Maajabu ya Jua

stars

JF-Expert Member
Sep 10, 2020
819
1,111
Jua limekuwa likitoa nishati miaka mamilioni na mamilioni, na hakuna dalili zinazoonyesha nishati hiyo kupungua. Nijuavyo, nishati yoyote ile haidumu kwa muda usio na kikomo; kwa mfano, magari yanatumia nishati ya mafuta (diesel au petrol), lakini gari likitembea umbali fulani, nishati hiyo huisha. Hali kadhalika umeme tutumiao majumbani, huisha, na tunalazimika kununua Luku.

Tulitegemea nguvu ya jua ipungue kwa kadiri siku zinavyokwenda, lakini hali ni tofauti, kwani kila siku nguvu ya jua ni ileile. Chanzo cha nishati ya jua ni nini hata kisiishe? Hata kanuni za nishati zinasema kuwa, nishati itabadilika kutoka hali moja kwenda hali nyingine. Hii maana yake ni kwamba nishati ikibadilika kwenda hali nyine, basi ile hali ya mwanzo haipo tena. Hivyo, jua kama nishati, nalo linabadilisha nishati, sasa kwanini linaendelea kubaki?

Kama kanuni ya kubadilika kwa nishati, kutoka hali moja kwenda nyingine ni kweli, basi tutegemee jua litakuja kuzima. Yawezekana, linapungua nguvu, lakini hatugundui kutokana na sababu mbalimbali, kama vile mabadiliko ya tabia nchi. Lakini pia tujiulize, jua likizima, nini kitaendelea? Litakuja jua lingine?
 
Jua lenyewe ndy hili kubwa la njano,na dunia ndy hiyo ambayo mshale umeelekea,Kama punje ya mchanga
IMG_20220812_085850.jpg
 
Kulingana na sayansi, Nishati ya jua itaisha siku moja( Inasemekana miaka bilioni tano ijayo litaanza kufa). Wanasayansi wameshachunguza na kuona baadhi ya nyota nyingine(Jua) zinazozaliwa na kufa huko deep space.

In about 5 billion years from now, the sun will begin to die. As the Sun grows old, it will expand. As the core runs out of hydrogen and then helium, the core will contract and the outer layers will expand, cool, and become less bright. It will become a red giant star.
 
Jua lenyewe ndy hili kubwa la njano,na dunia ndy hiyo ambayo mshale umeelekea,Kama punje ya mchangaView attachment 2321545
Daaah, umetoa ufafanuzi mzuri sana na kueleweka vyema, lakini ulichokiandika hapo kwenye jua ni matusi na udhalilishaji (piece of shit).

Hata hivyo, ukubwa wa jua sio hoja. Kama unamaanisha ukubwa ndio sababu, kwa hiyo baada ya matirioni ya miaka kupita, litapungua na hatimaye kuisha kabisa?
 
Kulingana na sayansi, Nishati ya jua itaisha siku moja( Inasemekana miaka bilioni tano ijayo litaanza kufa). Wanasayansi wameshachunguza na kuona baadhi ya nyota nyingine(Jua) zinazozaliwa na kufa huko deep space.

In about 5 billion years from now, the sun will begin to die. As the Sun grows old, it will expand. As the core runs out of hydrogen and then helium, the core will contract and the outer layers will expand, cool, and become less bright. It will become a red giant star.
Naona hapo kuna logic. Je, nyota zinazokufa ndio zitatengeneza jua lingine ili kuhalalisha ile kanuni ya nishati haiwezi kupotea?
 
Jua = mc^2

Wanasanyansi before Einstein walijiuliza sana ilo swali lako mbona halizimi, ndio walijua linachoma hydrogen lakini mbona kama haiishi?
Siri ndogo mpaka sasa juu ya jua inayojulikana ni kwamba linatoa nishati yake kwa reaction ambayo inaitwa fusion. Hii reaction ni mojawapo ya nyukilia reaction zinazofahamika, ambapo nyenzake mwanadamu ndio hutengenezea mabomu ya Nyukilia.

Kabla sijakuchanganya ana nirudi kufafanua equation niliyoanza nayo. C ni speed ya mwanga 30000000 mper sec na m ni uzito. Kila kitu ulimwenguni ni energy!

Kwa sasa kuna mbio kwa mataifa makubwa USA, FRANCE, UK, CHINA kasoro RUSSIA wapo kwenye mbio ya kufanikisha kutengeneza kinu kitakacho fanyiza fusion reaction atakaye shinda ndio atakuwa new master.

Tukija kiroho jua ndio limetuumba sisi ndio linatupa nguvu, kuliabudu hawakukosea. Maana elements zote zinatoka kwake akishamaliza hydrogen yake.
 
Back
Top Bottom