Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Nimefurahi umeamia Chadema chama cha Tanzania bara as wewe ni mbara, hao wa cuf wivu nawe waachie huko na kukuonea wivu wa kuwa mbara na cheo ulichokuwa nacho, hii inaonyesha kuwa wameona wafatilie zaidi ushindi zanzibar, na ndio kukuachia wewe mbali na kusahau kuwa umechangia mengi katika chama chao

Natumaini huko chadema wamekukaribisha salama, na weye kazania kuwa muongozi wa jimbo unalotoka aschana na vyeo

hivi chadema si ya wachaga au imechanganya?
 

Kitila,
Wonderful. Nimeweka post yangu kabla sijaona ya kwako na suprisingly zina mawazo yanayoshabihiana. Umesema kweli
Ubarikiwe mkuu.
 

Habari zilizovunjika sasa hivi huko VOA kwa sauti yake mwenyewe Lwakatare ametamka kuwa mkutano wa wanachama wote wa tawi lake la CUF-Kideta (uliomalizika muda si mrefu) wameamua kwa kauli moja kumruhusu bwana Lwakatare aachane na CUF na kuhamia CHADEMA ambako wataambatana naye.
Tehetehe.....Natoka kidogo kwenda kupata kahawa
 
Mkuu hilo la kukwambia muongo mi nakataa, sjalelewa katika malezi hayo dharau na bezo kwa watu,awe mkubwa au mdogo na nikiteleza huwa mwepesi kujirudi, ila nichokumbuka kusema kuwa habari ile ilikuwa na maswali mengi na nilihoji maksudi ili nipate more details tu.
Kuhusu CUF kufa na chadema kuwa mbadala wake, hilo naona uendelee kuota maana kama mngekuwa na ubavu tungekuoneni kule Busanda,lakini zilikuwa kelele tu za kukusanya watu mkawaonyesha helikopta yenu tu.
Halafu CUF(siwasemie maana ndo walivyo) hawamtegemei mtu kushawishi maendeleo yake hayo mambo ya KI CCM, na ndo maana wanaogopa kuruhusu wagombea binafisi kwa kuwa chama chao na chadema wanawafata naona, kinategemea watu, nkupe mfno, Zitto alipotangaza ku'ngatuka karibu mfe nyote kwa Presha, mnajua hakuna anaweza kusimama kuliltea tena bungeni jimbo la K/kaskazini.
CUF mtandao wake kule zanzibar umeshaimarika wakati wowote wanashika dola hili tukubaliane kwanza(chadema hamjafika huko kwenye maji makubwa), ujenzi wa chama Tzbara ni mipango ya muda mrefu inthe long run, Kwa hiyo usilanginishe chadema na CUF havifanani bana we!!Chama kina wabunge kumi hawafiki ndo ukakifananishe na chama chenye nguvu ya kushika dola wapi na wapi!
 

Ndio sababu wanataka kumuongeza na mhaya? hoja za chi chi emu zitakuwa zimefikia kikomo😀
 

Mna mpango wa kushika dola ipi?
Najua bado mnaota kuja na visingizio vya kuibiwa kura. Mbona siku zote mnaibiwa Zanzibar tu?
Mi sioni tatizo maana kafu=Zanzibar na Chadema=bara.
Lwakatare ni wa Bara anatakiwa kuwa Chadema.
Hiyo post ya Chibidu hapo juu umeisoma. Bukoba hamna kitu maana tawi zima linajigeuza chama cha chadema😀
 
Bado hutaki kukubali kuwa matandao wa wanangangari Tanzania ni mkubwa na ndo maana vyama vingine vinawaonea gere, havishi kujifananisha nao(kama chadema), CUF ipo kila kona ya Tanzania, chadema hata Rufiji hamjafika.
Ndugu zetu wa BK nawafahamu kwa biashara za namna hii kwa hiyo nanyie chadema mjitayarishe msije mka Mchacha Wangwe huyo Lwakatare siku atakayochagiza kuwakimbia.
 

Mkuu uishi kucheua pumba?

Hizo pumba zipo sehemu gani hapo juu?
 

Mkuu Mkandara,
Read between the line, Bukoba Mjini hakuna chama chochote kilichojiimarisha zaidi ya CCM. CUF unayoisikia huko Bukoba Mjini si kama ambavyo ungetegemea kuwa, Bukoba Mjini kuna wafuasi wa Lwakatare tu ambao wanaweza kuwa CHADEMA au hata NCCR- Mageuzi depending na huyo mfuasi yuko chama gani. Kama kweli Lwakatare alifanya kazi nzuri ya kuimarisha CUF Bukoba Mjini tunone kama akiondoka CUF itakuwa the same. Kwa muda wote aliokuwa Naibu Katibu Mkuu Bara alijiimarisha yeye mwenyewe Bukoba Mjini kwa wakati wote na kuacha chama hicho kikizorota sehemu zingine hapa bara, amechangia kuiua CUF bara.
 
