Serikali iendelee na sensa. Takwimu zitakapotoka watu wasije kulalamika kuwa hawakuhesabiwa au kwa huduma hjazitoshelezi kwa sababu serikali itakuwa inatumia takwimu zisizojumlisha baadhi ya watu bila kujali ni madhehebu gani. Tunaingia kwenye mchazo mchafu kwa vigezo vyovyote vile.
Mkuu Petrol, zoezi la sensa ni la lazima sio option kama uchaguzi, its a must hakuna room ya kusema anayetaka!.
Mimi nawaunga mkono ndugu zetu Waislamu ili kikiongezwa hicho kipengele cha dini na cha kabila tutakipenyeshea hapo hapo angalau tujue wale Wahdzabe waliokuwa 250 sasa wamebaki wangapi. Miaka ya 80 iliwachukua kinguvu watoto wao 4 na kuwasomesha boarding mpaka la 7 hakuna aliyefaulu, lakini wote wanne wakapelekwa Pugu na kusomeshwa mpaka form four, wote walipata Div. 0!. Wakarudishwa kwao msituni ili kupeleka civilization kwa ndugu zao ikiwa ni pamoja kuwajengea nyumba za kisasa na kupewa nguo na vifaa vya kisasa!. Baada ya mwezi mmoja serikali ilirudi kuwatrace ilikuta vile vitu vyote walivyowapa viko pale pale walipoviacha na yale makazi yakiwa kama yalivyo na more surprising hata zile nguo za wale wasomi 4 nazo walizivua na kuziacha!.
Hivi tutaendelea kuwategemea wazungu mpaka lini?. Wazungu watuhesabie tembo wetu, Mama Jane Goodhall atuhesabie sokwe wetu!, sasa hata makabila yetu nayo ndio tusuburi wazungu watuhesabie?!.
Tulipopata uhuru tulikuwa na makabila milioni 12 na makabila 120, kwa wastani wa watu laki moja kila kabila, sasa tunaenda milioni 50 kwanini tusijue na makabila!.
Mfano wangejua kabila linaloongoza kwa procreation ni kabila gani ili elimu ya uzazi wa mpango iwe concetrated huko na makabila gani yana hatari ya kufutika ili yaingizwe kwenye 'endagered species' ili kuyalinda!.
Wangapi kati yenu mnajua Watindiga wamebaki wangapi?, Wahadzabe, Wasandawi, Wataturu Wabalungi, Wakonongo etc. etc.
Kuna ubaya gani kujua tunawapagani wangapi, Hindu, Budha, Bahai, Baniani, Waislamu wa Ahamadiya, Waislamu wa Shia, Waislamu wa Sunni, Waislamu wa Ismailia, Waislamu Makadiani etc?. Kuna ubaya gani?.
Kama rais wa kwanza wa Tanzania alikuwa Mkatoliki, Mkapa nae ni Mkatoliki, Membe, Dr. Slaa na Magufuli nao ni Wakatoliki wanaosubiria kupangishwa pale nyumba nyeupe!, kuna ubaya gani tukiwajua wako wangapi, na Anglicana wangapi, Walutheri, Waadvetisti Wasabato, Memonite, Walokoke etc. etc. Hivi kuna ubaya gani?.