ujenzi Wa Daraja La Kigamboni Ambao Unatarajiwa Kuanza Hivi Karibuni . Ujenzi Huo Ambao Utatekelezwa Na Serikali Kwa Pamoja Na Nssf Kama Main Financer Au Kama Mwekezaji Wa Mradi Huo Mkubwa.mradi Huo Mkubwa Kuchukuliwa Na Kuekelezwa Na Nssf Ni Mkubwa Na Wa Aina Yake Kutekelezwa Na Mfuko Huo Wa Penseni Utagharimu Zaidi Ya Shillingi Billioni 35. ( 35,0000,000,0000.00)na Mradi Huo Utaendeshwa Kwa Mtindo Wa Build, Run And Transfer Yaani Wawekezaji Nssf Watawekeza Hizo Billion 35 Za Walalahoi Yaani Michango Yetu Sisi Kwenye Hili Daraja Na Kuliendesha Kama Road Toll . Kwa Muda Wa Miaka 25 Na Baada Ya Hapo Watalikabidhi Kwa Serikali Waliendeshe Wenyewe.
Mutakumbuka Ya Kwamba Nssf Imeanzishwa Kama Ni Mfuko Wa Pensheni Kwa Wafanyakazi Wa Makampuni Ya Binafsi Yaani Private Sector . Inatarajiwa Hawa Nssf Wawekeze Katika Miradi Ambayo Itakua Na Tija Ili Wastaafu Waweze Kupata Faida Kubwa Wakati Wa Kustaafu . Hili Ndio Lengo La Mfuko Huu Wa Nssf.
Huu Mradi Wa Daraja La Kigamboni Hauna Tija Ni Wa Kisiasa Zaidi Na Pia Hata Hio Upembuzi Yakinifu Yaani Feasibilty Study Iliofanywa Anaonekana Ni Fake Na Haikuzingatia Ukweli Yakinifu Kwamba Ni Hasara Kubwa Kwetu Sisi Tunaochanga Ndani Ya Mfuko Huo Kwa Kutegemea "viji9senti" Tutapokua Tumestaafu.
Laiti Hizi 35 Billion Za Michango Yetu Zingewekezwa Katika Miradi Mingine Kama Real Estates Basi Uwezekano Wa Wanachama Kupata Bonus Kwa Wanachama Ni Mkubwa Sana.
Inawezekana Hapa Kuna Ufisadi Wanalazimishwa Nssf Kuingia Ili Watu Wapate Ulaji.
35,000,000,000/= Ni Nyingi Mno Kuzirejesha Na Kupata Faida Kwenye Daraja. Fedha Hizi Ili Zirudi Kwa Faida Ya Wanachama Basi Daraja Hili Liwe Na Uwezo Wa Kuipatia Nssf Tzs 615,881,988.56 Kila Mwezi (ukichukulia Interest Ya 21% Inayotolewa Na Mabenki Kama Mikopo ). Sasa Jee Nssf Wataweza Kupata Tzs 615,881,988.56
Kwa Mwezi? Ukweli Hapana Hata Kama Kila Gari Itatozwa Tshs:1000 Kwa Kila Trip Moja Inayopita Kwenye Daraja Hilo.hata Kama Kutakua Na Investment Aina Gani Huko Kigamboni Haitarajiwi Kuwa Na Movements Ya Magari Zaidi Ya 1000 Kwa Siku Kutumia Daraja Hilo . Hivyo Nssf Watarajie Kupata Tshs:30,000,000/= Kwa Mwezi . Si Dhani Kama Itaku Haki Kuwatoza Ushuru Wataopita Kwa Miguu Kwenye Daraja Hilo.
Kwa Hio Nssf Wacheni Kuingia Kwenye Mradi Huu Kwa Kutumia Mapesa Yetu Wanachama Hauna Faida Kwetu Na Kwa Mfuko Ni Hasara Kubwa.ila Labda Kuna Maslahi Ya Kifisadi Tu.
Daraja Lijengwe Lakini Si Na Nyinyi Nssf Bali Serikali Itafute Fedha Zake Wenyewe Kwa Wafadhili Wafanikishe Huu Mradi Na Sio Nssf . Mukiendeleza Na Mradi Huu Basi Hamtakua Mumetenda Haki Kwa Wanachama Wa Mfuko Huu.
Natoa Mwito Kwa Nssf Wastop Kuendeleza Mradi Huu. Nssf Ni Kwa Wanachama Wa Mfuko Huo Sio Kazi Yake Kuingia Katika Miradi Ya Miundo Mbinu Hii Ni Kazi Ya Serikali Kuu Inayokusanya Kodi. Nssf Wanatukata Sisi Kwa Ajili Yetu Kupata Mafao Bora Na Mengi Zaidi Kuliko Sasa Ambapo Tunapata Sio Zaidi Ya Kile Tulichochanga Kwani Mfuko Huu Unatumiwa Vibaya.
Ndio