Maajabu ya kijiji cha llubengela-ziwa Tanganyika Kigoma

Ndio maana yaneno maajabu
ulitegemea neno ajabu lije kwa mtu kula ndizi huku akitembea!!
Ndugu yangu dunia inamengi na sio kila jambo lazima utalifaham
Nenda kule utaambiwa
Hao nyoka ni nyoka wakichawi sio nyoka tuwajuae sisi
na anapo kuuma nimekuambia lazima ukatibiwe na Mganga jamii ya kabila hilo lakitongwe
kutapika kwako hayo magamba ndio kupona kwako yanatoka kama sumu meusi,
pia nikupe nyingine
kule Mbuzi hafungwi zizini
Kiangazi huachwa msimu mzima wakizurula hovyo
Na ifikapo masika ndio hukamatwa na kufungwa nyuma ya nyumba kamba miguuni nje kabisa ya nyumba na kwakuwa ni msimu wa kilimo tu
sasa olewako uibe
Mbuzi ataita Meee mee tumboni kama mmemla
na kama umembeba Hatashuka
Tanzania ni kubwa
 
Watu wanajua ni uongo lakin ukwel ndio huo, Mimi nipo iki kijiji kwa muda wa miez minne sasa nimejionea mengi ya kustaajabisha apa kijijini LUBENGELA, awanywi bia ila wanapombe yao inatoka Congo inaitwa SEN'XA, gongo inasubili kwa huo mziki wa SEN'XA, jamaa awachimbi vyoo, wanajisaidia kwenye mawe kandokando ya ziwa
Kuna shule huko?
 
Wadau kijij hiki kinapatikana kusini mwa mkoa Wa Kigoma uliopo kanda ya ziwa, Kijij hiki ni kidogo sana kina wakazi wasiozidi 2000, kijiji hiki hakuna mwizi. Kila baada ya nyumba mbili kuna mchawi, ukiwaangalia mikononi wamevaa ma bangili ya shaba.

Asili yao ni wakongo karibu wote, hakuna umeme, nishati inayotumika ni kuni, mkaa, sola pawa, watu wanaacha vitu nje, maduka wazi na hakuna anayethubutu kuiba. Shughuli yao kubwa ya uchumi ni uvuvi,

Sasa kubwa kuliko ambayo imenifanya nicharaze uzi huu ni kwamba Luna MAMBA ambaye anaonekana Mara kwa Mara hapa kijijini na inasadikika ni MAMBA wa MTU , yupo hapo kwa ajili ya kusaidia kazi za uvuvi za uyo MTU. Watu wanafanya shughuli zao kama kawaida na akamati mtu, mimi ni mgeni mahali hapa na nimemshuhudia kwa macho yangu uyo mamba na nikajaribu kutoa wazo auwawe lakini nikaambiwa na wazee wa kijiji kuwa nisirudie kusema hivyo.

Nikakaa zangu kmya coz hapa nimekuja kufanya kazi ya muda mfupi halafu nitaondoka kurejea mkoani, Kigoma kuna mambo.


Waha si watu....wana mambo ya hajabu sana. Kipindi nilikuwa naishi na kufanya kazi Kasulu Nilishuhudia ujinga wa hajabu sana, yaani jamaa alikuwa anatembea na koboko mfukoni mwake na watu hawamshangai. Anaweza kukaa na kucheza draft nyoka ghafla akamtoka mfukoni anakwenda ota jua, jamaa akiwa tayari kuondoka unaona yule nyoka anajikunja na kuingia mfukoni bila hata kuitwa, mara ya kwanza nilivyo ona nilimshangaa jamaa na kuanza kukimbia akaniambia nisiogope mi si mtu mbaya, nikamshangaa ena ananijuaje. Kuulizia wenyeji ndipo wakasema kuwa jamaa anaitwa (…..) ni mchawi/mganga....ukimvamia kumuibia unakumbana na huyo nyoka na akikugonga hauponi. Yule nyoka ni mlinzi wake na anakunywa damu tu wala si unga.
 
Hahahah!
Nimecheka unasema unacharaza bandiko

BTW kwa muda niliokaa na kufanya kazi huko nasema uko sahihi
Kigoma iliyopakana na kagera na Tabora ina unafuu kuliko kigoma iliyopakana na ziwa na mikoa ya kusini(Rukwa)
 
Huo ukanda wote wa ziwa Tanganyika hapafai, kuna wachawi balaa

Kuna kijiji kinaitwa KALEMA, pale kulikua na mamba mkubwa sana, alikua anatafuna watu balaa

Siku ameuawa walikuta pale tumboni ameandikwa kwa maandishi makubwa BADO WEWE.
Karema ya wapi hiyo mkuu
 
hapa niliwahi kuambiwa . kuna jambazi wa kikongo .aliyekuwa anateka maboti ziwani. alikamatwa na wanajeshi waliokuwa katika operation ya kutokomeza wahamiaji haramu. wanajeshi waliamua kumuua kwa kumpiga risasi bila mafanikio. yaani wakimlenga risasi inatoka inaangukia chini ,karibu na mpigaji.

lakini alitokea mzawa akawaambia huyu ana uchawi wa vidono ( aina ya uchawi unaozuia kudhurika mwili iwe ni panga au risasi) ,,, akashauri wauzingue .. wakampa smg .. alichoma chini ,akachoma kushoto ,kulia na juu ... alivyomuelekezea .alisambua kichwa . wanajeshi wakabaki wanashangaa.... wakaambiwa welcome kigoma.... wao wanakuita KUSINI .
 
Nasikia kuna sehemu moja huko kilwa kivinje kuna mtu mmoja anaitwa Sharif.uyo ni balaa nasikia anatembea juu ya maji kutoka kwenye kisiwa anachokaa mpaka kwenye vijiji vingine.uwa ijumaa ndo anaonekana maana upenda kuswali katika ivyo vijiji siku iyo ya ijumaa
 
Ndio maana yaneno maajabu
ulitegemea neno ajabu lije kwa mtu kula ndizi huku akitembea!!
Ndugu yangu dunia inamengi na sio kila jambo lazima utalifaham
Nenda kule utaambiwa
Hao nyoka ni nyoka wakichawi sio nyoka tuwajuae sisi
na anapo kuuma nimekuambia lazima ukatibiwe na Mganga jamii ya kabila hilo lakitongwe
kutapika kwako hayo magamba ndio kupona kwako yanatoka kama sumu meusi,
pia nikupe nyingine
kule Mbuzi hafungwi zizini
Kiangazi huachwa msimu mzima wakizurula hovyo
Na ifikapo masika ndio hukamatwa na kufungwa nyuma ya nyumba kamba miguuni nje kabisa ya nyumba na kwakuwa ni msimu wa kilimo tu
sasa olewako uibe
Mbuzi ataita Meee mee tumboni kama mmemla
na kama umembeba Hatashuka
Yakutoshuka nilishuhudia jamaa aliyeiba mikungu ya ndizi kwa mzee mmoja, Tiba yake alipigwa fimbo moja kiunoni na mikungu ya ndizi ikadondoka fasta. Ila jamaa alitozwa dume la kondoo.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom