Ngoja leo tuambiane ukweli Vijana wenzangu namna ya kufanikiwa kiuchumi

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,398
Wewe una miaka 40+ bado huna Nyumba, Huna Gari. Hata ukija pata umebakiza miaka 20 au 10 ya kuenjoy. Miaka 40, 50 hukuwa na gari unapata pesa badala uwekeze kwa wanao ndio unaenda nunua gari. Ili iweje sasa? Anyway kama una usafiri endelea kutumia. Huo na Sehemu ya kujihifadhi. Nyumba tunajenga wenye pesa na kumiliki magari pia.

Haina haja ya kupaka maneno rangi, tuambiane tu ukweli vijana wenzangu wa Kitanzania. Maisha hayana Formula ambayo ni constant (never changes)

Nimeangalia maisha ya watanzania wengi ni maisha ya kupambana toka day one anapozaliwa. Mtoto anaanza kukutana na misuko suko akiwa tumboni mama yake. Kunyanyaswa na Manesi, kutukanwa na kukosa maisha matunzo mema.

Mtoto huyu anapozaliwa bado anakuja oneshwa Dunia ilivyo kwa machungu. Unakuta mtoto anapambana sana hakuna anachopata kirahisi.

Ukiacha sisi ambao tumezaliwa na Golden Spoon. Wengi wanakuwa na hard time na wanajifunza upambanaji toka wakiwa wadogo. Wanakuwa kwa mapambano mpaka kufikia umri huu ameshapambana mara nyingi na Malaria, Pepopunda, Degedege, Tetekuwanga, Kuhara, Minyoo, Typhoid, Mafua, Kifua, Kurogwa n.k na kuibuka mshindi.

Hii spirit huwa kwa vijana wengi inakoma akibalehe. Kutoka hapo unakuta kijana sasa anaanza kupambana kwa mambo ya kipuuzi. Anaanza kupambania wasichana. Hapo ndo anaanza poteza mwelekeo.

Sisi ambao wazazi wetu walikuwa na pesa toka mwanzo tunazaliwa ktk mazingira mazuri. Huwa mara chache nawaambia kuwa shida pekee iliyokuwepo home ni kuwa kila kitu kipo.hata wakati wa kula unashindwa kukataa kusema sitaki pizza nataka Chips kuku. Ili washindwe kuzipata usile. Unakuta vyote vipo mezani (buffet) kama hotelini.

Mimi siku pekee nlijifunza kutokuwa na kitu nlipomuuliza Mzee kama ana ndege Binafsi akasema hana. Ndo hapo nikagundua kumbe kunakukosa pia. Ila magari yote mazuri yapo n.k

Anyway. Sasa unapoenda pata Elimu unapaswa ujiulize ninyi ambao mnatumia mfumo huu wa Kiswahili wa Elimu( Mimi nlisoma Cambridge)

Unatakiwa ujue unaenda kusoma ili iweje?uwe nani? Na kwanini ukasome?

Watu wengi wanasoma kwa fashion.kuwa watu wote wanasisitiza shule so naye anaenda kusoma.

Nliwahi mshauri mtu mmoja aachane na kumsomesha mtoto wake chuo. Jamaa hakunielewa. Akamsomesha mpaka Kumaliza Degree ya Udaktari. Yule bwana mdogo hakuwahi enda fanya kazi kama Daktari. Amefungua mabanda ya kuuza Chips mengi ndo anaendesha maisha yake. Mwaka wa 4 huu. anasema ameshaanza sahau hata Udaktari n.k

Baba yake analalamika. Namwambia nlikushauri kipindi kile hukunielewa.

Haiwezekani wote tusome. Na akili za mtu hazipimwi kwa mfumo huu wa Formal Education.

Kama ukimchukua Samaki na Panya ukataka wapima akili kwa uwezo wa Kuogelea. Ni wazi Samaki ataonekana ana akili sana kuliko Panya.

Utahitimisha kuwa Panya hana akili. Samaki ni Intelligent. Lakini kumbe hukutumia vipimo sahihi kwa specimen hizo mbili. Wana tabia tofauti na uwezo tofauti.

Huwa nawaambia watu mchezaji kama Messi au Ronaldo ni Intelligent katika field yake. Its possible Darasani hakuwa mzuri. Ukamlazimisha asome na A reseat mara kadhaa ukimpotezea muda. Leo hii Messi/Ronaldo asingekuwa alivyo.

Haya maisha namna yako ya kufanikiwa unayo wewe. Sikiliza your instinct inakwambiaje? Usilazimishe kuwa somebody ambaye hutoweza kuwa.

Wangapi wanajuta kwa kupoteza muda kusoma na wasifanikiwe kiasi kile walichotaka? Wangapi waliacha au kukomea level flani ya Elimu leo wana mafanikio kuliko wenye Degree,Masters au PHD?

Kuna kipindi Mfumo unakukataa makusudi. Unagoma unataka pambana unapoteza kile ambacho mfumo mwingine ulikuwa unakihitaji from you.

Waliofanikiwa na kuwa vile walivyo kutokana na Elimu ni kwa kuwa Mfumo huo ndio ulikuwa njia sahihi kwao.

Unapofeli kwenye njia moja jiulize sababu ni nini. Kuna mtu anasema alifanya mtihani vizuri kabisa ila matokeo yalikuja amefail.hakuelewa ame fail vipi. Au alikuwa ana akili lakini alifail kwenye mitihani.

Pengine hii ni njia ya kukupeleka kwenye kusudio lako halisi. Akili ile ikatumike kwenye jambo jingine kubwa.

