Maafa kutokea muda wowote Tanzania baada ya BUSARA kutoweka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maafa kutokea muda wowote Tanzania baada ya BUSARA kutoweka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, Oct 17, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Busara ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu.

  Katika kusoma kwangu falsafa kwa muda mrefu nimekumbana na maandiko mengi sana yanayohusudu busara na kuipa thamani ya juu kabisa kuliko kitu chochote kile.

  Pale busara inapotea miongoni mwa watu wa mataifa basi hali ya baadae ya watu huwa mashakani na maisha ya watu huwa katika
  hatari kubwa.

  Kwa maana halisi ya falsafa ni mapenzi ya busara au Maarifa. Falsafa kwa kiingereza ni philosophia inatokana na maneno mawili ya kigiriki yaani "PHILO" ambalo maana yake ni mapenzi na "SOFIA" ambayo maana yake ni busara basi ukiunganisha hivyo vitu viwili
  unapata PHILOSOPHY, yaani mapenzi kwa busara.

  Maarifa na busara ni mambo mawili muhimu sana kwa uhai na maendeleo ya binadamu. Bila busara na maarifa vizazi vya binadamu vitaangamia. Ujinga huua na kuangamiza vizazi, bali busara huokoa.

  Kitabu cha mfalme suleiman cha methali kinatuambia kunapokuwa "hakuna maono watu huangamia".

  Ni maono pekee yanayopelekea dira ya watu na kujua wapi wanaelekea bila maono binadamu huangamia.

  Wakati binadamu wanapoacha kutumia fikra walizopewa na mwenyezi mungu na kuendekeza matamanio ya mwili na tamaa za mwili basi maisha ya binadamu hupotea katika njia yake stahili.

  Sio nia yangu kuandika dini au falsaha bali kujadili mambo yanayotokea na kuonekana dhahiri miongoni kwetu kwasasa. Mambo yanayotugawa na kuondoa umoja wetu kama Taifa na kufuta kabisa dira yetu na mwelekeo wetu kama Taifa.

  Plato anatueleza vita vyote huletwa na mwili na matamanio yake na ndio hivyo hivyo Biblia inatueleza na Quaran inatueleza.

  Ni ukweli usiopingika binadamu wameumbwa waishi kwa amani na upendo pamoja na ushirikiano.

  Taifa letu liko kwenye migawanyiko mikubwa mno.

  Ninaweza kuitaja kadhaa ambayo kwa hakika inahitaji akili zenye busara ili kuunganisha vipande hivi ambavyo vinaonekana kukua kwa kasi.

  Nitaanza kuendelea Ubaguzi wa kidini na kutokuheshimiana miongoni mwa dini hizi kuu mbili.

  Mdomo wa binadamu ni kitu chenye faida na chenye madhara makubwa mno. Mdomo huunganisha watu lakini mdomo huo huo hugawanya watu. Mdomo huleta uadui lakini mdomo pia huleta urafiki, Tutawezaje kuchunga mdomo usiotulia unaotema hila, uongo, ulaghai na kuleta migawanyiko miongoni mwa watu? Mdomo haujatulia, mdomo hautunzi siri una haraka sana ya kunena bila hata kufikiri, mdomo hujitukuza na kutaka sifa.

  Ni dhahiri ya kwamba ni muhimu tuchunge midomo yetu kwakuwa uhai wetu upo katika midomo yetu. Ni muhimu pia tubadilishe jinsi tunavyofikiri ili tuwe na mabadiliko ya kimatendo.

  Migawanyiko ya kidini ni kati ya migawanyiko mibaya sana. Na moto wake hauzimiki haraka. Hujenga chuki na uhasama kwa vizazi vingi kwenye chuki hakuna busara, hakuna fikra, bali watu huongozwa na hisia za chuki zinazochoma Nafsi zao na kuwaunguza, wanakuwa vipofu wa ukweli.

  Ni muhimu sana kutokupandikiza chuki katika Taifa hili
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  E Mungu tuepushe na ubinafsi, taifa letu lij angamia.
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu, The meaning ya shule uliyoshuka imekaa vizuri! Lakini Adjust basi ... ikae vizuri!!
   
 4. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tulipofikia ni afadhali kujaribu kuzima moto unaowashwa na akina ponda na redio imani kabla haujasambaa nchi nzima. Hata kama vita haepukiki lakini inaweza kuwa ndogo kuliko sumu ya ponda na Farid ikiendelea kuachwa. Bado kuna waislamu wengi tu hawataki vita na kama itatokea watakuwa upande wa Watanzania wanaoombea taifa letu amani.
   
