Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,907
- 1,081
Mkuu mm sipingi.
Huo umati ulioelezea hapo ni mkubwa mno kiasi kuwa hawa wawili tu ndio uliwaona ww (au umehadithiwa Mkuu?) pia si vibaya ushatusaidia, halafu zaidi heading inasema "wananchi wa Bukoba wataka...." wakati mkutano ni wa CUF waliohudhuruia hapo ni wanachama wa CUF(au niseme ni wa Lwakatare),halafu mkuu unaapa? unasema "...ukweli mtupu..."
Kwenye umati mkubwa unaweza kuhesabu mikono na kuona miwili tu?
Wanacheza hawa, either kulikuwa na watu wa kuhesabika, au hawakuweza kuthibitisha kwamba ni mikono ya watu wawili tu.
The whole presentation seems like there is a big PR move behind this, wote hawana imani yangu, si CUF wala huyu Lwaka nani sijui, wasanii watupu.
mkuu Bluray
Hili halikushangazi wewe tu, bali hata mimi.
Lakini nakwambia kama unayo source nyingine fanya homework yako badala ya kutaka kubadilisha ukweli kuwa uongo. Nini ambacho hakiwezekani?
Kama huu ni uongo, kaa hivyo hivyo ukifikiri ni PR mwisho wake utauona🙁
Pundamilia07,
Hapana mkuu mimi siitazami picha hii kama unavyoitazama. Kwanza kumbuka maelezo yote aliyoambiwa Lwakatare ni nje ya kiofisi, hakuna barua wala maelezo yalitolewa na uongozi wa CUF kwa nini jina lake halikuteuliwa kugombea tena kiti hicho, jambo ambalo hata mke wa Kaisali asingeweza kujisafisha maadam talaka imeshatolewa..Unajisafisha ili iwe nini?...utajisafisha wakati tuhuma zinapowekwa mbele yako na hujapoteza ndoa lakini sii baada..Lolote utakalo sema halina turufu kwani mume kisha fikia maamuzi ya kuvunja ndoa hata kama hukufanya baya lolote...kifupi ameshakuchoka!
Uamuzi uliofikiwa ni sawa na ule wa Mzee Malecela alipotaka kugombea Urais, jina lake liliondolewa hata kabla ya wajumbe kupiga kura. Kama kweli Lwakatare angekuwa hivyo wanavyodai basi hapakuwa na haja ya kuondoa jina lake maanake kura asingezipata..sidhani kama wajumbe wangeweza kumchagua mtu wa aina hiyo tena chama chenyewe CUF!..Hivyo binafsi nina imani kabisa kwamba viongozi wa juu wa CUF walikosa imani na mtu huyu yapo maswala mazito zaidi ya madai yaliyotolewa pengine hata hizo tuhuma za kuhamia Chadema ama yawezekama pia msimamo wake kuhusiana na swala la RA linapingana na mtazamo wa viongozi wa CUF kina Lipumba..
Kifupi mkuu wangu CCM wamekwisha ifanya kazi wanayotakiwa kuifanya kabla ya uvhaguzi wa mwaka 2010..Vyama vya Upinzani vimebakia dhaifu kabisa, kujitoa kwa Zitto, Lwakatare na wengine kibao watafuata wakiwa na sababu za msingi kabisa..
Mwisho wa picha nzima mkuu wangu - NJAA mkuu wangu njaa ndiye adui mkubwa wa Umaskini angalia kilio chote cha Lwakatare kimeishia wapi?..kalia na tumbo lake akatiwe japokuwa kidogo maanake haoni mbele (future) nje ya CUF pamoja na majigambo yote yaliyotangulia...
.....Lwakatare aliitisha mkutano huu ili kueleza wanachama wa CUF na wapenzi wake kisiasa nini kimetokea na kumlazimisha ajiuzulu uongozi wote ndani ya CUF....
...... Umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria ni watu wawili tu walionyoosha mkono kwamba aendelee kubakia CUF na wengine wote ......wanataka ahamie Chadema.
Suala la Lwakatare kupokelewa kwa shangwe, kuhutubia umati na kupewa maelekezo na wananchi akachambua na kufuata siyo habari kabisaaaa. Wao wanasema "Nosindika Atandamile" (Ni sawa na kumsukuma aliyechuchumaa) Siyo kama namkandia Mchukia Fisadi bali nawaweka sawa wasioijua Bukoba na mapenzi ya wanaBK kwa Entare, Lwakeupe, Lwaks, famously known as Lwakatare.
Wakati wengine wanajiua kwa Arsenal kufungwa na manchester, BK alijiua mtu eti kisa Kagasheki katangazwa mshindi. Huyu hata Lwaks mwenyewe hakumjua kwa sura. Visa vya kisiasa vimedudu miaka mitatu sasa utafikiri uchaguzi ni kesho. Harusi na misiba ya watu wa CUF imekuwa kama ni misiba ya kichama. Ujio wa Lwaks Bk siku zote imekuwa kama ujio wa mkombozi.