Angalia. Wajasiliamali wakubwa,matajiri waajiri. Si watu wenye Elimu kubwa sana ya Darasani. Wengi walikuja ongezea kusoma kwa leisure wakiongezea katika kile ambacho walikuwa wame master tayari.

Ukiacha sisi wachache ambao tumetajirika toka kwa wazazi na pia Elimu ikaendelea kupaka rangi maisha yetu. Wengi ni waliokuwa Daraja la pili au Tatu Darasani Kielimu ndio wamekuja kuwa waajiri Matajiri.

Wazungu wanasema anything you are good at contributes to your happiness. Lolote uwezalo lifanya vizuri linachangia kwenye furaha yako.

Ukifikia hatua ukaamini your instinct ambayo inakwambia wewe si wa kusoma. Ingawa umefaulu una Division 1/2 but wewe ni mtu flani. Ukasema jamani siendi Chuo. Nafanya jambo hili. Ujue umefikia hatua ya kujielewa.

Then simamia unachoamini. La msingi ni how do you channel your ability to the right purpose.

Inawezekana we mzuri sana wa kutongoza. Achana na mademu tumia hicho kipaji kushawishi watu ukifanya biashara wawe wateja wako uingize pesa badala ya kutoa.

Inawezekana wewe ni Tapeli mzuri sana. Achana na Utapeli anzisha mradi ambao ule ujanja ujanja wa kutapeli watu utatumika huko positively.

Una tabia ya uongo uongo. Acha uongo kuwa mwandishi wa stories. Utauza na ukitunga na Movies au Tv Series.

Sikiliza sauti yako and chase your dream.hukuumbwa eti wewe kazi yako iwe ni kuchanganya tu wasichana. Hapo maana yake ulipewa talent then unaitumia isivyopaswa.

Ni sawa na kuivisha kidani cha dhahabu pua ya Nguruwe.haiwezekani wote tukaajiriwa. Haiwezekani. Haiwezekani wote tukaenda Darasani na kupitia hii mifumo yenu ya Elimu nchi maskini mna enda kukariri mpaka mna maliza.

Kijana ufanye nini?
1. Jitambue wewe ni nani

2. Unataka nini?

3. Utafanyaje?

4. Amua, halafu wekeza katika maamuzi yako. Ukiinuka usitizame tena nyuma songa mbele.hakuna kujuta.

Umepambana na malaria,pepopunda,tetekuwanga,surua,kifuakikuu (ninyi wengine mlikuwa na minyoo mpaka inakuwa mingi inatokea puani na mdomoni) na magonjwa yote ya utotoni. Ukashinda.

Sasa acha ujinga ukubwani unataka kushindana kuwa na wanawake wengi. Badala ya kuhamishia mapambano katika maisha. Kubali kujifunza kwa watu wenye Uelewa wa jambo flani. Halafu fanyia kazi.

Nachelea kusema kuwa mimi nmeanza endesha gari nikiwa na umri mdogo sana. Hivi sasa maisha haya na uzuri wake huwezi nidanganya kuwa eti nihangaike na msichana. Msichana ndo atahangaika na mimi.

Mimi nampa msichana pesa 1,000,000 halafu akianza kunipigia pigia simu namwambia aniache kwa sasa nahitaji pumzisha akili naenda Zanzibar then Arusha. Ile pesa nlimpa tu kama msaada.

Na ndo maana sometimes nawaambia napenda nipate mwanamke mzuri na mwenye akili. Dada mmoja nimuuliza nikimpa Mil 20 atafanyia nini. Akanambia ataenda kununua Usafiri Toyota Harrier. Nikamuuliza utafanyaje service na kuweka fuel? Maana hakuwa na kazi. Hapo kwenye gari GMC nina Mil 25.

Akainamisha kichwa chini, nikagundua pengine anamaanisha sehemu zake za siri ndo zitalipia. Nliinuka nikaenda kwenye gari nikachomoa tu mil 2 nikamwambia atumie nauli aende home mi nmepata dharura. Akashukuru sana na kutaka nikiss nilimkumbusha kuwa nlimwambia no touching no kissing.

Alishapagawa kwa Mil 2. Kesho yake nikamwambia asinitafute nipo busy. Nikaacha kuwa na ukaribu naye. Maana angeniambukiza Upumbavu tu. Unapo date Mwanaume/Mwanamke Mpumbavu automatically unanyonya Upumbavu wake.

Vijana tufanyeni kazi, hasa ninyi ambao hamna cha kurithi kwa wazazi wenu zaidi ya madeni na maradhi,masimango na mikosi. Fanyeni kazi kwa bidii katika kila jambo unaloweza lifanya. Go extra mile. Usizimie moyo. Aluta Continua
 
Kwa kweli je kwa wale vijana wasio na connection tufanyajee
 
Sijui kwanini akili inaniambia wewe ni Chizi Maarifa katika ID nyingine,

Ila kiukweli katika siku zote leo nimekuelewa ulichoandika, aisee hii ni kama umeniandikia mimi

Kama nisingetumia miaka yote niliyotumia shule kusomea huu ujinga niliousomea nadhani sasa hivi ningekua mbali sana kimaisha
 
Yaani Umesomea mtaala wa Cambridge halafu unaandika vizuri Kiwashili kuliko hata kidhungu!! 😇

Anyway, mada yako ina mafunzo mengi kwa vijana ukiondoa hizo taizi na kiki ulizo jipa kama kawaida yako.
Hebu nikosoe nilipokosea kiingereza ili nikulipe pesa. Huwa hizi roho zenu za chuki ndo umaskini wenu. Nafahamu lugha zaidi ya nne fluently like a native speaker. Wewe endelea kubaki na roho ya wivu, chuki na husda.
 
150 Reactions
Reply
Back
Top Bottom