Hamza Mohamed Hassan azikwa makaburi ya Kisutu, Dar. Mazishi yachelewa kutoa risasi zilizokwama mwilini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,135
Hamza Mohamed Hassan aliyefanya mauaji pale Selender bridge azikwa. Jamii, rafiki na ndugu zake Wamzika

====

Dar es Salaam. Mwili wa Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na jeshi la Polisi amezikwa leo Jumapili Agosti 29, 2021 saa 2:30 usiku katika makaburi ya Kisutu.

Mwili huo umezikwa baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Mamuur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Awali mwili huo ulitarajiwa kuzikwa saa 7 mchana katika makaburi hayo, lakini msemaji wa familia Abdulrahm Hassan alisema mwili huo ulichelewa kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama.

mazishi-pc-data.jpg

Chanzo: Mwananchi Digital

Zaidi...

HAMZA MOHAMED AZIKWA LEO: Mwili wa Hamza Hassan Mohamed umezikwa usiku huu kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kusaliwa katika Msikiti wa Maamur.

Hamza alifikwa na umauti baada ya kufanya mauaji ya askari polisi watatu na askari mmoja wa Kampuni binafsi ya Ulinzi ya SGA na kisha kufyatuliwa risasi na polisi iliyopelekea kifo chake.
 
Back
Top Bottom