Jua limekuwa likitoa nishati miaka mamilioni na mamilioni, na hakuna dalili zinazoonyesha nishati hiyo kupungua. Nijuavyo, nishati yoyote ile haidumu kwa muda usio na kikomo; kwa mfano, magari yanatumia nishati ya mafuta (diesel au petrol), lakini gari likitembea umbali fulani, nishati hiyo huisha. Hali kadhalika umeme tutumiao majumbani, huisha, na tunalazimika kununua Luku.
Tulitegemea nguvu ya jua ipungue kwa kadiri siku zinavyokwenda, lakini hali ni tofauti, kwani kila siku nguvu ya jua ni ileile. Chanzo cha nishati ya jua ni nini hata kisiishe? Hata kanuni za nishati zinasema kuwa, nishati itabadilika kutoka hali moja kwenda hali nyingine. Hii maana yake ni kwamba nishati ikibadilika kwenda hali nyine, basi ile hali ya mwanzo haipo tena. Hivyo, jua kama nishati, nalo linabadilisha nishati, sasa kwanini linaendelea kubaki?
Kama kanuni ya kubadilika kwa nishati, kutoka hali moja kwenda nyingine ni kweli, basi tutegemee jua litakuja kuzima. Yawezekana, linapungua nguvu, lakini hatugundui kutokana na sababu mbalimbali, kama vile mabadiliko ya tabia nchi. Lakini pia tujiulize, jua likizima, nini kitaendelea? Litakuja jua lingine?