Maajabu kwenye maziko ya Nabii Eliya

Maajabu kwenye maziko ya Nabii Eliya

Msitutanie hapa:

Waliochukuliwa MBINGUNI wakiwa hai
1. Eliya - alichukuliwa na Gari la Moto ( wa kwenye Biblia) siyo huyu feki.
2. Enoko
3. YESU Kristo.
4. .................... mwenye kumjuwa aniongezee hapa.
5......Abednego
 
Hapa tunaandaliwa kisaikolojia msije kushangaa tukaambiwa amefufuka au ametwaliwa mbinguni akiwa hai
Hawa wawekezaji wa kiimani ni sheedah$
 
Napata sana shida mtu anapojiita nabii,mtume,nabii wa manabii,eti adam wa pili!Siku si nyingi kuna mtu atajiita yeye ni roho mtakatifu na wafuasi atakuwanao wa kutosha na watuwa watetezi wake.

Nimeanza kumsikiliza na kumjua Mwalimu Mwakasege kwa miaka 17. Bado ni yule yule,hana ulinzi,hana ufahari,haja jibandika majina ya ukubwa.
Sasa hao wachungaji wa sasa wameanza biashara juzi juzi,mara wafuasi hao,utajili huo!injili yao kuu ni utajirisho tu.Siku saba za juma we unaenda kusali,Utatajiri utaupataje?
Mkuu nilikuwa naangalia kipande kimoja cha video kutoka kenya kinaitwa "makri ya injili" mbona nilichoka, mpaka sasa nikisikia mtu sijui anajiita mtume au nabii roho yangu inapata ukakasi wa kuamini hata punje ya haradani
 
Mtume wa mwisho ni Mohamed na hakuna mwingine. Ni ufreemason unawafanya watu wajiite watume.
 
Eee Mungu tuepushe na masihi Dahal, kwa wasio mjua huyu Masihi Dajal ( Mpinga kristo kwa wenzetu wakristo) Mungu anasema atakuja siku za mwisho za uhai wa dunia,, huyu atakuwa na miujiza kweli , ataponya na kufufua wafu, kuhamisha milima na mengine mengi, kila utakalo mtaka akufanyie ili usadiki uungu wake atafanya. huyu atawakumba na kuwaangamiza wengi sana. Huyu kwa mujibu wa dini yangu atauwawa na Yesu, ( Issa A.S) na hii itakuwa moja ya mission ya Yesu ( A.S) kurudi kwa mara ya pili duniani. KIBAYA NI KUWA WAKATI MASIH DAJJAL ANAKUJA TAYARI MILANGO YA TOBA NA KHEIR ITAKUWA ILISHA FUNGWA... Kwa kawaida wenye imani haba tu toka enzi za Yesu ndo waliamini kwa kuona miujiza mfano ni Tomaso. ukiona mtu anakimbilia kanisa flani kisa kuna miujiza ujue huyu imani yake ni haba. unatakiwa umuamini Yesu A.S kwa kuamini mandiko yake sio mpaka mazingaombwe ya Nigeria.
 
In fact ni mashetani yanatotumia jina la mungu vibaya
now labda ni kuni za wenzie huko mbele za haki
 
Nilifikiri watu wangejadili hicho kinachoonekana kwenye picha na kuonyesha kama ni usanii umefanyika vipi, lakini watu wanaponda tu.
Mkuu LIKUD elezea kilichotokea na ilikuwaje na siyo picha tu bila maelezo ya kutosha.
 
VIFO VYA MITUME​

Mathayo - Alikufa kwa kuuwawa kwa upanga mbali kidogo na mji wa Ethopia.

Marko - Alikufa kule Alexandria baada ya kukokotwa kikatili kwenye barabara ya mji.

Luka - Alitundikwa juu ya mti wa mizeituni katika nchi ya Kigiriki ya kimaendeleo.

Yohana - Alitiwa kwenye pipa la mafuta yanayochemka lakini hakufa kwa njia ya miujiza na baadaye akapelekwa kwenye Kisiwa cha Patimo ili afe hata hivyo hakufa huko. Alikufa huko Efeso miaka 100 BK.

Petro – Alisulubiwa kule Rumi kichwa chini miguu juu mwaka 67 BK.

Yakobo Zebedayo – Alikatwa kichwa kule Yerusalemu mwaka 44 BK, Mdo 12:1-2.

Yakobo wa Alifayo – Alitupwa kutoka kwenywe kinara na kisha kupigwa na rungu
lenye misumari mpaka kufa, mwaka 62 BK.

Batholomayo – Alichunwa ngozi akiwa hai mpaka akafa.

Andrea – Alifungwa kwenye msalaba huku akiendelea kuwahubiria wale watesi
wake mpaka kufa.

Thomaso – Alishindiliwa mkuki ndani ya mwili kule Klemandel nchi
ya India ya mashariki.

Yuda Thadayo – Alipigwa kwa mkuki mpaka akafa.

Barnaba wa Mataifa – Alipigwa kwa mawe kule Thesolonike.

Mathayo – Kwanza alipigwa kwa muda mrefu na baadaye akakatwa kichwa.

Paulo – Aliteswa kwa muda mrefu na baadaye kukatwa kichwa kule
Rumi na Mfalme Nero mwaka 67 BK.

Historia hii ya vifo vya Mitume aliiandika Dk. Mulu Bale wa Ikizu store – Kororogwa Kibaha. Aliinukuu kwenye kitabu kinachoitwa NIGHTSMATER BOOK OF ILLUSTRATIONS.

nimekuwa nikikupa like siku zote ila kwa ili no! siyo kila kitabu ukikisoma unakiamini kwa 100% fikiria zaidi kwanza
 
Nilifikiri watu wangejadili hicho kinachoonekana kwenye picha na kuonyesha kama ni usanii umefanyika vipi, lakini watu wanaponda tu.
Mkuu LIKUD elezea kilichotokea na ilikuwaje na siyo picha tu bila maelezo ya kutosha.

Hakuna. La ajabu lililotokeA mambo ya kisayansi
 
Back
Top Bottom