Profesa: Waalimu wenzangu, hivi mnawafundisha nini hawa vijana?!"

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
120
250
TUJIKUMBUSHE..

"WAALIMU WENZANGU, HIVI MNAWAFUNDISHA NINI HAWA VIJANA?!"

MWAKA 1995. KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU, CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)

download (33).jpeg


Moja ya maeneo ambayo Prof. Lipumba alifika kufanya kampeni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ilikuwa ni katika chuo cha usimamizi wa fedha, IFM

Ukumbi ulijaa hadi kufurika. Uadui ulioonyeshwa na hadhara iliyokuwepo ulikuwa wa juu na wa wazi mno kiasi kwamba ungeweza kuuhisi kwenye hewa. Huu uadui ulikuwa ni wa nini?!

Profesa Lipumba alipokaribishwa tu kuzungumza angani kuliinuka msitu wa mikono, wote wakitaka kuuliza maswali!

Profesa Lipumba aliwapuuza akajaribu kuendelea kuzungumza. Minong'ono iliyokuwa ikizizima chini kwa chini sasa ililipuka na kuwa kelele. Nilimwandikia Profesa Lipumba ujumbe kwenye karatasi na kumsihi apokee maswali ya hao waliotaka kuuliza, au shughuli nzima ingeharibika.

Baada ya kuusoma ujumbe wangu Profesa Lipumba alisita katika hotuba yake, akamnyooshea mmoja wa wale walionyoosha mikono juu huku akionekana kuchachawa sana, na kumwambia:

"Haya Uliza"

Alisimama yule kijana huku uso ukiwa umewiva kwa ghadhabu.

"Unataka kutuambia nini wewe! Wewe ulikuwa mshauri wa raisi. Ulimshauri rais vibaya mpaka nchi ikaingia kwenye hyperinflation. Leo unakuja hapa eti unataka urais!"

Alisema yule kijana.

Profesa Lipumba alinyamaza mpaka akajiridhisha kuwa yule kijana alikuwa amemaliza. Ukumbi mzima ulikuwa unalipuka kwa shangwe! Profesa Lipumba aliangalia huku na kule, akaiinamia kisemeo (microphone) na kuuliza:

"Waalimu wenzangu, hivi mnawafundisha nini hawa vijana?! Kijana wa IFM leo hajui tofauti kati ya hyperinflation na inflation ya kawaida?!"

Ukumbi mzima ulipoa ukatulia kama umemwagiwa maji.

Profesa Lipumba alianza kutiririka vitu ambavyo nadhani katika historia ya chuo hicho walikuwa hawajawahi kuvisikia.

Ghafla watu, walimu na wanafunzi walitoa notebooks wakaanza kuandika kwa kiu kubwa, yale aliyokuwa akiyasema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba aliongea kwa saa nzima. Alipomaliza ukumbi ulilipuka kwa shangwe! Kila mmoja sasa alitaka kumpa mkono Profesa na kupiga naye picha! Wote walisahau kwamba walimkaribisha kwa uadui wa wazi.

Huyo ndiye Profesa Lipumba! Mzalendo ambaye wachumia tumbo wana hofu naye kubwa! In sha Allah Watanzania watakuelewa tu!
 

parts

JF-Expert Member
Mar 31, 2018
1,729
2,000
Huyo mzee anasababisha uprofesa uonekane kitu cha kawaida sana.
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,696
2,000
Kashindwa kuongoza chama,ataweza kuongoza nchi,CUF ilikuwa chama kikuu Cha upinzani,bara na visiwani,leo hii,hakuna kitu,
 

Maili tatu

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
424
1,000
Ohoo watu wanafundishwa udongo tu.lipumba sasa atulie tu afanye mengineyo mbona anaweza akaeleweka hata nje ya cuf aisee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom