Maajabu ya Mji wa Chato

Maajabu ya Mji wa Chato

Wa-Tz bana, mtu akijenga kwao anasemwaaa, asipojenga anasemwaaa!!!

Lipi bora?

Bora tule wote, kujenga home ndo uwajibikaji! Viongozi wapuuzi na wabinafsi hawakumbuki kwao.

JPM, has done well. Wengine waige kwao. Nilipitaga jimbo la aliyekuwa waziri wa kilimo Eng Chiza huko Kakonko, pabayaaaaaa utafikiri ni njia ya kuelekea jalalani huku jamaa linaishi Dar! Nikapita jimbo la Lukuvi, nako hovyo tu....

Sasa lipi bora???

Kwaio unaimiza ukanda na unyumbani wewe? Unaigawa nchi mzee.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chato ni mji pekee duniani ambao punda wamewekewa traffic light pia mbuzi wana uwanja wa kuchezea umewekwa lami
Vile vile mji huu ni maarufu kwa kilimo cha samaki

Acha uchochezi mkuu hahaahahah
 
Uncle wake dotto hasemwi vibaya huku, ni kumpa misifa tu hata akivurunda. Kwa sisi tuliozoea kumkosoa tukitembelea huku tunapata shida kwenye hilo, inabidi tujitoe ufahamu kidogo na kuwa kama nyumbu

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Mkuu unazoea vipi kumkosoa mtu?hiyo ni chuki binafsi ruhusu upendo utawale,kumchukia mtu hakukupi amani bana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aiseh....! wafanye mpango na morogoro waweke taa....., mfano pale makutano ya iringa road na barabara ya tumbaku, hatari sana pale, pia eneo la kihonda magorofani na makutano ya dodoma road na pale njia ya mazimbu road,,,,ni maeneo hatari sana
 
Jamaa aliziwekaga kitambo sana nadhani tangu iyo Barbara ya kutoka mwanza inakamilika mwaka 2009
 
Katika pilika za hapa na pale, basi nikafanikiwa kufika chato baada ya muda mrefu toka mara ya mwisho nlivyofika mahala hapa. Yafuatayo nimepata kuyaona kidogo:

Kati kati ya mji huu kuna mataa ya kuongozea magari barabarani, taa hizi ni kituko kidogo maana zinakusubirisha wakati hakuna magari mengine au watu wanaopita, yaan unaweza kujikuta uko tu mwenyewe na unasubiria tu taa zi ruhusu. Naam wale wa mikoa kama morogoro pamoja na umaarufu wa mkoa wake ila mataa kwao ni habari nyingine, hakuna kabisa kwaio hapa wanaweza wasinielewe.

Mitaa yote ya mji huu ina barabara za lami, ni karibu asilimia 90 mkeka tu, kuanzia za kati ya mji mpaka mitaani.

Wakazi wa huku kama nao wanajiona waTanzania namba moja, yaani kiburi kiburi hivi.

Barabara nzuri ila baiskeli zimetawala kweli kweli, anyway nyie wa rorya hapa mnaweza msinielewe au nyie we marinyi barabara mbovu wilaya nzima, kwaio naombeni utulivu wenu hapa.

Hospitali za mji huu ni full air conditions tu, kipupwe safi kabisa, na sijaona vihospitali kama sinza, Sijui temeke au wapi huko bado sanaa, kimiundo mbinu kwa hospital za chato.

Majengo ya serikali ni nadhifu na mazuri sanaa, yanavutia ata kuyatazama tu.

Kuna ulinzi mzuri tu, migambo wamejaa kila mtaa na wanachokera wanajifanya ni matrafic wanakamata hadi magari, sijui mamlaka haya wameyatoa wapi.

Kuna airport karibuni itaanza kutumika, japo ukiwaangalia wananchi tu walio wengi kwa kweli labda nauli zishushwe.

Wakuu tukumbuke kujenga vijijini kwetu ni muhimu sanaa. Ni haya machache tu na ndio nliyoyaona kwaio nisije kupangiwa vya kuona na kusema.
Nimekuelewaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom