M4C ndani ya Ndanda ~ Masasi

Kweli Chadema hawafanyi makosa! Nilimcheki kamanda akihitimisha baraza la M4C jana huko Ndanda pale alipowakumbusha kuwa CCM ni marehemu na wawe makini kung'amua hilo. Niliachwa hoi na art aliyotumia na kuwaacha hoi halaiki iliyokuwa inamsikiliza. Kwa maneno yake mwenyewe alisema:

"Kupe; si mnamjua kupe? Kupe akishamndandia ng'ombe yeye basi keshamaliza safari. Ng'ombe anapelekwa gulioni kupe yupo; ng'ombe anauzwa kupe yupo; ng'ombe anachinjwa kupe yupo tu; ng'ombe anachunwa ngozi kupe yupo tu; ngozi ikianza kuchomwa ndo kupe anazinduka, 'alaa, huyu jamaa kumbe kachinjwa!'

Waosha magamba mpooo?

Sasa ndio nini hicho?
 
Wewe ambaye hujaelewa,alimaanisha kwamba watu wajivue magamba wasiwe kama kupe kung'ang'ania hata mzoga ambao ktk lugha ya fasihi ni ccm.watu wafunguke macho ngombe angali mnadani.yeah hiyo ndo m4c bana.
 
Mlitika= Mtikila , umechakachua tu kiaina lakini bila kuongeza wala kupunguza herufi jina lako ni mtikila

Usipotezee kizoba zoba; kamanda anakuongelea wewe na kupe wenziyo kuwa huyo ng'ombe keshakuwa mzoga hakuna cha kunyonya tena; liachieni!
 
Ukisikia ambiguity ndiyo hiyo hapo kwenye RED inayofuatiwa na BLUE. Sina haja ya kusema mengi kwa kuchelea mada husika kuitoa toka kwenye mwelekeo uliokusudia!!!
Yaani amefanya chini juu, juu chini. Halafu bado anabisha.
 
Hata mimi niliiona hiyo. Jamaa aliniipress sana. Afu umati ulikuwa nyomi mbaya. Makamanda naona wamejipanga sana safari yao ya kusini. nilisoma hapa JF hii ratiba ya Dr. wa ukweli, A.K.A. Prof. Slaa:

Katibu mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa ameelezwa kuwa mpiganaji asiyechoka kutokana na kazi kubwa anayofanya huko kusini tangu CDM ianze operesheni Okoa Kusini wiki moja iliyopita.

Taarifa kamili zinasema Dr Slaa amekuwa akihutubia mikutano mitatu kila siku ambapo kwa siku zote hali chakula chochote mchana kutokana na kubanwa na muda.

Baada ya mikutano Dr Slaa anaongoza mikutano ya ndani mpaka saa 6 usiku na kisha anakuwa wa kwanza kuamka na kuwaamsha vijana wake waanze siku nyingine ya mapambano.

Imedaiwa pia kabla ya kila mkutano Dr Slaa anazindua matawi katika mitaa yote ya eneo husika.

Source: Kamanda Mwesilwa Perfect aliyeko kikosi kinachoongozwa na Dr Slaa katika opere


Nahisi hii ndiyo ratiba ya makamanda wote huko kusini.

Kweli Prof. Slaa ni kisu cha moto.... yaani naona kwa mbaaali mnara wa kijani wa Babeli ukianguka, maana magamba yamegonganisha lugha.
 
"Kupe; si mnamjua kupe? Kupe akishamndandia ng'ombe yeye basi keshamaliza safari. Ng'ombe anapelekwa gulioni kupe yupo; ng'ombe anauzwa kupe yupo; ng'ombe anachinjwa kupe yupo tu; ng'ombe anachunwa ngozi kupe yupo tu; ngozi ikianza kuchomwa ndo kupe anazinduka, 'alaa, huyu jamaa kumbe kachinjwa!'

Dah wanadamu wanamisemo! hii kali

Salam kwa Magamba hiyo,
akina Rejao bado wameganda kwenye ngozi,
wakati ngozi imeanikwa batini subirini ngozi inazidi kukauka.
 
tehe tehe tehe, eti vyama vya musimu, sasa ni full mzuka pale magogoni
 
aksante wadau nafurahi kuona thread niliyoanzisha inachangiwa,nilihaaidi kupost picha,bahati mbaya flash imeleta shida,badala yake nitapiga hard kopi kwa digital then iwe soft kopi kama proof kwa wanajamvi,picha na Kamanda Lema siku ya Jumapili tarehe 3 June hapa Ndanda.
 
Back
Top Bottom