Mwana Kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2011
- 652
- 607
Umejibu sawa ila tatizo Voda imepandikiza watu wa kujibu humu ndani kutetea unprofessional conduct. Ni sawa na kusema mtu aliyepata ajali kwa uzembe asipate matibabu atajijua mwenyewe.Wanapaswa kuangalia kama kweli mteja katuma hela na aliyetumiwa hela kaipokea na kuitoa. Hapo ni kuisitisha kwa muda namba ya mteja aliyepokea pesa kimakosa mpaka atakapoirudisha. Kinyume na hapo hao voda wanaendekeza wizi kwa pesa za wateja wao.
Wewe utakuwa unatumia benki za vikoba za akina mama, mtumie mtu ela toka benk kwenda moja kwa moja kwenye simu yake kule jina litaenda lako na pia lake kabla kutuma litakuja.FEDHA IMETUMWA TOKA ACCOUNT YA BANK KWENDA MPESA NA HUWA HAIONYESHI JINA . Ingekuwa ni kama unavyosema isingekuwa rahisi. next time tumia maneno ya kistaarabu usifikiri wote humu ni watoto wenzako
Na siku hizi kwa mpesa hatua ya mwisho ni kuhakiki jina la mtu unayemtumia pesa. Nafikiri ni ngumu kwa jina la mtumiwa kimakosa kufanana na lile sahihi lililokusudiwa.Nadhani huwa unapata Ujumbe kuwa Hakikisha Namba Kabla ya kutuma Fedha zako, Makosa ni yako hapo sio yao!
Sio sawa kwasababu aliyetoa hela taarifa zake zinafahamika na proof ipo.Mkuu Hapo usiwablame Voda hata kidogo hata Mimi niliwahi kukosea Japo ka elfu hamsini ila ikapotea kwa sababu Muhusika aliitoa, ni sawa na wewe udondoshe Fedha kisha useme kwanini Polisi wasimtafute aliyeziokota!
Ni kweli aliyetoa namba yake ni 0759548521 na ni mteja wao na wakala ni wa VODACOM na location wanaijua hivyo mtu kukosea isiwe kigezo cha kupoteza hela zakeSio sawa kwasababu aliyetoa hela taarifa zake zinafahamika na proof ipo.
Pole mkuu... Ila kuna matukio mengine huwa mtu unatoa sadaka kwa staili nyingine...Nimetuma hela kwa mtu anaitwa Samweli Deus kimakosa na in ten minutes nikawapigia MPesa kwa dial 100 na niliongea na dada aliyeko kitengo cha lugha ya Kiingereza na akaniambia nimpe receipt number ya hiyo transaction. Amekuwa fasta kucheki na kuniambia niliyemtumia hela ameshazichukua kwa wakala na THEY CAN DO NOTHING na itanibidi mimi nimpigie mwizi wa hela zangu na akikataa niripoti polisi. Hii ilikuwa accident na sijawahi kosea tangu nianze kutumia hii huduma. Nimesikitika kuwa MPESa haina mechanism ya security kuhakikisha watumiaji wa huduma hawaibiwi. Kwao wanahesabu wamefanya business bila kujali mteja kaibiwa;. Nimejiuliza maswali yafuatayo:
1. VODA hawana uwezo wa kumtrack mteja wao aliyewaibia wateja wengine?
2. Namba ya aliyechukua hela zangu ni 0759548521 inakuwaje Vodacom wanashindwa kunisaidia kupata hela zangu na badala yake kuniambie is non of their business.
3. TCRA inawabanaje hawa wenye kutoa hizi huduma kuhakikisha fedha za mteja hazichopolewi hata pale anapokosea namba au ni kilio cha samaki.
4. Im sure voda wanamjua hata wakala aliyetoa hela na ni rahisi kwa wao kumtumia kumtia mbaroni mwizi ; how come hawataki kujishughulisha na kumwachia aliyeibiwa afanye negotiation na mwizi?
5. Aliyeibiwa yuko Arusha na aliyeiba yuko kanda ya Ziwa na wao wana muscles za kufuatilia nchi nzima ni kwa nini tusione kuwa MPESA siyo salama?
Naomba tusaidiwe hata kama tulikosea ili kupata hela zangu na bado ninaamini wana uwezo wa kufanya hivyo onlu nimekutana tu na VERY WRONG IRRESPONSIBLE AND SHORTSIGHTED STAFF.
