Ma HR wenzangu, tuwasaidieni hawa vijana

Hapana, hapana hukutenda haki wala uadilifu.

Uadilifu ni kulitenda jambo ki haki bila kumpendelea wala kumuumiza mtu.

Mwizi ikigundulika kaiba basi haki na uadilifu juu yake ni kumfunga tu bila kujali kama ana familia inamtegemea ama nini.

Haki ina sifa ya kuto pinda, haki siku zote ni nyoofu na wala haiangalii unaitenda kwa nani ili mradi mwenye haki yake na apewe.

Umemdhulumu bure kijana wa watu kisa umri.
 
Daah! Sasa ungekuwa ujatenda haki kijana kukaa kwao siyo ndiyo kigezo cha yeye kuwa na unafuu wa maisha, inawezekana yeye kwao ndiyo kichwa cha familia.
Umefanya jambo jema ila ningekua mimi ningetumia vigezo tofauti kidogo .Kama mmoja kati yao ameanza kujitegemea kwa maana amepanga na mwingine anaishi kwao, basi yule anayeishi mwenyewe(anajitegemea) angepita bila kupingwa.
 
Ninyi ndio mnaua makampuni/mashirika kwa kuajiri watu kwa kuwahurumia.

Kampuni Haiwezi Kuajiri Mtu Kwa Kuwa Ana Shida, Umri Umeenda Au Atatue Shida Zake.

Wala Kampuni Haiajiri Watu Kwa Lengo La Kujaza Nafasi.

Mtu Yeyote Hata Kama Yukoje Au Ana Elimu Gani, Kama Anaweza Kutatua Kile Ambacho Kampuni Inakitaka, Ndio Anastahili.

Ndio Maana Makampuni Makubwa Kama Google, Facebook, Safaricom, Clouds Media, VodaCom Hawana Muda Na Degree Siku Hizi.
Umeambiwa hao wote wawili walifika final na walikuwa na sifa wote tofauti ni mmoja alikuwa na kigezo cha ziada ambacho mimi binafsi naona hakimtofautishi sana na mwenzie. Unawezaje kusema hana uwezo? It's not like alichukua CV zote za waliotuma maombi then akachagua mwenye umri mkubwa
 
Niccolo Machiavelli

HR mwenzetu kitu ulichofanya sio cha kiungwana hata kidogo na hupaswi kuja hapa kifua mbele na kujiona kuwa una huruma kwani uhalisia ni kuwa umri wa mtu hauwezi ukakupa picha halisi ya muhusika mambo ni Vice Versa so ukweli utabaki vilevile kama unataka kuajiri basi usiajiri kwa upendeleo bali kwa uwezo wa wahusika tu kwani ukitaka kuchimba personal issues za mmoja utajikuta unafanya wrong choice.
 
Umefanya kitu cha kiungwana kumchagua Yes, ila tukija katika proffesional ethics ni kwamba umempendelea basing on non merit factors like Age, race, colour, religion, sex, national origin, political affiliation, sexual orientation, gender identity, marital status, disability, genetic information etc

Na kwa yule aliyekosa ina maana umembagua kutokana na umri(discriminate against age).

Next time take care ingawa hukuwa na bad intention.
 
Back
Top Bottom