Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,706
- 149,945
Naona watu wanawathumu maafisa wa serikali waliokuwa na dhamana ya kusimamia madini kuwa huenda walihongwa kutuhujumu lakini binafsi najiuliza tutapa wapi ushahidi kuwa wamehongwa?
Vile vile najiuliza tutawashitaki vipi na kuwatia hatiani iwapo ACASIA hawakubaliana na findings za kamati na hii inaweza kuwa ni moja ya sababu itakayolazimisha uchunguzi huru.
Nachokiona hapa labda ni uwezekano wa kuwashitaki kwa matumizi mabaya ya madaraka na uzembe kazini lakini hili la kuwatuhumu kuhongwa naona ni gumu sana kulitolea ushahidi mahakamani.
Hata waliosaini hii mikataba sijui nao tutawabana kwa ushahidi gani?
Anyway,labda kwa kuchunguza mali walizonazo na kutawaka watoe maelezo ni vipi wamepata mali hizo pamoja na kuchunguza miamala ya account zao ingawa sidhani kama nao wanaweza kuwa wajinga kiasi hiki cha kuweza kutumia account zao kufanya miamala itakayowatia matatani.
Mpaka leo najiuliza ni maelezo gani Chenge alitoa ingawa hakushitakiwa na watu wakaridhika kuhusu vile vijisenti na kama Chenge alifanikiwa sijui ni kwanini na hawa wasifanikiwe kujitetea iwapo nao watakutwa na vijisenti.
Mimi naona hii imekula kwetu ila sasa ndio tujifunze na ikibidi tuje na sheria ya kunyonga wahujumu uchumi na utekelezaji wa hukumu hii usisubiri idhini ya Raisi.
Tumechoka.