M4C Masasi Balaa...

Bartazar

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
1,043
565
Katika kile kinachoonekana kwa wananchi kuipokea nguvu ya mabadiliko kwa hamasa kubwa, wanakijiji 150 wa kijiji cha Mnavira Masasi wamejiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Wanabodi mnaweza kupata picha juu ya idadi hiyo, kijiji hicho hakina idadi kubwa sana ya watu, hivyo kupata idadi hiyo ya wanachama, ni kama robo tatu ya kijiji. Viongozi wa wilaya wanaendelea kupokea mialiko kwa ajili ya kupokea wanachama wapya na kufungua matawi!

Katika hali nyingine, mbunge wa Masasi Mariam Kasembe alijikuta kwenye wakati mgumu alipokuwa akitembelea jimbo, kwenye kijiji cha Mpanyani baada ya kushindwa kujibu Maswali kutoka kwa wanakijiji na wanakijiji wakaanza kuzomea! Aliishia kupanic na kupanda gari lake kurudi mjini! Baada ya hiyo sintofahamu habari za uhakika ni kwamba aliimwagiza mtendaji aorodhesha majina ya waliomzomea,na alipelekewa hayo majina na mtendaji huyo. Kisha alilipeleka suala hilo polisi na kuwapakazia vijana hao kuwa walimtishia kumuua!

Vijana hao waliwekwa ndani na sasa hivi wapo nje kwa dhamana!
Majuma kadhaa yaliyopita Makamanda wa CDM Masasi walitembelea kijiji hicho katika vuguvugu hili na kuwapa wananchi mbinu za kuwahoji viongozi wao kuhusu uwajibikaji wao kwao na utekelezaji wa ahadi walizozitoa wakati wa kampeni...!
 
Anawawekan ndani vijana leo lakini baada ya miaka 2 atawafuta kuwaomba wamsaidie kufanya campaign! Sijui wakati mwingine watu wanafikiria nini?
 
CCM B mpooooooo?

Sasahivi sijui wako wapi baada ya kuondoka na wale wanachama wao wanaowatembeza mikoani kufuta aibu ya kukosa watu.
Walipiga kelele kwamba wanakwenda kwa akina nshomile lakini sijawasikia tena.
Au fungu la mafuta kwa ajili ya coaster 15 limemalizikia Arusha?
 
Back
Top Bottom