Lyumba aachiwa kwa dhamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lyumba aachiwa kwa dhamana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 9, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Nora Damian
  ZIKIWA zimesalia wiki mbili ili amalize kifungo chake cha miaka miwili jela, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, amepandishwa tena kizimbani akikabiliwa na shitaka la kukutwa na simu gerezani na kasha kuachiwa kwa dhamana.

  Jana, gazeti hili liliripoti kwamba Liyumba angepandishwa kizimbani baada ya kukutwa na nyenzo hiyo ya mawasiliano kinyume na sheria ya magereza.Jana mchana Liyumba alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda.

  Wakili Kaganda alidai kuwa, Julai 27 mwaka huu, katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alikutwa akiwa na simu gerezani kinyume na Kifungu namba 86, kifungu kidogo cha kwanza na cha pili cha Sheria ya Magereza iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
  Hata hivyo, kabla ya kuendelea na kesi hiyo, Hakimu Mkazi Stewart Sanga, alilazimika kuiahirisha kwa muda na kuamuru upande wa mashtaka urekebishe hati ya mashitaka.

  Sanga alitoa amri hiyo baada ya upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Majura Magafu kudai kuwa, hati ya mashitaka ina upungufu wa kisheria hivyo mteja wao hawezi kukubali, au kukataa shtaka hilo hadi itakaporekebishwa.
  “Mashtaka haya yako kinyume cha sheria na mahakama haiwezi kumtaka mteja wetu aseme ndiyo au hapana, hivyo tunaomba hati yote ya mashtaka iondolewe,” alisema Magafu.

  Awali, upande wa mashitaka ulisoma shtaka hilo kwa kutumia kifungu namba 86 cha Sheria hiyo ya Magereza kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
  Lakini, Magafu alidai kuwa, kifungu namba 86 kilichotajwa na upande wa mashtaka hakijakamilika na kwamba, ili mtuhumiwa awe na haki ya kujibu lazima mashtaka yawe yanaeleweka na kifungu kiwe sahihi.

  “Tunaomba upande wa mashtaka wafanye marekebisho ya hati ya mashtaka, yanaweza kufanyika hata kwa mkono na watueleze wanamshtaki chini ya kifungu gani ndipo taratibu nyingine ziendelee,” alidai Magafu.
  Magafu alidai kwamba, hata kifungu namba 86 kifungu kidogo cha tatu nacho hakijengi kosa bali kinakataza tu na kutoa mamlaka kwa ofisa wa magereza kuitaifisha mali iliyokamatwa ama kuiharibu.

  Wakili wa Serikali alikubaliana na hoja za utetezi na kudai kuwa walimaanisha kifungu chote namba 86 kifungu kidogo cha kwanza na pili cha Sheria ya Magereza.
  Baada ya hoja hizo, Hakimu Sanga alikubaliana na upande wa utetezi na kuamuru upande wa mashtaka ufanye marekebisho yanayostahili katika hati hiyo na kuirejesha upya.

  Baada ya kusomewa upya mashtaka, Liyumba alikana na upande wa mashitaka ulidai upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

  Dhamana
  Wakili wa utetezi, Magafu aliiomba mahakama impatie mteja wake dhamana katika kesi hiyo kwa kuwa amebakiza muda mfupi kabla ya kumaliza kifungo chake.Magafu alidai kuwa mteja wake anatarajia kumaliza kifungo Septemba 23, mwaka huu hivyo anaomba apewe dhamana.
  Upande wa mashtaka haukupinga na Hakimu Sanga alitoa masharti ya dhamana, kwa masharti ya mshtakiwa kusaini dhamana ya Sh50,000 na kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika.

  Liyumba alitimiza masharti hayo ambapo alidhaminiwa na mfanyakazi wa BoT, Otto Hathangeus.
  Hakimu Sanga alisisitiza kuwa dhamana hiyo ni kwa ajili ya kesi hiyo tu.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 29, mwaka huu itakapotajwa tena.

  Kifungo chake
  Liyumba alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi, yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh221 bilioni.Baada ya hukumu hiyo alikata rufaa Mahakama Kuu ambako nako aligonga mwamba na kuendelea kutumikia kifungo hicho.Hivi karibuni alikamatwa gerezani akiwa na simu inayodaiwa kuwa alimpigia Rais Jakaya Kikwete.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,981
  Trophy Points: 280
  Braza Liyumba, pole sana.
  Mungu akunusuru ulimwe faini badala ya kifungo
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kuna uzi mwingine wa wklks unakuja juu ya vyombo vyetu vya dora kuingiliwa na watu wenye mamlaka katika maamuzi yao. Ni hilo tu.
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Source wapi??? Wewe unaandika eti ''kwa mujibu wa gazeti hili'', kwani JF imekuwa gazeti siku hizi?
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Liyumba haponi hata kwa hili, inaonekana ana siri fulani ndio maana wanamfinya
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,375
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Do pole sana Lyumba naona ulijisahau kumpigia mkuu simu, kama hakukusaidia mpaka unamaliza kifungo bado unadhani kuna msaada kweli?
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Lyumba amewasha mzigo mkubwa sasa jamaa wamemwambia wagawane akiwa ndan atakihata hiyo simu nasikia alikuwa akiongea na rais nini sijui
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Unaingizia taifa hasara ya Bilion 221 unawekwa gerezani only 2yrs, unakuwa unakula good time mpaka ki-black berry chako unacho. Eti week kama tatu ndo wanagundua kisa umemkorofisha mkuu na kilong longa chako...afu unafunguliwa toka kifungoni, hamna ulichotaifishwa maisha kama kawa unaendelea kula bata mtaani. ndugu familia kila mtu wako poa, ma-investment ya kufa mtu......Acha kabisa ONLY IN TANZANIA!!!!
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,424
  Likes Received: 12,692
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  JAMAA KACHOKA MKANDA UNAKARIBIA ZUNGUKA MARA YA PILI KIUNONI! JELA MBAYA SAAANA
   
 10. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Yule baba anatia huruma aisee.wizi mbaya
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Kipindi alichokuwa anawanunulia viescudo na Rav 4 hamkujuwa kwamba wizi mbaya?
   
 12. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  huyu kiumbe Kamaliza hukumu lini
   
 13. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,424
  Likes Received: 12,692
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  HAAAA NDO UMEAMUA KUTUTUKANA! ANGALIA JAMAA ANACHAIN NDEFU UNAWEZA JIKUTA NAWE UMO KWENYE LIST YAKE MUZEE!!!
   
Loading...