Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,930
Prof. Muhongo amemnukuu Rais Kikwete na vision 2025!! RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE: NATAKA KUWA RAIS WA MWISHO KUONGOZA TANZANIA MASIKINI | Blogu Rasmi ya Ofisi ya Rais
Mimi nadhani Hawa wote ni wana siasa na ni wababaishaji, Wazungu walisema ' a bird in hand is more worthy than 10 on top of a tree' Leo anatupa Tumai kwa uchumi wa gesi ambao uko 10 years away, na hata wakati huo at an unexplainable costs zilizotumika Leo. Wakati easy win kwa yeye, Ingekuwa Leo angelazimisha Sumatra kupunguza bei ya reja reja ya Mafuta equivalent na punguzo la world markets ( Mafuta yamepungua kutoka usd 132 to usd 57) toka mwezi wa August mwaka jana, ingewalazimu au angewalazimisha Tanesco wapunguze rates, na hata reflection ya usafiri kwa watanzania ingekuwa Nafuu. Leo wenzetu Kenya wamepunguza Mara mbili, sisi bei zimekomaa pale pale . Yeye haoni kama hiyo ingemrudishia credibility kidogo. Kweli Maneno ya Mengi kuhusu huyu professor yanaanza kuniingiaKama tunaongelea utendaji kazi katika baraza hili la Mawaziri la Jakaya Mrisho Kikwete, no doubt, Prof. Muhongo ranks top. Nasema hivyo kwa dhamira hasa. Ni Waziri pekee ambaye hana unafiki wala kutafuta kujipendekeza kwa yeyote, huwa anasema kile kilichopo moyoni mwake na kile anachokiamini.
Ni bahati mbaya sana Watanzania tumezoea unafiki, tunapenda sana kusifiwa hata tusipostahili. Professor Muhongo, kwa kauli zake amewaumiza wengi, hasa wanaoamini kuwa huwa hawatakiwi kuambiwa ukweli katika udhaifu wao.
Ningetamani sana kama siku moja tutakuwa na baraza la Mawaziri lenye mawaziri wote wa namna ya Muhongo. Tukifikia hapo nidhamu ya utendaji kazi serikalini itarudi. Kwa sasa Muhongo ana maadui wengi, kuanzia wizarani pake kwa sababu ni mwepesi sana wa kuwaambia anayoamini ni mapungufu yao, na anapotamka hamung'unyi maneno.