Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,847
- 30,189
LUTHERAN PRIMARY SCHOOL MOSHI KAMA ILIVYOKUWA 1950s NA SASA
Nilianza darasa la kwanza mwaka wa 1958 kwenye jengo hilo hapo chini lililokuwa ni Kanisa la Kilutheri.
Baada ya miaka mingi nilifika Moshi kuangalia pale nilipoanza shule.
Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 20 December, 1986 na nikapiga picha hiyo ya kwanza nimesimama kwenye mlango wa kuingilia kanisani ambako ndiko nilipoanza kusoma.
Ile piano ambayo Mwalimu Paul alikuwa akipiga na sisi wanafunzi tukiimba ''hyms,'' ilikuwa pale pale ilipokuwa mwaka wa 1958.
Piano ile ilirejesha kwangu kumbukumbu nyingi pamoja na nyimbo nilizojifunza pale na zote nikizikumbuka kama vile niliziimba jana ---''Damu ya Kondoo,''Ni Nani Aliyetuumba ni Mungu Mwenyewe,'' ''Ewe Mwezi ni Rafiki Yangu,'' ''Tunamsifu Baba Marehemu Kingi George.''
Kuzunguka kanisa kulikuwa na bustani nzuri ya maua ya rangi tofauti na kulikuwa na ukoka uliopandwa kiasi huoni ardhi.
Mwalimu Paul alikuwa mtu mzima na ndiye aliyeniandikisha shule nikiwa na miaka sita.
Alikuwa siku zote akivaa pama hata darasani.
Alikuwa akitufundisha kuwa watu wakifa wanakwenda mbinguni.
Miaka miwili tu mama yangu alikuwa amefariki na ndiyo sababu ya mimi kuchukuliwa na mama yangu mdogo na kujanae Moshi alipokuwa akifanya kazi katika Nursing Home ya Mgiriki Dr. Georgedis nianze shule.
Hospitali hii ilikuwa makhsusi kwa Wazungu tu.
Kwa kuwa Mwalimu Paul alikuwa akitufunza kuwa watu wakifa wanakwenda mbinguni nilikuwa na kawaida ya kukaa kwenye ukoka kwenye bustani peke yangu na wakati mwingine nikilala chali kuangalia juu mawinguni nikitegemea kumuona mama yangu.
Namkumbuka mwanafunzi mwenzangu umri sawa na mimi akiitwa Njuguna wakati mwingine akija kukaa na mimi pale bustanini.
Njuguna alikuwa mzuri na nikipenda sana awe karibu yangu.
Miaka ilisogea na pamoja tukawa wakubwa kiasi miaka miaka 12 hivi.
Siku moja kwenye fete alipewa microphone akaambiwa aimbe nyimbo yoyote aitakayo.
Junguna akaimba, "Oh Carol," ya Neil Sedaka kwa ustadi mkubwa sana.
Kila niisikiapo nyimbo hii humkumbuka Njuguna.
Njuguna ametangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita.
Namkumbuka Hidaya yeye tukifuatana pamoja kwenda shule.
Siku moja nikauliza kama Hidaya yuko mjini.
Nikafahamishwa kuwa amefariki miezi michache iliyopita.
Alikuwa nurse Hospitali ya Mawenzi.
Majonzi yalinijia ingawa tulipoachana sote tulikuwa watoto wadogo labda wa miaka 10.
Miaka imekwenda wapi?
Picha hiyo ya pili nimeipiga tarehe kama hii ya leo mwaka jana nikapiga sehemu ile niliyosimama mwaka wa 1986 miaka 36 iliyopita.
Kanisa ambalo ndani yake ndiko lilipokuwa darasa langu la kwanza pamebadilika sana kama inavyoonekana kwenye picha.