Last edited:

Punda, hapa kuna mahali umesema ukweli na uongo mwingi pia.
*Ni kweli wapenzi wengi wa Lwakatare walitoka vyama mbali mbali Bukoba
*Si kweli kwamba Sisi Maf.... wana wanachama wengi Bukoba. Hii ni kujidanganya tu na kujipa moyo. Hapa imenidhihirishia kuwa huijui Bukoba.
*Si kweli kwamba kafu ina wanachama kidogo Bukoba. Nadhani kwa Bara ni kati ya maeneo yaliyo wanachama wengi.
*Si kweli kwamba Lwakatare alijiimarisha binafsi Bukoba, maana hata kafu wenyewe wamekili kuwa alifanya kazi nzuri katika kukiimalisha chama bara. Ni vizuri uelewe si kiongozi au mwanachama mmoja anayeweza kuleta mabadiliko katika chama. Always leaders works together to build a party. Hata Sisi Maf........ akijengwi na Kikwete, mbabaishaji Makamba na Mzee Pius pekee. Wala Chadema si kwamba kinajengwa na Mbowe na Zito au Dr Slaa pekee.
*Ni uongo kuwa Lwakatare amechangia kuiua kafu bara. Ningekubaliana na wewe kama ungeliyasema maneno haya mwaka jana na si kusubiri kaondoka kwenye chama mje na allegation hizi.
 

Junius,
Unanichekesha sana.
Ni wewe na Lipumba ambao mmesema siku zilizopita kuwa hata Lwakatare akitoka nyie Bukoba mmejijenga imara na hamna wasiwasi maana chama kiko imara BK.
Leo umejikanyaga kwa kusema Ndugu zetu wa BK nawafahamu kwa biashara za namna hii kwa hiyo.
Inaelekea mnazungumza bila kuijua Bukoba vizuri. Nimekwambia katika post yangu nyingine kwamba kama ilivyo Pemba. Kafu = Seif. Na Bk Kafu = Lwakatare. Still not believing?
 

Ukweli ndiyo huo na CUF kama haitafanya jitihada za wazi kuua dhana hii ya udini, kitabaki chama cha Pemba na pengine Rufiji (kutokana na maelezo ya Junius).

Amandla......
 
Lipumba alisema hayo rohoni akiwa anaumia na kwa lugha nyingine tuseme CUF WAMEFULIA!

W amempoteza mpiganaji wa kweli na alikuwa mtu anayeiunganisha sana CUF tz bara kufuta ile nadharia ya kwamba CUF ni chama cha Pemba na cha waislamu. CUF wamekosa mwelekeo na wana kashafa ya kufadhiliwa na kigogo wa CCM hawajaijibu. Lwakatare shukuru Mungu kakuonyesha njia ya kutokea.

Last time lipumba alisikika akitetea kwa nguvu ufisadi kwa madai ya ubaguzi wa rangi. Hapo sikumwelewa na inatufanya hata sometimes tuamini kwamba unapoendelea kusoma saaana busara zinapungua. Ajibu hoja za lwakatare

Eti wahindi ni wenzetu kasema nani? sisi tukienda India tunakirimiwa hivyo hivyo kama tunavyofanya huku. Aaache kutumia neno Prof halitendei haki.
 
Ukweli ndiyo huo na CUF kama haitafanya jitihada za wazi kuua dhana hii ya udini, kitabaki chama cha Pemba na pengine Rufiji (kutokana na maelezo ya Junius).

Amandla......


Give me a break! hayo mambo ya ku bandwagon kampeni za CCM. Kwa hiyo Chadema nayo ni ya wachaga? Mbona hiyo nafasi ya Lwakatare kaingia somebody Joram i hope sio muislam!

Huyo Kitila "kachanganyikiwa" na masuala ya Housegirl wake sasa anamwaga utumbo tu
 
Pundamilia huna hoja. Lwakatare alikuwa naibu katibu mkuu unasema kaua CUF bara, kwani katibu mkuu ambaye ndiye bosi wake anafanya kazi gani asifanye yeye kukijenga chama bara?
 
Khee. Hivi huo muda wenu lini utafika? Si uliishia pale ulipomalizika uchaguzi wa 2005. Ondokeni Bwana-mnagharibu bahati za CUF

Yani Lipumba angejua hata urais mwaka kesho angeacha asigombee. mie nashangaa hivi kwanini vyama vya upinzani hawataki kuwaachia wanachama wao wagombee urais kila mwenyekiti wa chama anataka na yeye agombee urais kama sisiem. Hawa wapinzani wana wanachama wazuri tena wengine ni wahadhiri vyuo vikuu hebu wawape nafasi nao wagombee urais.
 
Ukweli ndiyo huo na CUF kama haitafanya jitihada za wazi kuua dhana hii ya udini, kitabaki chama cha Pemba na pengine Rufiji (kutokana na maelezo ya Junius).

Amandla......
Nimesema CUF ipo kila kona Tanzania, chadema hata Rufiji hawajafika.
 
Bado chama kipo BK na ndo maana Mw'kiti akasisitiza kuwa Lwaks na aondoke lakini asikiharibu chama. Staki uamini kuwa hakutakuwa na chama BK baada ya Lwaks kuondoka, hata wale wawili uliosema hawakunyoosha mikono kumtaka ahame bado wapo.CUF ya Pemba na BK ni tofauti kabisa Pemba kinapendwa chama na si Maalim Seif na kwa taarifa yako tu hata leo Maalim Seif akisema anarudi CCM wapemba hatakuwa pamoja nae na watampiga marufuku kukanyaga Pemba na pengine hata akifa atazikwa Dodoma na si Mtabwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…