mwalukuni mchanyato
JF-Expert Member
- May 15, 2013
- 401
- 220
Ndugu wana Jf.
Nimeona nianze kuwa na wasiwasi na huyu mgeni wetu klabuni yaani namaanisha kocha wetu Lwandamina kutokana na kauli yake kuwa wachezaji wa kibongo ni legelege.Hii kauli naiona kama inaukakasi au kama si hivyo inamaanisha ni tusi au kejeli kwa kizazi hiki cha soka la Tanzania.
Nijuavyo Mimi wachezaji wote ni ngangari kwa kuwa ni wanamichezo na wanafanya mazoezi kila siku.Hivyo ulegelege hamna.Yeye alitakiwa kusema wachezaji wa kibongo wanahitaji mazoezi ya ziada kuwajengea stamina, hususan katika timu yake ya Yanga kwani ndio timu inayomuhusu zaidi.Kutoa majumuisho ya wachezaji wote ni kukosa busara na weledi na kuwakosea heshima watanzania kwa muono wangu.
Angekuwa muungwana kwa kauli hii,inabidi awaombe radhi wachezaji wa Tanzania kwa hili. Amepewa Yanga aifundishe na sio timu ya taifa,hivyo tathmini ya ulegelege aitoe kwa yanga na si kwa wachezaji wa vilabu vyote Tanzania.