Habari za muda huu...
Leo nimewaza jinsi madalali wanavoharibu soko la vitu TZ ila ni sisi wenyewe ndio tunawaendekeza sana, nikiangalia vyuo vyetu UDSM, DIT, MUST etc etc wanazalisha ma IT kibao kila mwaka ila wote wanaishia kutengeneza website ambazo ndani ya mwaka zinakufa.
Leo naomba niwaulize kwanini hawa IT wasitengenezee LEGITIMATE real estate website ambazo wenye Nyumba/mali ndio wanapost wao wanakua wanalipisha tangazo hilo ila lazima wafanye verification na mwenye mali na kuweka details zote
Unajua nchi yetu Ujanja Ujanja mwingi sana, kila mahali dili (hawa madalali ndio wanafanya bei ziwe juu) ila akitokea IT mmoja aisee hamtaamini macho yenu.
nimeweka mfano wa web mojawapo kwa nchi za wenzetu.
Kama mtu akatengeneza Website ya Hivi kuna mtu atahitaji Dalali kweli? mwenye mali anaweka tangazo lake anatafutwa moja kwa moja na mteja.
mlioko vyuoni hii inaweza kuwa Project yako
tembelea
Kijiji.ca
kwa kuangalia website inavofanya kazi, zipo nyingi ila hii ndio kama Jamii forum kwa bongo kwenye kutafuta kupanga na kupangisha