Maajabu ya kijiji cha llubengela-ziwa Tanganyika Kigoma

Tanzania ni kubwa
 
Kuna shule huko?
 


Waha si watu....wana mambo ya hajabu sana. Kipindi nilikuwa naishi na kufanya kazi Kasulu Nilishuhudia ujinga wa hajabu sana, yaani jamaa alikuwa anatembea na koboko mfukoni mwake na watu hawamshangai. Anaweza kukaa na kucheza draft nyoka ghafla akamtoka mfukoni anakwenda ota jua, jamaa akiwa tayari kuondoka unaona yule nyoka anajikunja na kuingia mfukoni bila hata kuitwa, mara ya kwanza nilivyo ona nilimshangaa jamaa na kuanza kukimbia akaniambia nisiogope mi si mtu mbaya, nikamshangaa ena ananijuaje. Kuulizia wenyeji ndipo wakasema kuwa jamaa anaitwa (…..) ni mchawi/mganga....ukimvamia kumuibia unakumbana na huyo nyoka na akikugonga hauponi. Yule nyoka ni mlinzi wake na anakunywa damu tu wala si unga.
 
Hahahah!
Nimecheka unasema unacharaza bandiko

BTW kwa muda niliokaa na kufanya kazi huko nasema uko sahihi
Kigoma iliyopakana na kagera na Tabora ina unafuu kuliko kigoma iliyopakana na ziwa na mikoa ya kusini(Rukwa)
 
Huo ukanda wote wa ziwa Tanganyika hapafai, kuna wachawi balaa

Kuna kijiji kinaitwa KALEMA, pale kulikua na mamba mkubwa sana, alikua anatafuna watu balaa

Siku ameuawa walikuta pale tumboni ameandikwa kwa maandishi makubwa BADO WEWE.
Karema ya wapi hiyo mkuu
 
hapa niliwahi kuambiwa . kuna jambazi wa kikongo .aliyekuwa anateka maboti ziwani. alikamatwa na wanajeshi waliokuwa katika operation ya kutokomeza wahamiaji haramu. wanajeshi waliamua kumuua kwa kumpiga risasi bila mafanikio. yaani wakimlenga risasi inatoka inaangukia chini ,karibu na mpigaji.

lakini alitokea mzawa akawaambia huyu ana uchawi wa vidono ( aina ya uchawi unaozuia kudhurika mwili iwe ni panga au risasi) ,,, akashauri wauzingue .. wakampa smg .. alichoma chini ,akachoma kushoto ,kulia na juu ... alivyomuelekezea .alisambua kichwa . wanajeshi wakabaki wanashangaa.... wakaambiwa welcome kigoma.... wao wanakuita KUSINI .
 
Nasikia kuna sehemu moja huko kilwa kivinje kuna mtu mmoja anaitwa Sharif.uyo ni balaa nasikia anatembea juu ya maji kutoka kwenye kisiwa anachokaa mpaka kwenye vijiji vingine.uwa ijumaa ndo anaonekana maana upenda kuswali katika ivyo vijiji siku iyo ya ijumaa
 
Yakutoshuka nilishuhudia jamaa aliyeiba mikungu ya ndizi kwa mzee mmoja, Tiba yake alipigwa fimbo moja kiunoni na mikungu ya ndizi ikadondoka fasta. Ila jamaa alitozwa dume la kondoo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…