Naunga mkono hoja yako..... maana mkataa kwao ni mtumwa.Kila kiongozi angekuwa anafanya hivyo home kwake nadhan tz ingekuwa kama Kwa Trump vile
Viongozi hawajazaliwa mijini,wamezaliwa vijijini,lakn,ukienda hata barabara ya kuingilia kijijin kwake hakuna
Hongera mjomba
Sent using Jamii Forums mobile app
Shangaaa wewe.Wa-Tz bana, mtu akijenga kwao anasemwaaa, asipojenga anasemwaaa!!!
Lipi bora?
Bora tule wote, kujenga home ndo uwajibikaji! Viongozi wapuuzi na wabinafsi hawakumbuki kwao.
JPM, has done well. Wengine waige kwao. Nilipitaga jimbo la aliyekuwa waziri wa kilimo Eng Chiza huko Kakonko, pabayaaaaaa utafikiri ni njia ya kuelekea jalalani huku jamaa linaishi Dar! Nikapita jimbo la Lukuvi, nako hovyo tu....
Sasa lipi bora???
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulevi tu !Hakuna mahali kama Arusha.
nyumbani kwa rais na waziri wa muda mrefu serikalini miaka ya nyuma. Tujifunze kujenga kwetu tupatapo fursaKatika pilika za hapa na pale, basi nikafanikiwa kufika chato baada ya muda mrefu toka mara ya mwisho nlivyofika mahala hapa. Yafuatayo nimepata kuyaona kidogo:
Kati kati ya mji huu kuna mataa ya kuongozea magari barabarani, taa hizi ni kituko kidogo maana zinakusubirisha wakati hakuna magari mengine au watu wanaopita, yaan unaweza kujikuta uko tu mwenyewe na unasubiria tu taa zi ruhusu. Naam wale wa mikoa kama morogoro pamoja na umaarufu wa mkoa wake ila mataa kwao ni habari nyingine, hakuna kabisa kwaio hapa wanaweza wasinielewe.
Mitaa yote ya mji huu ina barabara za lami, ni karibu asilimia 90 mkeka tu, kuanzia za kati ya mji mpaka mitaani.
Wakazi wa huku kama nao wanajiona waTanzania namba moja, yaani kiburi kiburi hivi.
Barabara nzuri ila baiskeli zimetawala kweli kweli, anyway nyie wa rorya hapa mnaweza msinielewe au nyie we marinyi barabara mbovu wilaya nzima, kwaio naombeni utulivu wenu hapa.
Hospitali za mji huu ni full air conditions tu, kipupwe safi kabisa, na sijaona vihospitali kama sinza, Sijui temeke au wapi huko bado sanaa, kimiundo mbinu kwa hospital za chato.
Majengo ya serikali ni nadhifu na mazuri sanaa, yanavutia ata kuyatazama tu.
Kuna ulinzi mzuri tu, migambo wamejaa kila mtaa na wanachokera wanajifanya ni matrafic wanakamata hadi magari, sijui mamlaka haya wameyatoa wapi.
Kuna airport karibuni itaanza kutumika, japo ukiwaangalia wananchi tu walio wengi kwa kweli labda nauli zishushwe.
Wakuu tukumbuke kujenga vijijini kwetu ni muhimu sanaa. Ni haya machache tu na ndio nliyoyaona kwaio nisije kupangiwa vya kuona na kusema.
Barabara nzuri ila baiskeli zimetawala kweli kweli, anyway nyie wa rorya hapa mnaweza msinielewe au nyie we marinyi barabara mbovu wilaya nzima, kwaio naombeni utulivu wenu hapa.
Mwalimu Nyerere angefanya hayo Butiama lingekuwa jiji la mfano...
Lakini Mwalimu hakuwa na ubinafsi kiasi hicho...
Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha aise nimecheka sanaKwa uongozi mzuri wa Magufuli, na kama amekuwa mbunge wa Chato kwa miaka mingi lazima patakuwa hivo tu. Viva JPM. Wewe ni mfano wa kuogwa
Naunga mkono tusi lako kwake.nimekutukana !
Nitandikien jamv mitaa yng ya ihimbili pale...nikirud nisilowe vumb...Mpango wa kuweka traffic light pale Magu upo, zitawekwa kwenye makutano ya barabara JIRANI na eneo la gulio pale . Nadhani Chagadema watajinyonga very soon.
Sent using Jamii Forums mobile app