LWAKATARE: Kuna unafiki CHADEMA

LWAKATARE: Kuna unafiki CHADEMA

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,410
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, WILFRED LWAKATARE amesema kuwa siasa za chuki na majungu ndani ya chama hicho zimetawala hali inayokwamisha harakati mbalimbali za kisiasa za chama hicho hadi kufikia kusalitiana hatua iliyofanya hata mipango mbalimbali kukwama. Alitolea mfano wa video aliyorekodiwa kuwa ililenga kumuumbua yeye.

Aidha taarifa za ndani za chama kutolewa nje kwa maadui wa CHADEMA kisiasa nyingi zinatolewa na viongozi na wanachama wasio waaminifu.

Hayo aliyasema wakati wa Mkutano na wanachama wa chama hicho uliofanyika Juni 19, 2013 kwenye Viwanja vya mashujaa maarufu kwa jina la Mayunga mjini Bukoba.

Aidha, Lwakatare aliwaambia wananchi waliokusanyika katika viwanja hivyo vya mashujaa kuwa nafasi yake na Ukurugenzi wa Ulinzi na Usalama inamsaidia kuwagundua maadui wake.

SOURCE:Gazeti la FAHAMU, JUMANNE Juni 25 - Julai 1, 2013


View attachment 99510View attachment 99516View attachment 99517
 
Hawa wanasiaasa wanatuchanganya sana.

Sasa kama alishazungumza na Mbowe kuhusu unafiki ndani ya chama, kwanini aende kulizungumzia hilo tena kwenye mkutano wa hadhara? Au viongozi wa juu wa chama hawaelewani?

Kweli, kufikia ukombozi wa kweli ni mission.

CHADEMA imekuwa kama serikali ya CCM, viongozi wa juu wote chamani wanalalamika; Zitto analalamika, Lwakatare analalamika! Sasa nani atachukua hatua?
 
maana hata aliyemrekodi alikuwa 'mwana-cdm' na homeboy mwenzake, sasa akisema hivyo anakosea wapi!?
 
mtuhumiwa wa ulishaji sumu anapataje uhalali wa kuanza kutamba mitaani??
 
Dah, mbona lwakatare analalamika sana. Ni vema akatusaidia kutubainishia kirusi ndani ya chadema ambacho zitto alikiibua
 
kama kweli cdm mnania ya kuchukua nchi nilazima muwe wamoja otherwise mtakua wasindikizaji tu.
 
maana hata aliyemrekodi alikuwa 'mwana-cdm' na homeboy mwenzake, sasa akisema hivyo anakosea wapi!?
Kumbe ndo maana ile ziara yake mikoani ilifutwa kwa vile aliona kuwa iliandaliwa kinafiki. Chadema bana!
 
Kwa hiyo ina maana hana haki ya kutoa maoni yake?
atulie sasa mana kuhtuhumiwa ni kuhusishwa, utakaposhinda kesi ndio unaweza kuwa na ujasiri wa kuongea, saivi bado ana hadhi ya kulisha watu sumu
 
Kumbe Lwakatare aliuzwa na viongozi wa Chadema, leo hii ndiyo umejua, unacheza na kaskazini wewe.
 
Back
Top Bottom