Bila shaka ndivyo ilivyokuwa mkuu junius.Hivi ndo stori uliyopata kwa source wako wa uhakika inavyosema,sasa hawa "wengine wote", wamo pia wa hivyo vyama 3 vikuu, ambao na wao wamenyoosha mikono yao kumtaka ahamie CHADEMA, wanachama wa SISI EMU walikuwapo na wao pia walimtaka ahamie CHADEMA? hii vp Mkuu...
Hakipendwi chama anapendwa mtu!😀
Lakini hapa hakipendwi Chama, anapendwa mtu😎
Bukoba hakipendwi chama, anapendwa mtu! Lwakatare ni bomu linaloelekezwa kuimaliza CHADEMA. Nikiwa mwanachama wa CHADEMA, nimeshuhudia ujio wa Guninita, Akwilombe, Chacha Wangwe na wengine ambao hatima yao tunaijua. Nimewahi pia kuwepo kwenye mmoja kati ya mikutano ya op. Sangara na kushuhudia wananchi maskini kabisa walivyoitikia wito wa viongozi wa chama kutoa michango ili kufanikisha ziara za operation hiyo. Wametoa michango ya sh 500/=, 1,000/= nk kila mtu kwa uwezo wake, huwezi amini kiasi kilichopatikana. Hawa ndio aina ya wanachama wanaohitajiwa na vyama vyetu hivi.
Huyu Lwakatare miongoni mwa sababu zinazomtoa CUF ni chama kushindwa kumlipa mafao na kushindwa kumlipia gharama za kesi yake. Kama kuna kiongozi wa CHADEMA ambaye yuko radhi kutoa pesa yake mfukoni kum-bail huyu Lwakatare, sina ugomvi. Lakini ikitumika hela ya chama inayotokana na ruzuku na michango ya wanachama maskini hawa wasio hata na uhakika wa mlo wa siku, I'll be the first member to raise hell.
Kuna member hapa JF anayejitambulisha kama Omutwale, ninayo kila sababu ya kuamini kuwa yuko karibu sana na Lwakatare. Kuna post moja kaandika kuwa ameongea na Lwakatare jinsi baadhi ya viongozi walivyojisajili kwa majina yao halisi lakini baadaye wakaishia kwa majina mengine na kumtaja mmoja kama Mr Dowans. Huyu ni kiongozi anayetaka mchango wake CUF utambuliwe kwa kuwa amekuwa huko tangu chama kikiwa CCW lakini anasahau kuwa huyu anayemkebehi kuwa ni Mr Dowans amechangia kwa kiasi kikubwa chama kinachonyemelewa hadi kukifikisha hapa kilipo. Zito amewahi kuandika kuwa kwa Kigoma CHADEMA ni zaidi ya chama. Wameondoka kina Kabourou lakini CHADEMA bado inapeta. Huko Tarime kuna watu walidhani wakimnunua Wangwe na hatimaye kuondoa uhai wake chama kingekufa, lakini chama ndio kwanza kinashamiri.
Nafahamu kuwa viongozi wengi wa CHADEMA ni members hapa. Jengeni chama huko Bukoba kama taasisi na si kutaka kubebwa mgongoni kwa Lwakatare. Mkishindwa kutimiza matakwa yake atawabwaga chini huyu.
Soma vizuri habari hiyo tena. Ondoa hapa uzushi wa kitu ambacho sikukiandika.
*Hakuna nilikoandika kuwa mkutano ulihudhuriwa na wana kafu peke yao.
*Wala sikusema wale wawili walionyoosha mkono against kafu walikuwa wana kafu.
Kama wewe una data za hakika weka thread yako usilete upotoshaji hapa. Hizi habari nimezipata kutoka kwenye zaidi ya source tatu kule Bukoba.
Hivyo vyote alikuwa navyo alipokuwa CUF, tena analala navyo kwake.Ameandaliwa kadi na sera za CHADEMA
Mimi naijua full story ya lwakatare.Alikuwa mpiga debe wa hali ya juu CUF,mwaka 2000 lipumba akamteua kuwa naibu katibu mkuu bara na baraza kuu la uongozi la chama chake likampitisha,then baada ya uchaguzi wa ndani ya chama wa CUF wa mwaka 2004 Lipumba aliposhinda alimteua kuwa naibu katibu mkuu tena.
Mwaka 2005 nyote mnakumbuka Chama chake kilipigana naye bukoba mjini lakini wakashindwa kwa balozi kagasheki(kagasheki alimshinda lwakatare kwa kura 130 tu)Baada ya kushindwa alifungua kesi ya kupinga matokeo hayo,yeye lwakatare ndiye aliyeongoza chama chake CUF katika chaguzi ndogo kadhaa za tunduru,mbeya vijijini na kwingineko(isipokuwa busanda).
