M-PESA.TIGO PESA na MAHUSIANO...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Kama ilivyo matumizi ya simu yalivyo badili mahusiano

sasa kuna hili la matumizi ya kutumiana pesa kwa njia ya simu

m-pesa,tigo-pesa..airtel money,z pesa na kadhalika.......

je unafikiri mahusiano yame athirika kwa kiasi gani sasa?????

nini kimeongezeka zaidi?faida? au hasara??????

kwa uzoefu wangu wanaume wengi 'wanaona hii teknolojia' imewasaidia wanawake

zaidi since wanaume ndo 'main provider' kwa sehemu kubwa ya jamii....

imekuwa rahisi 'kuchunwa' kwa kupigiwa tu simu na kutakiwa utume pesa....

na wengine wanaona now ni rahisi hata 'kumzidi mtu' maarifa kwa njia hii

na wengine wanaona 'utapeli' wa mapenzi na 'wizi' umerahisishwa......

je wewe waonaje ?

uzoefu wako ukoje kwa hili????????
 
mi naona imenifanya niweze kushare kidogo kilichopo na mpenzi wangu.nikpungukiwa pese ya mboga nanirushia elfu 5
 
A "blessing in disguise"! Na kwa jinsi mitandao hii inavyosumbua naona kama ni rahisi kukwepa....japo kwa muda tu!:lol::lol:
 
ha haa utaikwepa hadi lini?????
 
Ukikitumia kitu vibaya lazima upate athari zake....btw Boss naomba umwambie Lily Flower hapo chini namsalimia sana..muulize kama ana M PESA nimtumie hela ya kununua mchicha nasikia siku hizi umepanda bei fungu linauzwa buku...
 
Kama ilivyo matumizi ya simu yalivyo badili mahusiano

sasa kuna hili la matumizi ya kutumiana pesa kwa njia ya simu

m-pesa,tigo-pesa..airtel money,z pesa na kadhalika.......

je unafikiri mahusiano yame athirika kwa kiasi gani sasa?????

nini kimeongezeka zaidi?faida? au hasara??????

kwa uzoefu wangu wanaume wengi 'wanaona hii teknolojia' imewasaidia wanawake

zaidi since wanaume ndo 'main provider' kwa sehemu kubwa ya jamii....

imekuwa rahisi 'kuchunwa' kwa kupigiwa tu simu na kutakiwa utume pesa....

na wengine wanaona now ni rahisi hata 'kumzidi mtu' maarifa kwa njia hii

na wengine wanaona 'utapeli' wa mapenzi na 'wizi' umerahisishwa......

je wewe waonaje ?

uzoefu wako ukoje kwa hili????????

Dont blame the technology. Its matter of how u use it.
 
Hapo sasa....ukisema M-PESA ipo down anakwambia nirushie kwa Tigo-PESA! Hapa ndio umuhimu wa kuwa na line moja tu unapokuja...Lolz!

kuna wadada 'nitumie tigo pesa '
imekuwa kama salaam..lol
 
TB, umenikumbusha aisee, ngoja nimpige mzinga mtu manake anajidai alipo hamna bank,lol!
Note: CRDB ndo wameharibu mambo kabisaa! Ukijisajili mobile banking, unahamisha hela kutoka kwenye account yako kuingia m-pesa ama airtel money and vice versa. So kama huna hela kwenye m-pesa unahamisha from ur account, huna pa kuchomokea baba, nifanyie kale kazawadi kangu ka xmas basi,lol
 
mimi nilishakula vichwa vingi saaaana kwa njia hii
ujue inakuwaje
cheki hii
mpesa man: upo smile
smile :nipo my dear

mpesa man:ushakula baby wangu
smile fix: nimefulia dia leo sili

mpesa man:mmmh baby wangu usile na mimi nipo nikufate?
smile: hapana boss yupo siruhusiwi kutoka leo

mpesaman: basi nakutumia hela kidogo ya lunch.

smile:usjali dear usijitese nipo ok

mpesa man:nimekutumia laki moja dear laki si pesa mbonaa?
smile:mmmh thax anyway bye dia

idumu milele huduma ya mpesa na tigo pesa
 
The Boss aka Denzel..

Nadhani hizi huduma zimeathiri sana mahusiano..mimi naona mtu kama anakupenda kwa dhati hawezi kukuomba omba pesa kila saa unless ni shida genuine..mjini watu wanaishi kwa mahesabu siku hizi!
Kwa namna nyingine imerahisisha kutuma huduma ya pesa kwa wanandoa waliopo mbali mbali kama kutumiana pesa haraka kwa shughuli za kifamilia&maendeleo.
 
mimi nilishakula vichwa vingi saaaana kwa njia hii
ujue inakuwaje
cheki hii
mpesa man: upo smile
smile :nipo my dear

mpesa man:ushakula baby wangu
smile fix: nimefulia dia leo sili

mpesa man:mmmh baby wangu usile na mimi nipo nikufate?
smile: hapana boss yupo siruhusiwi kutoka leo

mpesaman: basi nakutumia hela kidogo ya lunch.

smile:usjali dear usijitese nipo ok

mpesa man:nimekutumia laki moja dear laki si pesa mbonaa?
smile:mmmh thax anyway bye dia

idumu milele huduma ya mpesa na tigo pesa

huu ni ujumbe kwa wanaume
tugome kujiandikisha m pesa na tigo pesa
mimi siku zote hujibu 'bado sija register' niki register nitakutumia lol
 
Mie naona imeongeza matatizo hasa kwa wamama wa nyumbani maana ukiomba hela ya matumizi unambiwa sina hela kumbe ziko kwenye simu.
 
TB, umenikumbusha aisee, ngoja nimpige mzinga mtu manake anajidai alipo hamna bank,lol!
Note: CRDB ndo wameharibu mambo kabisaa! Ukijisajili mobile banking, unahamisha hela kutoka kwenye account yako kuingia m-pesa ama airtel money and vice versa. So kama huna hela kwenye m-pesa unahamisha from ur account, huna pa kuchomokea baba, nifanyie kale kazawadi kangu ka xmas basi,lol

Kinga'sti sweetie
mimi simu yangu ni sasa tel
na benki yangu ni daresaalm community bank....
sijui nikutumie vipi honey ?lol
 
huu ni ujumbe kwa wanaume
tugome kujiandikisha m pesa na tigo pesa
mimi siku zote hujibu 'bado sija register' niki register nitakutumia lol
nadhani nyie wenyewe huwa mkiwa na salio zinawawasha mnapenda kuzigawa gawa so mlitaka tukatae?
 
Ukikitumia kitu vibaya lazima upate athari zake....btw Boss naomba umwambie Lily Flower hapo chini namsalimia sana..muulize kama ana M PESA nimtumie hela ya kununua mchicha nasikia siku hizi umepanda bei fungu linauzwa buku...

Wewe wewe hebu ni recharge kwa tigo pesa la aziz, sipokei salam mpaka unirecharge.
 
Back
Top Bottom