M-pesa, tigo Pesa, airtel Money na Maangamizo ya Uchumi wa Tanzania

Habari yenu wana Jf. Nimechukua nafasi hii ilikuongelea mashirika ya simu kujiingiza ktk biashara za kutoa fedha na kupoke kama ma Bank na vile yanavyo haribu uchumi wa Taifa letu. Unajuwa nilazima tujuwe uchumi wa nchi haupimwi kwa kupitia ktk utumiaji wa sim kama ma banks ila serikal inatumia ma bank kujuwa kiasi cha hazina yake.

Kuanzishwa kwa biashara za kutuma na kupokea fedha kunaleta madhara makubwa hasa kwa ma bank. Kutokana na kupunguza deposit ambazo zilikuwa zikifanywa hapo awali na watu. Kutumia sim as a means of bank, kunawatu wamefika hatuwa yakujivunia kutembea na pesa ktk m. Pesa. Huku wakisahau kuweka pesa bank inakupa riba,ila kuwa napesa ktk M pesa ni sawa na mtu kuchimbia fedha ardhini. Ninabaki kushangaa kwanin serikali imeridhia mashirika ya simu kuwaibia wanachi kwa kutoza gharama kubwa ktk kutuma na kupoke fedha kwa kiwango cha asilimia 200% tofauti na ma bank.

Pili uchumi wa tanzania unaenda kuhamishwa toka ktk ma bank nakwenda ktk mitandao ya simu? Jambo ambalo ni hatari sana, Prof Ndulu tafadhali tusaidie kujuwa ni kiasi gani ma bank yamepoteza as deposit tangau kuanza kwa mambo ya M. Pesa? Tukumbuke pesa iliopo bank ndio serikal inaweza kuikopa ama wananchi? Je ina maana M pesa anamkopesha nani?

Tatu hivi karibuni Tanzania bunge limepitisha AML ACT. Sheria ya kuzuwia utakasaji wa pesa? Je huon ma billion yalio potea serikalini yameenda kusafishwa via M. Pesa ? Nakurudishwa bank as white money? Jaman kwakwel hukunikukosa wasomi nakudharau kazi ngumu wanayo fanya ma bank. Je issue ya KYC INAKUWAJE? Serikali imekurupuka nakuleta tatizo ambalo lisipopatiwa dawa sasa basi taifa litakuwa kwenye maangamiz mengine ya kiuchumi.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake! Amen

Hakuna bank hapa nchini mkuu! kabda kama unaishi ughaibuni

hakuna reliable huduma za m pesa pia!! wizi na uongo mwingi

hakuna serikali pia! LOL!
 
Maoni yenu wadau nimeyasoma yote ila kumbukeni cheap ni haghali.

Watanzania wanapenda mchina sana kiasi tunashindwa kupambanua hathari zakiuchumi ktk hili. Hii ni sawa ulete mchele wenye sumu uwauzie watanzania kwa 1kg@Tsh1000/=. Nadhani utawauwa wote. Sii wasomi wala wasio wasomi we love cheap. Nahapa ndipo tunapo liangamiza taifa.

I love German maana ni moja ya mataifa yana vitu haghali ila durable. Nifafanue tu sipingi M. Pesa. Ila m. Pesa kufikia mpaka mamilion ku2ma ni hatari tena ni hatari bila kumumunya. Tena sasa hivi mpaka mishahara huu nauwita ujinga pasipo kufumba macho nakuvinyooshea vyombo husika kwakuwa vipofu ktk hili.

Mfano bank mtu anaweka fedha bure na kutoa kwa kati ya TSH 600 up to Tsh1000. Per Transaction of up to 25M. M. Pesa unatuma pesa 100.000/= kwa tsh2500/. Hii sio asilimia 200% ya makato? Nakuwanyonya wanyonge? Kumbe nibora kuwa na akaunti bank kuliko kufanya huu umasakuu? Pili kujuwa salio ni Tsh200 up 300 if not 400 ktk ATM. How much poor people charged for checking balance into M. Pesa? Kile mnasema kimeinua uchumi ni kama kujenga nyumba miamoja ktk kijiji zikawa unafuu kwa wananch kwa miaka mitatu ila kumbe zimejengwa ktk bonde mvua ikaja nakuzowa nyumba zote.

