1998, almost miaka 20 iliyopita lakini mji huu haujabadilika.

Miaka nenda rudi Mji wa Moshi upo vile vile tena upo kizamani sana. Wachagga mnaniangusha, yaani ile misifa yote ya Kugombea magari mwisho wa mwaka kumbe mnakuja kwenye kamji uchwara kama haka.

Wachagga hebu, amakeni acheni kujisifu haswa mkiwa nje ya Mo town, badilisheni hiki kijiji chenu mnakokaita Mji.

Baada ya Msiba nitafika huko A town kwa Machalii nikaone nini kimejiri, maana hawana tofauti sana na watu wa Mo town.

Old is gold
 
Wachaga si km makabila mengine wanaopenda kujenga mijini wachaga wanajenga kwao(kijijini) hebu nenda marangu mwika rombo machame na kwingineko pia wachaga ndio wanaongoza kujenga nyumba Tanzania kama ingetokea kila kabila libebe nyumba zao kuzipeleka kwao bs moshi kusingukua na nafasi ya kuziweka hz nyumba.mtoa mada mchaga hujisikia fahari kujenga kwao na kwenda kwao tofaut na makabila mengine kurudi kwao man wanaona aibu kwa kutokujenga nyumba na maendeleo mengine.
 
Huo ni ukweli ulio wazi kbs, nilisoma Moshi around 2000, na kwa ss natenbelea saana moshi, yaani pale moshi town mabadiliko ni madogo sana, ukiacha yale magorofa yanayomea karibu na mahakama pale,

otherwise moshi iko vilevile
Maendeleo kwako ni magorofa !!!!!
 
Moshi imebadilika sana kwanijuavyo sasa hivi kuna majengo mengi mazuri na marefu ya kuvutia, jamani waliyoko Ms naombeni mnipigie picha miradi iliyokwisha na inayoendelea ya ujenzi Ms ili afahamu ukweli.kwa mfano opp. Na benk ya Nmb kuna jengo limeshazidi 10 flrs na bado linaendelea
 
Back
Top Bottom