Maajabu ya Mji wa Chato

Maajabu ya Mji wa Chato

Hospitali ya wilaya chato.
5.JPG
 
Kwa uongozi mzuri wa Magufuli, na kama amekuwa mbunge wa Chato kwa miaka mingi lazima patakuwa hivo tu. Viva JPM. Wewe ni mfano wa kuogwa
Hahahaha wewe punguza mapenzi kwa Magu.Kwahiyo kuwa na barabara nzuri lakini wananchi hawana magari inaaminisha nini?kuwe na Airport nzuri lakini wenyeji hawapandi hizo ndege?kuwe na office nzuri za TRA lakini kodi inayokusanywa ni kituko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadi punda wanavuka mataa
Bongo pikipiki marufuku katikati ya jiji, lakini huku hata mkokoteni wa punda ni ruksa katikati ya jiji!
Lakini tusishangae, miundo mbinu lazima itangulie ili kuvuta kasi ya maendelei! Miji mingine igeni busara ya chato! Tangulizeni lami kabla ya magari kuongezeka na tangulizeni taa za kuingozea magari kabla magari hayajaongezeka! Tusilaumu Bali tusifu! Ni upangaji mzuri wa mipango ya maendeleo! Hongereni sana viongozi wa halmashauri ya chato! Ndiyo! si wao ndo walipanga na kutenga bajeti kwa ajili ya miundo mbinu hiyo?
 
Watu wanaizungumzia Chato kwa kejeli lakini tuizungumzie Chato kwa hoja na uhalisia wake. JPM ni Rais wa Tanzania na anatoka Chato kwa hiyo utake usitake mazingira ya Chato lazima yakarabatiwe na yarekebishwe kumuwezesha Rais kufanya kazi zake kwa ufanisi. Tukumbuke Rais haendi "likizo" kama likizo na hili linafanyika ulimwengu mzima. Mar-a-largo kule USA imefanyiwa hivyo. Pili kuhusu Airport nalo nafikiri ni la msingi ule ule tu. JPM atakauwepo miaka 5 ijayo na inawezekana hata 10. Kuutoa msafara wa Rais hadi Mwanza halafu uingize kwenye ferry halafu uende Chato nafikiri ni gharama kubwa sana vinginevyo uwe na "standby logistics kanda ya ziwa kitu ambacho nafikiri gharama zitakuwa kubwa sana sana. Kwa maoni yangu Airport ni shuluhisho muafaka. Assume JPM atastaafu 2025 bado eneo hilo litahitaji Airport kwa kuwa ukitua hapo utaweza kwenda migodini, Biharamuro, Muleba hadi Bukuba. Tatu turidhike tu kwamba zile nyakati za kujenga Airport Arusha na Moshi, barabara za lami kaskazini, umeme kaskazini zimefikia ukomo wa milele! Ni mawazo yangu tu lakini!

Sent using Jamii Forums mobile app
Very good, hujakosea najua wanaojadili Chato kimizaha wengi wao ni chagadema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, hii photoshop au!
Mi huwa nadhani ni fiksi tu. Basi hatari.
ahahahhaaaha nimecheka sana sana ni kweli nilifika Chato nikitokea Bukoba kuelekea Mwanza. Nilipita pale Chato saa kumi jioni, kwenye zile taa ilikua gari yetu, Baskeli upande wa pili na sijui ng'ombe au Punda wale. Dah nilishangaa sana sana sana.

Tulionywa pia na mwenyeji wetu mmoja kuwa kule lazima kwenye zebra usimame hata kama uko peke yako maana hata Mwenyekiti wa Kiyongoji anaweza kukukamata, atakusimamisha ukijua anaomba Lift kumbe anakukamata.

Niliona pia ujenzi mkubwa sana sijui ilikua ni kitu gani kile au ndio lile Jengo la TRA???
 
Back
Top Bottom