Lwakatare aachiwa huru kisha kukamatwa hapo hapo kwa kosa lingine

Hakimu kamuachia huru polisi wamemkamata hawajui kosa lakini wamesema watatafuta/kuchunguza kama anamakosa
Hahahahahaha hii ndo nchi polisi wanamkamata mtu hawajui kosa lakini watamtafutia kosa
...what happen to work done
when net force is zero?...
 
Never before in my life history has ever there such a noble and pressing task,
The accomplishishment which must be the common course
No sucrifise is too great no burden is too heavy for the achievement of our goal
Let us fight for revolution in a solid and militant chain and nothing under the sun will prevent our ultimate victory!2015 Yes!
 
Makubwa haya! Kila siku unanikashifu kuwa nimekithiri kwa matusi leo unanivika kilemba cha ukoka ili...............

Acha mbwembwe wewe muhaya wa katoma mbona threads zako zote ukiandika unanitag?? Kwahiyo unataka ukiandika pumba mimi nitikise kichwa tu bila kukuhoji? Ah wapi bana hiyo haitatokea.

We tiririka tu hata uki assume kwamba aliyekutaka ufafanuzi ni zemarcopolo poa tu.
 
Kwa hiyo mkuu, inabidi wamsikilize aliyewatuma kumkamata ili awaambie aina ya mashtaka mapya siyo? very sad.

Ofcose inabidi wamsikilize aliyewatuma huku wakiendelea kuchimba kwenye mabook ya sheria kuona wanaaccomodate vipi hizo concerns za mtawala
 
Wakuu,
Kuna Mambo Ma Kuu mawili, Kufutwa na Dhamana, haya yanakinzana, Binafsi nahitaji Mtu mwenye Full Info aje atutoe Gizani
Kabla wengine hatujaendelea Kuagiza More Tusker Barid Maofisini Mwetu...

Moja

Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Muganyizi Lwakatare,
muda huu ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
baada ya mashitaka yote yaliyokuwa yanamkabili kufutwa na muda huohuo kukamatwa tene na kufunguliwa mashitaka mengine.

Source
http://bloggers.com/post/breaking-news-lwakatare-aachiwa-huru-na-kukamatwa-tena-12228103


Nyingine ni Hii



Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi kwa siku 6
kwa tuhuma za uchochezi lakini akakamatwa tena muda huo huo kwa tuhuma za ugaidi na kutakiwa kupelekwa ngazi ya
juu ya Mahakama kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya ugaidi

Source

http://audifacejackson.blogspot.com...-lwakatare-aachiwa-huru-na.html#ixzz2O57kPt1V


My Take

Ma Kamanda Mikael P Aweda , Tumaini Makene, Ben Saanane, hebu fuatilieni hii issue kwa undani then tupeni jibu la kueleweka, Wengine tushaanza kufungua Champaign tayar kusherehekea Aibu ya CCM.
Please hebu leteni habari za kueleweka ili kama vp nistopishe order ya Tusker Barid niliyomuagiza huyu Mdada Ofisini Kwetu Hapa.
 
Hahaaa nimegundua kitu kimoja kuwa hatujui sheria hivyo ni vyema tukafuata ushauri wa thatha kuwa tupitie sheria ingawa naye hajui sheria wala wajibu maana mwenziye kauliza swali zuri kajibiwa apitie sheria. Ni kweli kilichowekwa hapa hakijaeleweka maana Lwakatare kwa makosa aliyoshtakiwa nayo angepaswa kuomba kupewa dhamana na ndicho mawakili wake walichokuwa wanakihangaikia toka akamatwe. Tuambiwe ukweli kuwa amekubaliwa dhamana akaachiwa kwa masharti ya dhamana akadakwa kwa kosa jingine na siyo kuwa ameachiwa moja kwa moja kana kwamba makosa aliyosomewa alionewa tu la hasha. Kwa kosa lake la ugaidi mkicheza mnaofurahia na kuona ni jambo la kukinufaisha chama fulani na kukishusha chama fulani kama ilivyokuwa kwa Obote na wenziye waliomdanganya utashangaa kuona wamarekani wanaingia kati mwisho ndugu yetu gaidi anayechipukia kwa kudanganywa na chama anaishia guantanamo.

