Maajabu 8 ya mkoa wa Mara

Serikali imeufanya mkoa wa Arusha Kama Kitovu Cha Utalii ( Makao Makuu ).

Ndio maana hata Manyara hainufaiki na vivutio vyake, mpaka Tanzanite mishe mishe zote Arusha wakati iko Manyara.
Unapofanya kitovu kuwa sehemu as arusha kuna umuhimu wa kugawa mapato kwa mikoa inayochangia mapato kutoka kwenye hiyo sector, mfano mapato yote ya serengeti yanaingia hazina je, hazina wanafanya direct divide ya revenue kwa mikoa hiyo?.
 
Sikujua Serengeti iko mkoa wa Mara, najua wazanaki , wajita na wakurya tuu hao wengine sijawahi kuwasikia, mna serengeti na wasomi kibao lakini maskini wakubwa hamna hata maendeleo na mna nyumba za tope kuliko za bati, mna shida kuliko chawa
 
Sikujua Serengeti iko mkoa wa Mara, najua wazanaki , wajita na wakurya tuu hao wengine sijawahi kuwasikia, mna serengeti na wasomi kibao lakini maskini wakubwa hamna hata maendeleo na mna nyumba za tope kuliko za bati, mna shida kuliko chawa
Sawa
 
Kanda ya ziwa naona Mara na Kagera mnahujumiana wenyewe.Mna wasomu wengi ila mmeshindwa kuendeleza mikoa yenu. Ukienda Bukoba au Musoma pako kama vimiji vya mwaka 1945 licha ya mikoa hiyo kuwa na wasomi wasio na faida ya kuendeleza mikoa yao, msilaumu Kilimanjaro wenyewe hamsaidiani na mna roho ngumu
 
Sikujua Serengeti iko mkoa wa Mara, najua wazanaki , wajita na wakurya tuu hao wengine sijawahi kuwasikia, mna serengeti na wasomi kibao lakini maskini wakubwa hamna hata maendeleo na mna nyumba za tope kuliko za bati, mna shida kuliko chawa
wana wasomi wengi kama ndugu zao Bukoba ila mikoa yao inachekesha kweli
 
1. Kiwango cha chini sana cha ushirikina
2. Ulaji wa Nyama ya kuchoma nu ugali wa mtama
3. Wale jamaa wanapenda sana kukopesha kwa riba.
4. Ni wakarimu sana, hapohapo ni wagomvi sana
5. Ni nadra sana kukuta mwanamke mkurya Malaya
6. Usijaribu kuoa single maza aliyezalishwa na mkurya hata kama wameachana.
7. Sabato ndio dini kuu huko.
8. Wingi wa hayo makabila wanasikilizana, wanashea majina yaleyale na tamaduni zile zile,
Jina la jumla wanaitwa Wakurya.
9. Mkurya sio mzulululaji sana kama wasukuma, wengi hubaki kuishi kwenye mikoa yao.
10. Tarime ni wilaya Giant kuliko zote mkoani Mara, ila ni mji mgumu sana kwa mtu asiye mzawa kustawi huko.
Watakuwa wanakugeuza kuwa mradi kwa kukuvamia..
11. Mara inaongoza kwa kuwa na polisi wengi waliozaliwa huko.
Siro, Wambura, muliro, na yule CDf aliyekufa na miaka 104 jina limenitoka
 
Umemsahau mkuu wa majeshi Mwita Kyaro pia. Na Musuguri
 
Musuguli, Nyerere alijua tabia yao ya kupenda ugomvi, ujasiri hivyo wengi aliwaita jeshini baadae kwa kutaka kuoneka majasiri wakawa wanajiunga jeshi. Mwanaume wa kikuria akiwa mwanajeshi kila mzazi anaona fahari binti yake kuolewa na mwanajeahi hivyo wanakuletea binto bure uoe ndio maana Musuguli alikuwa na wake wengi.
 
Mambo mengi umeeleza vizuri lakini historia yako imebase zaidi kwa wakurya kuliko makabila mengine.
Mimi pamoja na kuwa na asili ya huko makabila mengine nimeyajulia ukubwani.
 
Nimetembelea Mkoa wa mara, nakupinga kwa nguvu zote.
Hakuna mtu wa huko atakupa binti yake bure. Jiloge uende ujaribu kuchukua au kurubuni kujionyesha sijui una nyota ngapi ngapi, unataka mkamwana bure, utarudi hapa kusimulia ukiwa huna mkono mmoja au jicho moja.

Watu wa huko mabinti ni assets.
 
Bahati nzuri namjua Musuguri kwa karibu, si kwa kufanya naye kazi ila kimahusiano na familia, kila akirudi alijuwa anakabidhiwa mke bure.
Wazazi walijuwa wanaona fahari mtoto wao kuolewa na mkuu wa majeshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…