Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,915
- 30,259
- Thread starter
- #101
Mag...Mohamed Said, huchoki kusema uongo? Aliyeasisi na aliyekuwa Rais wa kwanza wa AA mwaka 1929 alikuwa ni Mwalimu Cecil Matola au unataka tukumbushane?
Mohamed Said, uongo mwingine huu. Hebu elezea...Abdul Sykes aliupataje U-President wa TAA 1951? Alichaguliwa na nani katika kikao gani? Yawezekana alikaimu hiyo nafasi baada ya bosi wake, Dr Vedasto Kyaruzi kupewa uhamisho na Wakoloni.
Mohamed Said, duh! Hata aibu hakuna. Eti TAA ilikufa baada ya Nyerere kuchaguliwa kuwa kiongozi wake mkuu (President). Huu uzushi unautoa wapi? Believe this and you will believe anything (James Hadley Chase!)
Naomba usiturudishe katika historia ya nyumba walikokuwa wakikutana waasisi wa AA mwaka 1929!
Mbona umeghadhibika?
Huu ni mjadala wa historia ambayo hakuna yeyote aliyepata kuijua ila wenyewe waliohusika na kuunda TANU.
Kwa nini ughadhibike na kuandika kwa ufedhuli?
Mbona mie naandika taratibu?
Ikiwa huamini niyasemayo kwangu si tatizo.
Bakia na hicho unachokiamini.
This is for Real (James Hadley Chase).