Tuache siasa chafu huku tukijificha kwenye mwavuli wa Demokrasia. Tanzania na watu na mali zake ziwe kwanza siyo vyama na madaraka.

.
Marekani na mimi mtanzania tunafahamu fika kuwa hakuna gaidi mkristo. Wote wanatoka ule upande mwingine. Labda sisiem waliolewa madaraka kwa sasa watengeneneze ugaidi wa kikristo na ndicho kitu ninachokiona kwa sasa.
.
 
MMH mimi naamini sasa nchi yetu imefikia kwenye high peak ya udikteta,watabiri wa mwanzo walisema kikwete atapanda juu ya maiti za watanzania ili tu awe raisi na abaki kuwa raisi na aweze kuwaachia wale watakaolinda maslahi yake kuna tetesi mgombea wa CCM 2015 ni Salma Kikwete na kwa kiwango kikubwa walivyoset majambo atashinda ngojeeni raisi wa kwanza mwanamke Salma Kikwete ndio maana yote haya yanatokea kupisha njia
 
Nilipoleta uzi hapa juu ya kutofautiana kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) na Polisi juu ya uwepo wa ushahidi na ni mashtaka gani hasa ashtakiwe nayo Alfred Muganyizi Lwakatare,Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA,wapo walionibeza. Lakini,walikuwepo walioniamini na kuchangia mada ipasavyo.

Leo,Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumetokea jambo jipya. Si jipya kwa kuachiwa kwa dhamana na kukamatwa tena kwa Lwakatare.La hasha. Lipo jipya hapa.Twende taratibu.

Alfred Muganyizi Lwakatare pamoja na Ludovick Joseph Rwezaura walifikishwa Mahakamani hapo Jumatatu iliyopita na kusomewa mashtaka manne: moja la kula njama na matatu ya ugaidi.Walisomewa mashtaka hayo kwa Sheria mbili tofauti. Ya kwanza ilikuwa ni Kanuni ya Adhabu,Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania ambayo ilitumika kwa shtaka la kula njama.Sheria ya pili ni Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002 iliyotumika kwa makosa matatu ya ugaidi.

Baada ya kusomewa makosa manne(matatu kwa wote na moja kwa Lwakatare pekee),Mawakili wanaomtetea Lwakatare: Profesa Abdallah Jumbe Safari,Peter Kibaatala na Tundu Antipas Mughwai Lissu walitoa hoja za kumwombea dhamana mteja wao,Alfred Lwakatare. Wakili Mkuu wa Serikali Kanda ya Dar es Salaam,Rweyongeza alipinga vikali. Baada ya mabishano ya kisheria,leo ilipangwa kuwa siku ya Mahakama kutoa uamuzii juu ya hasa ombi la dhamana.Leo,Wakili wa Serikali aliomba ridhaa ya kuondoa makosa matatu ya ugaidi dhidi ya washtakiwa na kubaki na moja la kula njama. Hakimu akaridhia.Hati ya Mashtaka ikabaki na kosa moja la kula njama ambalo lina dhamana. Hakimu akatoa dhamana kwa washtakiwa wote kiurahisi kabisa. Kosa la kwanza! Leo haikuwa siku ya kuzungumziwa kesi. Iweje Wakili wa Serikali awasilishe maombi hayo na uamuzi mwingine nao ufanyike?

Alichotakiwa kukifanya,kwa ufinyu wangu wa kuelewa,ni kuwasilisha ombi lake la kurekebisha hati ya mashtaka na kuomba ahirisho hata fupi tu.Hajafanya hivyo. Wakili wa Serikali amefanya kosa kisheria na kiuhalisia.

Tena,Lwakatare alikamatwa tena kwa makosa ya ugaidi ili eti akashtakiwe mahakama stahiki ambayo ni Mahakama Kuu. Kwani Mahakama ya Hakimu Mkazi kama Kisutu ni mara ya kwanza kuanza kushughulikia kesi ambazo haziruhusiwi kusikilizwa hapo? Mbona hata ya Papaa Msofe,tena ya mauaji,inashughulikiwa Mahakamani hapo hapo?

