M4C inaweza kuwa kuipeleka CDM Ikulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

M4C inaweza kuwa kuipeleka CDM Ikulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Aardvark, May 6, 2012.

 1. A

  Aardvark New Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau JF.
  Napenda kutoa changamoto ili kuweza kupata mawazo chanya juu ya mustakali wa chama chetu tukipendacho.
  Moja ya jambo ambalo limekuwa likinitatiza sana ni jambo la uwazi na uwajibikaji ambao chama chetu kimekuwa kikipambana nacho kwa maisha yake.
  M4C ni wazo zuri sana hasa tunapoongelea chama kinachoamini kwenye nguvu ya Uma. Na hili halina ubishi hata kidogo kwamba CDM ni chama cha watu. Wasiwasi wangu hapa siyo kuchallenge wazo la M4C bali kuangalia changamoto zilizoko mbele yetu na uzoefu uliopo juu ya fedha ambazo chama kwa namna moja imeshafanya. Moja ya tukio la chama kukusanya pesa jwa ajili ya shughuli za chama ni kwenye tukio la kuwaaga mashuhaa walouwawa kwenye maandamano ya tarehe 5 Jan2011. Wote tuliokuwepo pale watakubaliana nami kuwa zile fedha hazijawahi kutangazwa zilikuwa shilingi ngapi na zilitumika vipi, zaidi ya zile milioni 10 za Sabodo ambazo ndizo pekee zilitangazwa na matumizi yake.
  Chama tunaomba ufafanuzi kwani sasa tunaenda kwenye National level ya M4C tutakuwa tunawachangisha hawa masikini ambao kimsingi ndiyo watanzania walio wengi na unaweza fanya hesabu ndogo tu ya udadi ya watu waliokuwa pale uwanja wa NMC jana na kiwango cha fedha kilichopatikana.
  Wazo langu ni je M4C inweza kutuvusha 2015 kwenda Ikulu tukiwa salama? Naomba mawazo yenu wadau
   
 2. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huwa najiuliza ni nani muadilifu katika masuala ya pesa huwa sipata jibu. Kwa kweli kwenye pesa huwa hatuaminiani hata kidogo. Sijui lakini kwa upande wa hili. Hata hivyo mkuu umeandika maneno mazuri, ila nakushauri. Ilikufanya yakae vizuri hebu yasome kwa makini kisha hariri baadhi ya maneno
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Inawezekana taarifa ya mapato na matumizi ikawa imeshatolewa, lakini hawajaiweka wazi. Pamoja na hayo, zipo pia pesa zilizochangishwa, na mimi ni miongoni mwa waliochangia ni fedha wakati wa kampeni za m4c. Zile nazo hazijawahi kutangazwa kazi zilizofzywa. Ni vizuri zikatangazwa
   
 4. R

  RMA JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We gamba tuliza boli! Umetumwa? Mmemaliza pesa za ccm sasa mnachunguza za Chadema? Si kila jambo lazima lisemwe hadharani. Katika hali ya kawaida, jeshi linapokuwa vitani, mambo mengi huwa ni siri ya jeshi. Kwa mfano wanajeshi hawatakuambia ukubwa wa jeshi lao, idadi ya bunduki zao, idadi ya vifaru na idadi ya mabomu waliyo nayo. Na hiyo ni mbinu ya kumfanya adui asijue uwezo wa jeshi husika. Sasa ungependa kujua ili uchangie au?
   
 5. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Wahusika waweke wazi taarifa za michango inayo changwa. Ni muhimu kuweka wazi kuendelea kujenga imani kwa wachangiaji vinginevyo kutokutoa taarifa kutajenga wasiwasi wa pesa zetu.
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kweli, inabidi wananchi wapate taarifa za mapato na matumizi.
   
 7. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Punguza munkari ndugu, jamaa kama alichanga anayo haki ya kuhoji. Si kila kitu ni siri katika chama. Mambo yanayoshirikisha wanachama wote hayawi siri. Mbona mikutano ya hadhara haifanywi kwa siri. Iwapo michango ilichangwa hadharani bila usiri basi kinachopatikana lazima kiwekwe wazi ikiwa ni pamoja na kujua matumizi yake.
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tatizo la watu huondoka kwenye mikutano kabla mfano kilicho patikana jana kilitangazwa lakini wangapi wanajua kingine kama mtu unamwamini hutokuwa na wasiwasi na vitu kama hivyo..
   
 9. D

  Di biagio Member

  #9
  May 6, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kuwa na nafasi ya CAG ndani ya chama la sivyo zitaishia kwenye matumbo binafsi.
   
 10. A

  Aardvark New Member

  #10
  May 6, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo kuondoka kabla kwani hata kiwango kilichopatikana jana kilitangazwa hata wale wasiyokuwepo wanajua kiasi gani kilipatika. Pale Naura Spring kilitangazwa pia kwa maana hiyo kila mdau anajua. Hoja yangu hapa siyo tu kilichopatikana ila matumzi pia yanatakiwa kuwa wazi.
  Tofauti na hapa nina wasiwasi huko tunapokwenda italeta shida na inaweza ikatumiwa vibaya na wasioitakia mema CDM.
  Kwa mfano ni shilingi ngapi zilipatikana siku ya kuwaaga akina Shirima pale NMC? Na kama unakumbuka wabunge wote wa CDM walitakiwa kuchangia sh. 100.000.00 kila mmoja. Pia wananchi na wapenzi tulichanga pale uwanjani. Je wote walitoa na kama walitoa ni shilingi ngapi zilipatikana toka kwa wabunge pamoja na michango mingine mbalimbali? Je matumizi yake yalikuwa vipi? Taarifa hizo zinzpatikana wapi ama nani aulizwe?
  Tutakapokuwa na utamaduni wa kutoa taarifa itawafanya wananchi wawe na moorali ya kuchangia zaidi. Tofauti na hivyo tutegemee counterparts kuanza kuipotosha
   
 11. A

  Aardvark New Member

  #11
  May 6, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna gamba hapa. Na kama tunataka kwenda mbele na kuvuka salama lazima tujitofautishe na hawa magamba ambao hawana wala hawataki kuulizwa na kama tutaendelea na hii tabia ya kuogopa kuhojiwa then what is the different then?
   
 12. G

  Grayson Member

  #12
  May 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mkuu Crashwise,
  Wewe ni mtu muhimu sana humu JF. Kama una-access na wakuu wa CDM basi wafikishie hizi taarifa. Kuwe na taarifa ya mapato na matumizi hasa kwa hela zinazochangwa na walalahoi kwenye mikutano. Lkn na wewe unapopata taarifa yeyote iweke wazi. Kwa mfano wewe unafahamu kiasi gani kilichangwa jana basi weka hadharani kwa faida ya wale wasiojua, iwe waliondoka mapema au hawakuwepo kabisa. Kuna sababu nyingi zinazoweza kumfanya mtu aondoke mkutanoni mapema. Kwa mfano ndugu zetu wanaolinda usiku muda ule ndio wa kwenda kujiandaa. Kuna baadhi ya watu hawachangi sio kwa sababu hawana nia ya kutoa ila ni kwa sababu wanataka kujua matumizi ya fedha zinazochangwa
   
Loading...