Mwaka jana 2008 alikuwa kwenye mgogoro mkubwa na viongozi wake wa juu baada ya kutumia tshs 30,000,000(milioni thelathini) vibaya (alipewa pesa hizo akasimamie zoezi la daftari la wapiga kura kwa muda wa mwezi mzima) lakini akawashangaza wakubwa pale aliporudi baada ya wiki moja na kudai pesa zote zimekwisha huku ushahidi wa maafisa wa ngazi za chini alioenda nao ukionesha pesa zilizotumika kwa hiyo wiki moja hazizidi hata 5,000,000(milioni tano).Hiyo haikuwa mara ya kwanza,inasemekana huko nyuma alikuwa na rekodi chafu ya matumizi ya pesa ndani ya chama chake.
Inasemekana wakubwa walitaka kumuondoa mara moja lakini wakaona itaharibu sura ya chama chao,wakalimezea suala hilo na kukaa kimya kwani walijua bado miezi sita tu uchaguzi mkuu mwingine wa ndani ya chama ufanyike na walikuwa wakimtegea hapo.Uchaguzi mkuu wa chama cha CUF uliofanyika mwezi march mwaka huu ndio uliwaleta tena madarakani lipumba,machano na seif sharif na ndipo wakamtema lwakatare.
Inasemekana katika mkutano huo mkuu wa chama lwakatare alichaguliwa tena kuwa mjumbe wa baraza kuu la uongozi la taifa la chama hicho na tena alikuwa ana matumaini makubwa kwamba lazima atateuliwa kuwa naibu katibu mkuu kwani inasemekana aliwahi hata kutamka kwamba bila yeye tanzania bara chama hakipo.Siku ya uteuzi wa wakurugenzi na manaibu katibu wakuu wa zanzibar na tanzania bara ilikuwa siku moja baada ya mkutano mkuu wa chama.
Wajumbe wapya wa baraza walikutana ili kupokea uteuzi na kuukataa au kuukubali na mmoja wa wajumbe hawa alikuwa lwakatare huku akiwa anaamini kwa asilimia 100 kwamba lazima atateuliwa kuwa naibu katibu mkuu.Inasemekana alipata mshtuko mkubwa pale ambapo yalitajwa majina mawili kwa upande wa bara huku lake likiwa halimo na ndipo wajumbe wa baraza wote wakampigia kura JORAM BASHANGE.
Kutokana na mshtuko alioupata lwakatare palepale hakuchelewa alisimama na kutamka kikaoni hapo kwamba yeye anapinga uteuzi wa JORAM BASHANGE,alipoulizwa sababu ya kupinga akawa hana,na ndio kutokea hapo ikawa haieleweki;akaanza kuwaponda CUF na LIPUMBA na wengineo kwamba hawafai na wamekipeleka chama hicho kubaya.
Ikumbukwe kwamba lwakatare alikuwa anaongoza mambo yote ya utendaji wa chama na mikakati upande wa bara,na amekuwa katika kuongoza utendaji wa chama chake kwa miaka 10,iweje leo hii asipewe nafasi ya juu ndo anaanza kusema chama kimepoteza mwelekeo?
Nashauri ma-thinker wote walitizame suala hili vizuri bila ushabiki,iweje mtu anyimwe nafasi ya juu ndo anaona chama kibaya na waliomo hawafai?
Hivi tuseme leo hi lwakatare angekuwa ameendelea kuachiwa nafasi ya naibu katibu mkuu angetangaza kukihama chama chake?
Hivi leo hii mtu akinyimwa nafasi mahali ndio anahama? Viongozi wa namna hii sio wazuri hata kidogo.
Mimi nadhani ni yeye ndiye anajimaliza,ninamaanisha lwakatare anajimaliza mwenyewe- sote tunachojua ni kwamba anahitaji kulirudisha jimbo la bukoba vijijini mikononi mwake tena anakiri kwamba jimbo lile ni lake kwani alinyang'anywa na ccm mwaka 2005,if that is the case alihitaji kutulia ndani ya cuf na kuimarisha mtandao wake ili apate madaraka aliyokuwa anayahitaji.
Kwa kuhama kutoka cuf it means anaanza upya na chadema na najua ha taweza kuondoka na hata nusu ya wafuasi wa cuf bukoba mjini na hiyo itam-cost kwenye uchaguzi ujao kwani atamrahisishia kazi kagasheki iwapo cuf watamsimamisha mgombea mwingine anayekubalika.
Lakini pia napata bad news sasa hivi kwamba imebainika baadhi ya wabunge wetu wa CHADEMA wanachangishana ili kumuongezea nguvu lwakatare huko na tena jana usiku kulikuwa na kikao kati ya madiwani wa CUF walioko bukoba vs Lwakatare na viongozi wa chadema na madiwani wale wameahidiwa kupewa pesa za kampeni za uchaguzi mkuu ujao iwapo watang'oka CUF na kujiunga CHADEMA.
Habari hizi ni za uhakika na hivi ndio vyama vyetu vya upinzani.
Kama ripoti ni accurate (sadly I find myself prefacing most of my positions with that phrase, due to the obvious unreliability of our "press") huyu jamaa si kiongozi, ni mzugaji tu.