Maajabu na kweli katika ziara ya siku 4 ya Rais

Maajabu na kweli katika ziara ya siku 4 ya Rais

Mleta uzi, hapa duniani hakuna Mtukufu zaidi ya Mungu...sasa unavyomuita Magufuli mtukufu ni kumdhihaki Mungu.unaweza kumuita rais Magufuli au mh.magufuli na sio mtukufu!
 
Mleta mada ana hoja ya msingi..kuna tatizo kubwa ndani ya Ikulu, washauri wa Kiongozi pamoja na baraza la mawaziri..time will tell
 
Wakuu Heshima Mbele.
Ikulu kupitia msemaji wake mkuu, Ndg. Msigwa, waliuaminisha Umma wa watanzania kuwa Mtukufu Rais atakuwa na ziara ya kikazi katika Mikoa Minne kwa siku Nne yaani Mkoa wa Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.

Ajabu na kweli ni kuwa, Mhe.Rais hakuweza kufika Makao Makuu ya Mikoa hiyo kama ilivyo ada za ziara za wakuu wa nchi wakiwa mkoani.

Lakini pia hakuweza kusomewa taarifa za Mkoa kama ilivyo kawaida ya ziara za wakuu wa nchi wawapo katika Mkoa husika.

Si hilo tu bali hata hakuweza kufanya Majumuisho ya ziara kwa kila Mkoa kwa kukutana walau na wadau wa maendeleo wa Mkoa husika.

Nani alisimamia protokali ya ziara ya Mhe. Rais?

Haya ni Maajabu na Kweli Yametokea?
Yaani wewe una matope kichwani unasema maajabu nikadhani unamaanisha unachoandika ''MAAJABU" U HUELEWI MAANA YA NENO HILO? Hivi Rais akifikia kwenye Kata ni Mkuu wa Mkoa gani atakayebaki makao makuu ya Mkoa kusubiri Rais amfute? Huelewi mamlaka ya Rais kaa kimya.
 
Msitucheleweshe!
Tuko na bus la haraka.........
Mtupishee.
 
Nafikiri muda si mrefu raisi atajiuzulu,maana ameshahisi kila afanyalo anakosolewa,tujitayarishe kwa uchaguzi mpya!
 
Acha kukariri mambo
Magufuli hasubiri kufanya ziara mkoani ndipo asomewe taarifa.Taarifa zinaletwa kwake kwa mtiriko maalum
Sio lazima kufika makao ya mkoa na kuhutubia,wilayani pia kuna watanzania
My God tusamehe sana haya mawazo si ya mtu aliyeenda shule bali kutumia akili ya mtaani tu
 
Hizi shule za kusomea ujinga mnazipata wapi?

Kabla hujaleta ujinga hapa kwenye jukwaa jaribu kufanya hata utafiti kidogo.

Kwani Rais hakupita katika Mikoa minne?

Kwani ni lazima Rais afike Makao Makuu ya Wilaya na Mkoa ndio uelewe kuwa amefanya ziara.

Au ulidhani Rais alikuwa anasafiri kwa kutumia usafiri wa anga?
Alikuwa anatafuta wanachama kwenye kivuli cha ziara,tuwe wakweli
 
Hizo protokali zimefuatwa kwa miaka zaidi ya 50 na kutufikisha hapa zilipo, acha sasa abadili mwelekeo ili kuepuka kama yaliyomkuta Lowassa alipokuwa Nyamagana na kupewa taarifa za kilimo cha pamba kabla ya kuikataa.
 
Yeye anapata kero directly toka kwa wananchi. Taarifa rasmi huwa zina mambo yake
 
Back
Top Bottom