Maajabu makubwa ya prof.Muhongo

Maajabu makubwa ya prof.Muhongo

Kama ingefanyika tathmini duniani, Tanzania inaongoza kwa viongozi wenye fikra za njozi kuliko matendo. Wewe umepewa mamlaka ya kuwezesha wananchi kuwa na maisha bora halafu unakuja taarifa ambazo ni njozi. Kauli hii inafaa kutolewa na wahubiri makanisani na watabiri siyo kiongozi mwenye mamlaka ambaye tayari tumeona utendaji kazi na uwongo wake. Si kosa kwa yeye kubadili kazi na kutangaza sasa kuwa amekuwa mtabiri.
Mwaka 2015 uwe wenye mafanikio makubwa sana. Taifa letu linaingia kwenye Uchumi wa Gesi Asilia. Dira yetu ya Maendeleo inatulazimisha kufanya kazi kwa bidii zaidi na kwa ubunifu mkubwa kwa kutumia sayansi na teknolojia ili ifikapo Mwaka 2025 Tanzania iwe nchi ya kipato cha kati (uchumi imara). Umeme mwingi, wa uhakika, wa bei nafuu na unaopatikana kiurahisi vijijini na mijini ndiyo injini kubwa ya upatikanaji wa ajira mpya kwa vijana wetu. S Muhongo
 
lizaboni...umeme unaotumika mtwara nao ni wa gesi.bei ya umeme mtwara haupo wa bei ya chini.hiyo bei nafuu anaoahidi muhongo itatoka wp?
Huu ndio ujinga na umbumbumbu wa bavicha..
Gharama ya umeme mtwara ni ya chini kuliko eneo lolote tz na nilishawahi kulalamika humu kuhusu ubaguzi huu.
Mende utawajua kwa kupaparisha mbawa zao ila kamwe hawawezi hata kusogeza kabati.
COCKROACHES......
 
Ukisikia uongo wa mchana ndio huu, haya maneno huwa yanawaponyoka tu midomoni mwao ila mioyoni mwao wanajua ni uongo. Nani atamuuliza Muhongo muda huo ukifika, kwani atakuwa kwao mara akilima matunda ili auze kwenye viwanda vya juisi

Heading inanipa tabu kidogo na maneno yaliyomo kwenye message yenyewe. Sasa maajabu hapo yako wapi? Ni kitu gani kipya alichokisema hapo au ni ajabu gani unayoiona wewe mbulula. Hivi hujui kama maneno hayo kayachukua kwenye dira ya taifa ya 2025. Uliza kuelekea utekelezaji wa dira hiyo tumefanikiwa lipi na kwa kiasi gani. Hayo ni maneno tu kama yale yaliyoandikwa kwenye kanga wanazovaa akina mama zetu.
Uliza ni kwa kiasi gani Millenium Goals 2005_ 2015 Tanzania imefanikiwa? Uliza vile vile MKUKUTA 1&2 zimefanikiwa kiasi gani?
Unapokuwa na wasanii na watu waongo kama huyu Nasty Professor unatarajia nini. Alipoingia wizarani alisema bei ya umeme haitapanda tena leo bei ya umeme iko ngapi? Mgawo alisema ndio mwisho mie huku ninakoishi tunapata umeme kwa masaa kila siku. Katika swala la mgawo kilichofikia mwisho ni utaratibu wa kytangaza mgawo tuu lakini mgawo halisi on the ground upo pale pale.
Niungane kwa pamoja na yule mbunge aliyesema hajaona professor mwongo kama Professor Muhongo. Inawezekana hata thesis zake ama za kudakia kwa kazi za wengine maana wakati ule technolojia ilikuwa bado sana kuhusu kucheki plagiarism katika kazi za watu.
Hell with Muhongo. The naughty professor
 
Maendeleo makubwa yatoke wapi jamani? Mbona tumekuwa wajinga na wepesi wa kusahau. Mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 hao hao mawaziri wa ccm walikuwa wakijitapa kwa kuanzishwa uchimbaji wa madini mbalimbali yakiwamo Dhahabu.