 5. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Tuliowapa madaraka na uamirijeshi mkuu yaani mkuu wa majeshi yote yupo kwenye world tour na sasa yupo oman anakula tende!
   
 6. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuchomwa kwa makanisa Zanzibar, Bagamoyo na Mbagala na hatimaye kukamatwa kwa mtoto wa kikristo aliyekojolea koran katika utani wa kitoto busara na hekima ya wakristo imeongezeka maradufu kuepusha nchi na vita ya kidini hakuna mkristo aliyeandamana kudai mtoto yule atoke au kudai mahakama kumwachia mara moja.
   
 7. p

  promi demana JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods naomba muweke ule waraka wa Godblees Lema kwa Rais Jk kuhusu hali tata ya udini nchini kwetu.

  My beloved country Tanzania, i will gone mis u.

  Bye bye Tanzania.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Umeeleza jambo zito sana juu ya nafasi ya busara ktk maamuzi yetu. Sijui shule za viongozi wetu wa siasa na wa dini zinasemaje kuhusu busara.
   
 9. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yesu kiristo na Mtume Mohamed (S.A.W) walijaribu haya haya anayofanya Ponda kuigeuza dunia kuwa na dini moja lakini hadi kifo chao hawakufanikiwa. Wengi tumeambiwa walitumwa na Mungu ndio maana wanaitwa mitume lakini bado walishindwa mission hiyo, Je leo Ponda ataweza ambaye ni binadamu wa kawaida tu kama sisi?????

  Hakika anatumia muda wake vibaya akiwa bado hai pengine hata muda wa kupeleka watoto wake shule nzuri hana. Muulize Ponda ni shule ipi aliyopeleka watoto wake kusoma kisha wakabaguliwa kwa sababu ni waislamu hatakuwa na jibu.
   
 10. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...teh teh...anatangaza nchi kwa ndugu zetu wa 'damu' jamani...au ndio kajificha..
   
 11. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jiulize kwa nini Maaskofu wa kikristo akiwemo Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania Malasusa walisusa ziara ya Rais Kikwete mbagala na kumtuma Fupe wa KKKT ni ishara mbaya kwani ziara ya Rais ilikuwa ni muda mzuri kusikiliza mtazamo wa mkuu wa nchi na hatua ambazo angechukua nadhani kuna jambo si jema linakuja.
   
 12. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bye bye Tanzania.

  Nilikupenda sana lakini tofauti za kidini zinakupenda zaidi.
   
 13. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo linalonishangaza Mtume Mohamed na Yesu wana nguvu kuliko Mungu ..... mimi ni mwislamu yule ni mkristo.
   
 14. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kunapokuwa "hakuna maono watu huangamia".
   
 15. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wako wanaoamini kwamba kwa kuanzisha vita na ukristo kutainua uislamu kwa mtazamo wa Ponda.

  Hana maono tusubiri kuingia vitani tutapata majibu mbele ya safari kama Ponda alikuwa sahihi au alitudanganya.
   
 16. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Vita around the kona!
   
 17. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Wamemlea Ponda kwa muda mrefu alitakiwa awe hayupo siku nyingi kwani ameshapanda mbegu mbaya kama Osama kwa shanta ambao hawana kazi akiwadanganya kuwa huo ndio msingi wa kiislamu. Tunamwombea afe mapema na waliochoma makanisa wapigwe plague hadi watakaporudi kwa makanisa waliyochoma kupiga magoti kutubu na kulia.
   
 18. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  hivi kweli ccm na kikwete wanajua kuwa mbuyu ulianza kama mchicha
   
 19. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Jambo la kufanya kwa haraka ni kupiga marufuku shughuli zote za kuabudu zinazofanywa nje ya nyumba za ibada na kwamba vipaza sauti viwe kwa ajili ya kusikilizana ndani ya nyumba za ibada na kamwe si kupeleka mahubiri kwa watu wasiokuwa ndani ya hizo nyumba za ibada. Mh. Raisi usiogope kutoa agizo hili ingawaje litapingwa na wengi wanaoona njia ya kupata waumini ni kupitia mahubiri ya sehemu za wazi PakaJimmy Kitila Mkumbo Mkandara Mzee Mwanakijiji
   
 20. K

  KITENGE KOFIA Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 14, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najaribu kuwaza kama si misingi aliyoweka mungu wetu yesu,mpaka sasa tanzania ingeshawaka..we love u jesus our lord and savior
   
Loading...