Mkuu umenena aiseeMechanism ipo, ndo kama walichofanya. Bahat mbaya walikuta alishaitoa. But angekua hajatoa wangekurudishia. Again na ww tumia akili, inawezekana pia huyo mtu alikua anasubiri hela kutoka somewhere so hakua na shaka. Na pili, we unashindwa nn kumpgia umuombe akurudishie, sio kila mtu mhuni kama ww!
Kitu ambacho hakiwezekan pia ni voda kuzuia mtu aliyepokea hela eti asitoe kwa muda flan kwanza coz hiyo huduma sasa itakua sio efficient, itakua ina time lags na itakua haijasolve tatizo linalomaanishwa kuwa solved na huduma za e-money! E-money has to be instant and money received at real time when such amount is sent. Haitakiwi ku-hang yan haipo kwa mtumaji wala mpokeaji.
Narudia ushauri wangu kwamba kama mtu amepokea hela kimakosa na akatoa basi angalau awekewe shimo/deni kwenye akaunti yake ili akipokea hela nyngine akatwe! Ndivyo hata benki wanafanya ivo kama mteja atawekewa hela kimakosa na akaitoa/tumia.
Kwa bahati mbaya nimelala mlango wazi(nilijua kijana wangu amefunga kumbe nayeye alinitegea) halafu nikavamiwa na wezi halafu wahusika(polisi) hawajishughulishi kwasababu hatukufunga mlango...Ni kweli aliyetoa namba yake ni 0759548521 na ni mteja wao na wakala ni wa VODACOM na location wanaijua hivyo mtu kukosea isiwe kigezo cha kupoteza hela zake
Siyo salama kwa sababu hakuna mechanism ya kuhakikisha usalama wa hela ya mteja. Huyu mtenja ndiye anayeifanya MPESA iwe MPESA. Na kama hutamjali akaogopa kuitumia huduma lazima mpesa itayumba
Kosa ni mtumaji mana lazima uhakiki no plus jina ndio utume pesa,kuna mtu hajawahi kushika 50 elfu siku ikiingia anatoa fasta na kuhamia bar,heri ukosee upokee mwanamke kurudisha ni rahisi sana kuliko mwanaumehuo ni uzembe wa vodacom pia. sasa nini maana ya kusajili namba za watumiaji wa mtandao? kama wao wanaona shida wangekupa taarifa zake alizojisajili nazo umsake vizuri mwenyewe.
Umejibu sawa ila tatizo Voda imepandikiza watu wa kujibu humu ndani kutetea unprofessional conduct. Ni sawa na kusema mtu aliyepata ajali kwa uzembe asipate matibabu atajijua mwenyewe.
Well said ; ni kweli VODA hata picha ya huyo mtu wanayo na ingekuwa busara wakampigia tu kumweleza arudishe. hivi mtu aliyetuma hela yuko arusha na aliyezichukua yuko Mwanza je huu mchakato wa polisi na kufuatilia si utazidi kiasi anachodai? Voda onyesheni uungwanaHapa naona wengi tunachangia bila kuzingatia hoja ya msingi ya mleta thread, hoja ni kwanini kama huyo Mteja kwa mfano ni wa voda wenyewe wanashindwaje kuwasiliana na Mteja wao kama ingekuwa mitandao mingine sawa lakini huyo ni Mteja wao ni wao wenyewe ndiye waliye msajirj sasa anapofanya huo udanganyifu si ni wajibu wao kusaidia hata kwa kuongea nae kwa simu na kama kweli ikibainika amefanya udanganyifu wanaouwezo wa kusubiri akiweka pesa kwenye account yake wakazitoa na kumtumia aliyemfanyia udanganyifu huo. Ni vema kama tulivorahisisha utumaji wa pesa kwa mitandao ya Simu tukarahisisha pia utatuaji wa tatizo inapotokea mtu amekosea badala ya kuacha mfumo wa kawaida ufanye kazi ambao unashindwa kukidhi mahitaji ya wateja kama vile mtuma pesa yuko mbali na aliyefanya huo udanganyifu hata sura tu hamfahamu huko Police anakwenda na ushahidi gani si ni huo huo walionao hao Voda. Mi nadhani kweli wanatakiwa wajiongeze waweke kitengo cha kusaidia wateja wao wanapokosea kutuma pesa kwa baadhi ya wateja wasiowaaminifu.