LEO NATAKA KUSEMA IKIWA HIZI HUDUMA ZA M.PESA NAZINGINEZO ZILIZOOTA KAMA UYOGA HAPA NCHINI HAZITO ZIBITIWA BASI TUJUWE UCHUMI WA TAIFA ILI TUNAUJENGA BONDEN AND AFTER 5YR SERIKAL ITAKUWA IKIPATA MAUMIVU MENGINE..

Wewe umesahau simplicity na urahisi wa huduma hizi kwa wananchi amabo kuaccess huduma za kibenki ni ndoto. Hebu fikiria jinis ilivyokuwa rahihi kuwatumia fedha wazazi vijijini, watoto shuleni, wafanyakazi mashambani n.k all this contributes positively kweny uchumi wa nchi
 
Nimejaribu kusoma ujumbe wako ila sijakuelewa vizuri...Labda upunguze hoja katika para moja na ujaribu kufafanua issue moja moja.

Mfano, bank gani hapa nchini zinatoa riba kwa saving accounts ambazo ndiyo wengi wetu tunazotumia?

Babu DC!

Mkuu hata kama hazitoi riba ila pindi ile hela yako inapokwa bank
inaweza akatolewa kama mkopo ktk secta mbalimbali za uzalishaji
ambazo zitachangia ktk kipato cha taifa pamoja na ukuaji wa uchumii
la inapokuwa ktk M pesa au togo pesa haiwezi kukopeshwa na kufanya
uzalishaji kama unaofanywa na bank ambao ndo kasema kuweka hela
kwenye hiyo mitandao ni sawa na kuichimbia chini
 
Nafikiri huifahamu huduma ya M-PESA umekurupuka kuandika. Huduma ya M-PESA haitozi 200% huo ni uwongo wa hali ya juu kuna viwango vimewekwa kama service charge.

Pili hakuna benki inayotoa riba kutokana na fedha unayoweka kama ipo ni kiasi kidogo sana.Huduma ya M-PESA imeasidia sana hasa watu wa vijijin wasio na access ya huduma za kibenk.

Mkuu embu ongelea ktk upande wa uchumi ina madhara gani?
 
Hizi ndizo kero za Mabenki yetu.

1. Process ya kufungua account katika baadhi ya mabenki yetu ndefi.
2. mlolongo wa documents, lete barua kutoka kwa ofisi za serikali za mitaa, n.k
3. amount ya kufungulia account ipo juu hadi 50,000,
4. Huweza ku-access account yako muda wote.
5. Gharama kubwa za uendeshaji akaunti (maintance fee)

lakini mpesa ni kitambulisho chako tu. mabenki wanapaswa kuboresha huduma zao, imekula kwao. HEKO MPESA,Tigo PESA, Airtel Money.
 
aise ni same things walau hata hao m pesa na tipo pesa wanakwambia wanachukua kiasi gani. Shenzy mabenki kwa maskini tunaibiwa wala haizai na afadhali uichimbie chini utakuta pesa haijapungua. Benki kama una laki mbili tatu kaa mwaka uone pesa inauvyopungua kingine kinaogopesha wananchi hicho. Hawa elektronic money m pesa tigo pesa wanakwambia wazi
 
Sasa hivi huduma za Mpesa, tigopesa nk zinaratibiwa na BoT. Nadhani kuna kiasi ambacho wametakiwa kukihifadhi BoT kama inavyofanyika kwa mabenki...
Benki zilikuwa na miaka mingi ya kuwafikia wananchi wote kwa kipindi tangu nchi ipate uhuru mpaka hivi karibuni kulipoanza hizi M pesa nk lakini hazikufanya hivyo. Mpaka mwaka 2008, wateja binafsi waliokuwa na akaunti benki walikuwa hawazidi laki tano katika nchi yenye wananchi milion 36 by then. So benki wajilaumu wao wenyewe... Walikuwa na nafasi ambayo hawakupenda kuitumia...
 
Back
Top Bottom