Maajabu makubwa ya prof.Muhongo

Maajabu makubwa ya prof.Muhongo

Reginald Mengi aka mchaga mzinifu akiona haya anatamani kujinyonga
Jitahidi kujisimamia mwenyewe usisimame kwa miguu ya Muhongo na Mengi hutopata mafanikio utaishia kusifia ideas zao tu.
 
Hiyo gesi mnaanza kuvuna lini!!?
Nawasiwasi mtapata aibu ya karne,yetu macho
Hiyo gesi ilianza kuvunwa 2004, watueleze faida tuliyopata mpaka leo ili tuamini tutafaidika zaidi.
Kusema/kuimba maneno mazuri huku mikataba mibovu inayowapa wageni 76% nasi tukipata 24% ikiendelea, hakuna maana yoyote.
Miaka ya 70 Baba wa taifa alikataa mkataba ambao uliwapa wageni 60%, leo tunachekelea kuwapa 76%?
Hali hii haikubaliki hata kwa jamii ya wajinga wote!
 
Reginald Mengi aka mchaga mzinifu akiona haya anatamani kujinyonga

Mengi + Mkono = Sendeka gawanya kwa Kafulila.zito na filiponjombe. Kisha Vita ya kumung'oa Muhongo, Nyumbani kwa Mengi sasa wanashindia Mihogo pesa zote kazielekeza kwenye vita ya kumng'oa Mhongo.
 
Pamoja na yote uliyoongea lazima kwanza Muhongo awajibike ndio hayo yafanyike, sio rahisi kutusahaulisha kirais rais tu apishe wengine waje wafanye kazi.

Vitalu vya Gesi ndivyo tu ndivyo vimemfanya Mengi amkomalie Mhongo pekee na kuwaacha, Gavana, Majaji, Waziri wa fedha na Waziri wa viwanda na biashara ? au kuna mengine? Maana pesa alizotumia Mengi mpaka sasa ni nyingi na laiti angeziongezea kwenye mishahara ya wafanyakazi wake leo Hii kusingekuwa na kilio cha mishahara Mibovu.
 
Yangu macho, mungu anipe uhai nione hayo maana tulishaambiwa mengi lakini hamna kitu mpaka sasa
 
Prof kanena maneno ya busara sana. Hapo hakuna porojo. Ni ukweli na uhakika

Kuna watanzania wengine vichwa maboga kweli. Hiyo gas itafanya maajabu gani chini ya huu utawala wa ccm kama dhahabu ambayo Tanzania ni ya tatu kwakutoa dhahabu nyingi Africa haijasaidia lolote katika kukuza uchumi.
 
Ukisikia uongo wa mchana ndio huu, haya maneno huwa yanawaponyoka tu midomoni mwao ila mioyoni mwao wanajua ni uongo. Nani atamuuliza Muhongo muda huo ukifika, kwani atakuwa kwao mara akilima matunda ili auze kwenye viwanda vya juisi
Ni kweli kabisa mkuu ulichosema, nakumbuka nı Muhongo huyo huyo alijitokeza kwenye vyonbo vya habari mwaka jana na kutamba kuwa, suala la mgao wa umeme litakuwa ni suala la historia kuanzia mwaka huu wa 2015 (Kwa maana ya kuwa hakutakuwa tena na mgao wa umeme, kwa nchi nzima)

Sasa mbona tunaendelea kupata endless migao ya umeme nchi nzima kila siku?!

Hivi kama Profesa Muhongo tutamuita aka Profesa 'Muongo' tutakuwa tumekosea?

Kwa hiyo huo anaouita uchumi utakaopaa na kuwa uchumi wa kati kwa nchi yetu mwaka 2025, hiyo maana yake, hiyo maana yake watakaopata 'neema' hiyo ya kupfikiwa na boom hiyo ya uchumi ni aina ya watu wa design ya waliorushiwa yale mabilioni ya Escrow kwenye account zao!
 
Vision 2025 ndio inasema hivyo sasa yeye kama Prof. alitakiwa kuonyesha yaani kutoa evidence kwa anachokisema!
 
lizaboni...umeme unaotumika mtwara nao ni wa gesi.bei ya umeme mtwara haupo wa bei ya chini.hiyo bei nafuu anaoahidi muhongo itatoka wp?

Tatizo ni kutupa ahadi milioni huku mkitufanyia kinyume cha mambo.Prof sio mtaalamu wa nishati yeye alisoma miamba.Tunajua unadanganya,kibaya zaidi hao wazungu wa magharibi wakigoma kutoa pesa zao umekwisha kabisa.2015 ni mgumu kuliko 2014.
 
10366327_585072384927714_8479812993842761565_n.jpg
 
Ni ujinga uliopitiliza na kujitoa fahamu kudhani kuwa wawekezaji kutoka nje ya nchi ndo wana umuhimu...
Kwamba wawekezaji kutoka nje ndo wanaweza kutusaidia kuwa kwenye uchumi wa kati.... Viongozi na wakubwa serikalini wamepigwa upofu. Kwa makusudi wanashindwa kujifunza kutoka kwenye uwekezaji wa madini, samaki, utalii, n.k.
Ninachofahamu ni kuwa kinachotetewa hapa ni rushwa ya 10%..... Shangaa uwekezaji mkubwa hivi unapigiwa chapuo ufanyike kwa misingi ile ile ya usiri baina ya mwekezaji na 'aliyemleta'!!

Uchumi imara; uchumi endelevu ni ule unaomilikiwa na wazawa... Nchi isiyowawezesha wananchi wake kutumia rasilimali zake kushikilia vyanzo vya uchumi na kuleta maendeleo itazidi kudumaa miaka nenda rudi!!

Kwa stahili hii ya kuwatetea wawekezaji wa kimataifa tena kwa jazba, kiburi, dharau dhidi ya matakwa ya wazawa... nchi haitapata manufaa ya maana...!!
Wajanja wachache watapiga hela ña kutajirika kutipitia rasilimali za wote kwa manufaa yao na ya ndugu zao!!
 
Back
Top Bottom