Hii ni danganya toto na ni mbinu za Ofisi ya DPP kupoteza muda na kujipanga. Kuachiwa huru (kwa kufuta mashtaka) halafu kukamatwa tena kwa makosa yale yale na katika Mahakama ile ile si suala jipya.Wapo hata walioachiwa huru kabisa na kukamatwa tena.Lina ruhusa kisheria. Lakini,si kama ilivyofanyika leo. Leo ulikuwa kama mchezo wa kuigiza. Makosa yale yale,Mahakama ile ile;upya uko wapi sasa? Au Hakimu?

Kosa la kwanza la DPP ni kuchanganya makosa ya kutoka sheria mbili tofauti na kuyapeleka Mahakama moja huku akijua fika kuwa atayagawanya makosa hayo na Mahakama zake. Kosa la pili ni kuwasilisha maombi siku ya uamuzi. Ni vyema makosa kama haya yasijirudie tena ili haki itendeke na ionekane inatendeka.

DPP ameteleza;amefuta jibu na kuandika tena lile lile. Tusubiri tarehe 3/4/2013 tuone filamu hii itakavyoendelea.

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam


 
Puleeez, give me a break

Ngoja nikutafsirie basi, heading imebadilishwa, sio ilivyokuwa mwanzo wakati nachangia mara ya kwanza, happy?

Heading imekaa sawa hata kama mtu akichangia kesho. Mahaka,a imemuachia huru kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili polisi wamemkamata tena kwa kosa ambalo bado halijajulikana.Labda uniambie hufahamu kiswahili sawasawa, ukiwa unajua kukosoa na kutoa lugha isiyofaa kubali pia kukosolewa, haukuzungumzia muda wa kuchangia umezungumzia heading hii ina maana hata miaka kumi ijayo kwako haeding iyakuwa haijakaa sawa kama muda umekubadilisha mawazo, omba msamaha kubali kuwa ulipotoka huo ndio uungwana kwani ulishaita watu wajinga. Usipige pige na kutapatapa simama katika hoja yako ya heading kutokuwa sawa, maana imekuwa kawaida kubadilisha au kupindisha hoja, unapoenda mtaani ukiwamtupu basi lazima ujiandae,
 
Wakuu,
My Take

Ma Kamanda Mikael P Aweda , Tumaini Makene, Ben Saanane, hebu fuatilieni hii issue kwa undani then tupe jibu la kueleweka, Wengine tushaanza kufungua Champaign tayar kusherehekea Aibu ya CCM.
Please hebu lete habari za kueleweka ili niagize Tusker Barid hapa Ofisini

Ni viongozi wa chadema kuitisha press conference wa share na umma habari hii na kwa kiutaalamu wa kisheria watueleze mbinu chafu ya chama kongwe na washirika wake polisi na Usalama wa taifa watudadavulia coalition ya hao watatu wanavyolinda udhalimu na wizi wa raslimli zetu na ukopaji wa fedha nyingi mpaka kwenye mabenki ya kibiashara ili mradi kushusha hadhi ya nchi na kuiweka rehani kwa kikundi cha wachache wasio zidi 20 wanaoamua mustakabali wetu wote
 
Ndugu yangu mwenye uelewa mkubwa wa sheria hebu tuambie nini kinaweza kuwa kimetoke? Je inawezekana ameeachiwa kwa dhamana ndipo polisi wakaja tena kumkamata kwa kosa lingine? Kwa hiyo kama kweli aliachiwa huru kwa sababu yoyote ile utakuwa tayari kuja hapa na utaalamu wako wa sheria kutuambia nini ambacho ulikuwa hukijui kuhusu sheria?
kwenye red ndipo kwenye majibu, sawa mdogoangu.....??? aliachiwa kwa dhamana, ila akadakwa kwa polisi, kwa tuhuma za ugaidi....Mind you, kisutu haina hadhi ya kusikiliza kesi za ugaidi, hivyo haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa mtuhumiwa wa kosa la ugaidi....dhamana waliyompa ni ile ya yale makosa matatu...umenielewa???
 
ngoma bado mbichi. niliandika tangu juzi kuwa kesi ya ugaidi haiwezi sikilizwa kisutu. lwakatare bado ataendelea kusota. alipewa dhamana ya mashtaka matatu lkn hili la ugaidi likagonga mwamba.

ngoma inapelekwa mahakama kuu sasa

chezea mahakama ww!
 
Back
Top Bottom