Maajabu ya mchepuko wangu

Mkuu hebu mpe mtoto ii tanzania ina watu wachache sana
 
ni wachache kwa tofauti gani na wanawake? na umri upi ulio chini zaidi na upi ulio juu? acheni kuhalalisha ufirauni.
Fanya utafiti utagundua kuwa resho ya wanaume watu wazima 18+ ni karibu 1:3 ya wanawake wa umri huo,kwa uchache kila mwanaume anaweza kuwa na wanawake zaidi ya watatu bila effect yoyote,😛😎
 
Yaani hiyo ni mbinu mpya ya wadada kuwakamata wanaume, wala usithubutu huo ujinga kabisa, hamna mtu anaependa kulea mtoto peke yake, amka kwenye huo usingizi kijana
 
wadada wanaotaka kulelewa ndio wanapenda kuzaa na waume za watu.
 
Mkuu usithubutu...achana nae kabisa...utakuja kuishi maisha ya uchizi...Tulia na mke wako na utunze familia yako.
Otherwise kama unataka mke wa pili..fuata taratibu zote ikiwepo kumjulisha mkeo
 
Mkuu kwanini uzae mtoto kwa kulazimishwa na mtu mwingine pasipo kuamua mwenyewe?

Kwanini uzae na Mwanamke asiye mkeo ikiwa unathamini ndoa yako?

Una uhakika na matunzo ya huyo mtoto?

Hayo maswali ni ya msingi wewe kujiuliza.
 
Kweli nimeamini adui wa mwanamke ni mwanamke...kupenda maisha ya shortcut...sisi wanawake tulivyo anakutega huyoo mtu bado anaenda chuo mtoto wa nini?? anajua una mke hamuonei huruma mwanamke mwenzie pamoja na watoto tena kwa mshahara laki mbili....haya endeleeni na michepuko sukari elfu tatu kilo
 
Sasa tufanyeje wakati nyie mnataka
 
Mkuu kwanini uzae mtoto kwa kulazimishwa na mtu mwingine pasipo kuamua mwenyewe?

Kwanini uzae na Mwanamke asiye mkeo ikiwa unathamini ndoa yako?

Una uhakika na matunzo ya huyo mtoto?

Hayo maswali ni ya msingi wewe kujiuliza.
Kuzaa na mwanamke mwingine asiye mkd wangu si kwamba simpendi mke wangu pia namuhurumia watoto watatu tayari anao sasa na pia mimi sina shida ya kwanini nizae na mtu mwingine shida target ya huyu mwanamke itakuwa nini?
 
JAMII FORUM INATUSAODIA SANA NAPATA MAWAZO MAZURI SNA HAPA NA PIA NAHISI TATIZO HILI SI LANGU MWENYEWE
 
Unauhakika gani kuwa wewe siyo kilaza kwa haya uliyo andika hapa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…