Mpaka hivi leo tunaongea hakuna hata faida moja inayotokana na madini hayo ambayo serikali hii ya ccm inaweza ikasimama na kujinadi nayo. Huu ni upuuzi na kutufanya ss wananchi hatuna akili na wepesi wa kusahau.

Kimsingi ni kwamba ss wananchi sio wepesi kusahau bali tunahadaika na amani tuliyonayo sasa na ndio maana hakuna hata mmoja wetu mwenye kuthubutu kuinua mdomo na kuhoji na hata wale waliojaribu hawakuweza kuendelea kuhoji.

Sababu kubwa inayofanya haya yote yanatokea ni kwamba hatuna utamaduni wa "Kuwajibishana". Utaratibu huo ungeweza wafanya viongozi wetu kuchukua majukumu kwa umakini zaidi. Hivi leo Waziri Muhongo akimaliza muda wake na hata kama hayo matokeo anayoyazungumzia hayajatoa hapatakuwa na mtu wa kumhoji. Na isitoshe waziri ajae atakuja na sera zake pia ambazo hatimaye hazitakuwa na mafanikio na kuifanya nchi inakuwa masikini kizazi hadi kizazi.

Kipindi tunahaidiwa manufaa ya madini miaka ya 90 mwishoni mpaka leo kuna zaidi ya miaka 15 na kwa kifupi mtoto aliyezaliwa muda huo leo hii ni mpiga kura lakini mafanikio tajwa bado hayapo. Hii ni habari ya Abunuasi na inanifanya kuiona hii nchi ni kama ile ya "Mfalme JUHA"
 
Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Prince Bagenda, licha ya kuandamwa na #TegetaEscrow , Prof. Sospeter Muhongo ndiye aliyekuwa kiongozi bora wa 2014 baada ya kuwezesha wizara yake kufikia malengo kwa zaidi ya asilimia 90. Hii inatokana na Muhongo kusimamia kazi kubwa ya usambazaji wa umeme vijijini, ujenzi wa bomba la gesu, ujenzi wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme, kasi kubwa ya utafutaji mafuta na gesi, usimamizi wa sekta ya madini na kujadili upya mikataba ya uchimbaji dhahabu ili serikali ipate kodi zaidi.

Ama hakika, Sospeter Muhongo ni mchapa kazi na mzalendo mkubwa anayepigwa vita na wachumia tumbo.

9k=
Muhongo.jpg
 
Wadau, gazeti la kila wiki la Taifa Imara, Uongozi Bora la Jumatatu Tarehe 5 hadi 11 Januari 2015, limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari "Profesa Muhongo Kiongozi Bora 2014. Katika taarifa hiyo, waandishi Prince M. Bagenda na William Maganga wameeleza mafanikio kadhaa katika wizara ya Nishati na Madini chini ya uongozi wa Profesa Muhongo ambapo wizara hiyo imetimiza malengo kwa asilimia 90 waliyojiwekea mwaka 2014.

Hongera sana Profesa Muhongo. Endelea kuchapa kazi kuwaletea maendeleo wananchi
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    434.8 KB · Views: 118
Bagenda ni mchumia tumbo. Full stop

Hapana, Bagenda yuko sahihi sana kwa mtizamo wangu. Hapa ndipo wa-Tanzania tuapokosea, kusahau mema 1000 ya mtu aliyolifanyia Taifa, kwa kosa moja. After all, hela ya ESCROW haijaibiwa, ila imelipwa pre-matrurely. Ingekuwa imeibiwa, sasa hivi tungekuwa tunadaiwa deni la umeme na Kampuni ya IPTL.
 
..... Kiongozi Bora Wa Inchi Gani. Kwa Kugoma Kujiuzulu Au Kwa Kudalalia Wezi?
 
Hongera sospeter muhongo viongozi kutoka Mara ni wachapa kazi sana kuanzia Mwl. Jk hadi warioba nakuendelea
 
anastahilii hata kijiji kwetu mwaka huu waziri wa nishati amefika na umeme umefika baada ya miaka 53 ya uhuru
 
... Amewafanya Watanzania Kufumbuka Macho Juu Ya Sakata La Escrow Kwa Kugoma Kuondoka Madarakani.
 
Back
Top Bottom